WAFUGAJI NA WAKULIMA WAASWA KUTOCHUKUA SHERIA MKONONI

Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwa kushirikiana na Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa( OWM- TAMISEMI) zimetoa pole kwa wahanga wa migogoro ya wakulima na wafugaji Wilayani Tunduru mkoni Ruvuma iliyosabahisha vifo vya watu nane  na wengine kadhaa kujeruhiwa tukio lililotokea mwishoni mwa mwezi septemba 2025.

Akizungumza na Wananchi wa Tarafa ya Nalasi Wilayani Tunduru Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Balozi Dkt. Bashiru Ally Kakurwa amewaasa wafugaji na wakulima nchini kuacha kujichukulia sheria mkononi hasa pale inapotokea changamoto ya kuingilia matumizi ya ardhi.

“Nimekuja hapa na Mheshimiwa Naibu Waziri wa TAMISEMI kwanza kuwapa pole wote walifariki kutokana na migogoro huo uliotokea mwenyezi Mungu Awarehemu , lakini niwaase ndugu zangu wafugaji na wakulima mjishichukulie sheria mkononi , toeni taarifa mapema kwa mamlaka za kisheria” alisema Mhe. Balozi Dkt. Bashiru.

Aidha, Dkt. Bashiru amesema Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Wizara ya Ardhi na Ofisi ya Waziri Mkuu Tamisemi zimeanza kupanga mpango wa matumizi bora ya ardhi kwa kutenga maeneo ya malisho ya mifugo hatua itakayopunguza migogoro ya wakulima na wafugaji nchini.

Naye, Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Dkt. Jafari Rajabu Seif amewataka watendaji wa halmashauri nchini kutenda haki kwa wananchi na kutokuwa chanzo cha migogoro ya wafugaji na wakulima.

Mbunge wa Jimbo la Tunduru Kusini Eng.  Fadhili Chilombe amepongeza hatua za serikali za kutenga vitalu kwa ajili ya wafugaji na kuomba vitalu hivyo viwezeshwe miundombinu ili wafugaji waanze kuitumia kwa ajili ya shughuoi za ufugaji.



Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Balozi Dkt. Bashiru Ally Kakurwa  akizungumza na wananchi wa Tarafa ya Nalasi Wilayani Tunduru alipofika kutoa pole kwa wahanga wa madhila ya migogoro ya wakulima na wafugaji Machi 07, 2026.

Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Dkt. Jafari Rajabu Seif akitoa maelekezo kwa watendaji wa halmashauri kuacha kuchochea migogoro ya wakulima na wafugaji  wakati wa mkutano wa hadhara Tarafa ya Nalasi Wilaya ya Tunduru iliyofanyika leo Machi 07, 2026.

Wananchi wa Tarafa ya Nalasi Wilayani Tunduru wakifuatilia Mkutano wa Waziri wa Mifugo na Uvuvi na Naibu Waziri wa Ofisi ya Waziri Mkuu - TAMISEMI walipofik kutoa pole kwa wahanga wa madhila ya migogoro ya wakulima na wafugaji Machi 07, 2026.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

LESENI, VIBALI VYA MAZAO YA MIFUGO NA VYAKULA VYA SAMAKI KUTOLEWA KWA NJIA YA KIELEKTRONIKI

DKT. MHEDE AONGOZA ZOEZI LA UCHANJAJI WA MIFUGO MKOANI IRINGA, WAFUGAJI WAPONGEZA HATUA YA SERIKALI

SERIKALI KURASIMISHA BIASHARA YA MABONDO