TASFAM YAHAKIKI MAENEO YA MIUNDOMBINU

Wataalamu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi, kupitia Mradi wa Uendelezaji wa Rasilimali za Uvuvi na Ukuzaji Viumbe Maji (TASFAM), wanafanya ziara ya kikazi katika mikoa mitano ya utekelezaji wa mradi huo ili kuhakiki umiliki na kupata mahitaji ya maeneo patakapojengwa miundombinu mbalimbali ya kukuza sekta ya uvuvi.

Mikoa hiyo ni Tanga, Dar es Salaam, Pwani, Lindi na Mtwara, ambapo katika Mkoa wa Mtwara wataalamu hao wamefanya ziara kuanzia Tarehe 5 hadi 8 Mwezi Machi 2026, katika Halmashauri ya Manispaa ya Mtwara Mikindani kuhakiki eneo patakapojengwa mwalo wa kupokelea samaki katika Mtaa wa Miseti kata ya Chuno pamoja na Halmashauri ya Mtwara Vijijini, Mtaa wa Naumbu Kusini, Kata ya Naumbu patakapojengwa ghala la kuhifadhia mwani.

Aidha, wakiwa katika Halmashauri ya Mtwara Vijjini wametembelea Kituo cha Hifadhi ya Bahari ya Ghuba ya Mnazi na Maingilio ya Mto Ruvuma ambacho kipo chini ya Hifadhi za Bahari na Maeneo Tengefu (MPRU) katika Kijiji cha Ruvula Kata ya Msimbati, ambapo patajengwa gati kwa ajili ya kuegesha boti za MPRU na wageni wa hifadhi, kituo cha utafiti na malazi kiikolojia, pamoja na kituo cha taarifa kitakachojumuisha ukumbi wa mikutano, maktaba na sehemu ya maonesho.




Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

LESENI, VIBALI VYA MAZAO YA MIFUGO NA VYAKULA VYA SAMAKI KUTOLEWA KWA NJIA YA KIELEKTRONIKI

DKT. MHEDE AONGOZA ZOEZI LA UCHANJAJI WA MIFUGO MKOANI IRINGA, WAFUGAJI WAPONGEZA HATUA YA SERIKALI

SERIKALI KURASIMISHA BIASHARA YA MABONDO