SERIKALI KUTOA PIKIPIKI 200 KUIMARISHA HUDUMA ZA UGANI

Na. Stanley Brayton

Wizara ya Mifugo na Uvuvi imezamiria kuimarisha huduma za Ugani kwa kununua pikipiki 200 ambazo zitasaidia kuongeza ufanisi katika utendaji kazi wa maafisa Ugani wa Mifugo na Uvuvi katika kutekeleza majukumu ya kuwahudumia wananchi ili kuongeza uzalishaji katika sekta hizo.

Akizungumza Katibu Tawala Msaidizi Sehemu ya Uchumi na Uzalishaji Mkoa wa Pwani, Ndg. Shangwe Twamala, wakati wa hafla ya ufunguzi wa mafunzo rejea kwa maafisa hao kutoka Kanda ya Kati Mashariki leo Machi 11, 2026, mkoani Pwani, Ndg. Twamala amesema pikipiki hizo 200 zitasambazwa kwa maafisa ugani wote nchini.

"Wote tunashuhudia utekelezaji huo na hatua za Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwa kuwa miongoni mwenu wapo wataalam wa ugani ambao wameshapatiwa vifaa pamoja na mafunzo mbalimbali yakiwemo haya mafunzo ya leo ambayo nimepata nafasi ya kuyafungua kwa Kanda ya Kati Mashariki.” Amesema Ndg. Twamala

Aidha, Ndg. Twamala amebainisha kuwa Wizara ya Mifugo na Uvuvi inaendelea kutekeleza majukumu mbalimbali ikiwemo kampeni ya chanjo na utambuzi wa mifugo, ukusanyaji wa mapato kwa sekta za mifugo na kutoa mafunzo kwa wanajamii katika Halmashauri zote nchini.

Vilevile, Ndg. Twamala amewataka maafisa ugani kuongeza kasi katika utekelezaji wa majukumu yao, na ametaka wajikite katika kuboresha utoaji wa taarifa sahihi na kwa wakati, kusambaza teknolojia bora na bunifu zinazoongeza tija, kuimarisha elimu kwa wafugaji na wavuvi, pamoja na kutoa ushauri wa kitaalamu unaozingatia viwango na miongozo iliyopo.

Akizungumza kwa Niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Naibu Msajili wa Baraza la Veterinari Tanzania (VCT), Dkt. Obed Nyasebwa ameweka wazi kuwa mafunzo hayo ni mwendelezo wa hatua zinazochukuliwa na wizara za kuwajengea uwezo wataalam wa mifugo na uvuvi katika kutekeleza majukumu ya utoaji wa huduma za ugani nchini kama ilivyoainishwa katika Sera, Sheria na Kanuni za Mifugo.

Pia, Dkt. Nyasebwa amesema kupitia mafunzo hayo wataalam watapata nafasi ya kujadiliana kwa kina juu ya changamoto na utatuzi wake ili kuweza kuboresha sekta zote na mifugo na uvuvi.

Kwa upande wake, Afisa Mifugo Mkuu kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu - TAMISEMI, Ndg. Elisante Qadwe amewapongeza maafisa ugani wa mifugo na uvuvi kwa kuhudhuria kwa wingi katika mafunzo hayo yenye lengo la kufanya mapinduzi makubwa hasa utendaji kazi unaozingatia matumizi ya sayansi.

Naye, Mkuu wa Idara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga, Bi. Anna Kiria ameiomba Wizara ya Mifugo na Uvuvi kuendelea kutoa mafunzo hayo kwani yatazidi kuimarisha sekta na kuinua hali ya utendaji kazi wa maafisa ugani.

Mgeni Rasmi ambaye ni Katibu Tawala Msaidizi Sehemu ya Uchumi na Uzalishaji, Ndg. Shangwe Twamala (aliyekaa mstari wa mbele katikati), akiwa katika picha ya pamoja na Maafisa wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi, baada ya Hafla ya Ufunguzi wa Mafunzo Rejea kwa Maafisa Ugani wa Mifugo na Uvuvi Nchini Kanda ya Kati Mashariki, yaliyofanyika katika Ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga, Machi 11, 2026 Pwani.
Mgeni Rasmi ambaye ni Katibu Tawala Msaidizi Sehemu ya Uchumi na Uzalishaji Mkoa wa Pwani, Ndg. Shangwe Twamala, akihutubia Maafisa Ugani wa Mifugo na Uvuvi, pamoja na wadau wa Sekta hizo, katika Hafla ya Ufunguzi wa Mafunzo Rejea kwa Maafisa Ugani wa Mifugo na Uvuvi Nchini Kanda ya Kati Mashariki, yaliyofanyika katika Ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga, Machi 11, 2026 Pwani.

Mwakilishi wa Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi, ambaye ni Naibu Msajili wa Baraza la Veterinari Tanzania (VCT), Dkt. Obed Nyasebwa, akielezea lengo la Mafunzo, katika Hafla ya Ufunguzi wa Mafunzo Rejea kwa Maafisa Ugani wa Mifugo na Uvuvi Nchini Kanda ya Kati Mashariki, yaliyofanyika katika Ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga, Machi 11, 2026 Pwani.

Afisa Mifugo Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Ndg. Sebastian Shilingalila, akitoa neno la Utangulizi kwa Maafisa Ugani wa Mifugo na Uvuvi, pamoja na wadau wa Sekta hizo, katika Hafla ya Ufunguzi wa Mafunzo Rejea kwa Maafisa Ugani wa Mifugo na Uvuvi Nchini Kanda ya Kati Mashariki, yaliyofanyika katika Ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga, Machi 11, 2026 Pwani.

Afisa Mifugo Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu - TAMISEMI, Ndg. Elisante Saktay Qadwe (wa kwanza kulia), akielezea Mada inayohusu Ugatuzi wa Madaraka kutoka Serikali Kuu kwenda Mamlaka ya Serikali za Mitaa (MSM), katika Hafla ya Ufunguzi wa Mafunzo Rejea kwa Maafisa Ugani wa Mifugo na Uvuvi Nchini Kanda ya Kati Mashariki, yaliyofanyika katika Ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga, Machi 11, 2026 Pwani.

Mkuu wa Idara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga, Bi. Anna Kiria (wa kwanza kulia), akichangia mada, katika Hafla ya Ufunguzi wa Mafunzo Rejea kwa Maafisa Ugani wa Mifugo na Uvuvi Nchini Kanda ya Kati Mashariki, yaliyofanyika katika Ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga, Machi 11, 2026 Pwani.

Picha ni Maafisa Ugani wa Mifugo na Uvuvi, wakisikiliza Mada iliyowasilishwa na Afisa Mazingira wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Bi. Beatrice Temba (hayupo pichani), inayohusu Utunzaji wa Mazingira kwa Ufugaji unaostahimili mabadiliko ya tabianchi, katika Hafla ya Ufunguzi wa Mafunzo Rejea kwa Maafisa Ugani wa Mifugo na Uvuvi Nchini Kanda ya Kati Mashariki, yaliyofanyika katika Ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga, Machi 11, 2026 Pwani.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

LESENI, VIBALI VYA MAZAO YA MIFUGO NA VYAKULA VYA SAMAKI KUTOLEWA KWA NJIA YA KIELEKTRONIKI

DKT. MHEDE AONGOZA ZOEZI LA UCHANJAJI WA MIFUGO MKOANI IRINGA, WAFUGAJI WAPONGEZA HATUA YA SERIKALI

SERIKALI KURASIMISHA BIASHARA YA MABONDO