KAMATI YA BUNGE YAPONGEZA UTEKELEZAJI WA MIRADI YA TAFICO, CHANJO YA MIFUGO
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara, Kilimo na Mifugo imeipongeza Serikali kupitia Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwa kutekeleza miradi ya maendeleo inayolenga kuongeza uzalishaji na mchango katika pato la taifa.
Mwenyeketi wa Kamati hiyo Mhe. Deoudatus Mwanyika ametoa pongezi hizo leo Machi 10, 2026 Bungeni Dodoma kwa niaba ya wajumbe baada ya kupokea taarifa ya utekelezaji wa miradi ya Shirika la Uvuvi Tanzania (TAFICO) na Kampeni ya Kitaifa ya Chanjo na Utambuzi wa mifugo ilizinduliwa Juni 2025.
“Kama kamati tunaipongeza wizara kwa kuelimisha wafugaji na jamii kwa ujumla kuhusu chanjo, zoezi hili lilikuwa na mvutano sana kutokana na ukosefu wa elimu lakini sisi kamati tulisema ni lazima chanjo ifanyike. lakini pia, tunapongeza kwa miradi ya meli za TAFICO kwa ajili ya uvuvi wa Bahari Kuu, kamati hii imelipigania sana suala hili” alisema Mhe. Mwanyika.
Awali akitoa taarifa ya miradi inayotekelezwa na TAFICO Afisa Mtendaji Mkuu wa Shirika hilo CPA Shaibu Matessa amesema jumla ya ajira za moja kwa moja elfu 13,049 zitazalishwa kutokana na miradi inayoendeshwa na TAFICO ambapo hadi sasa shirika hilo limenunu meli mbili za uvuvi wa Bahari Kuu kati ya meli tano zinazopangwa kununuliwa.
Kuhusu Kampeni ya Kitaifa ya Chanjo na Utambuzi wa Mifugo, Mkurugenzi wa Huduma za Mifugo Dkt. Benezeth Lutege amesema hadi kufikia Februri 2026 jumla ya mifugo 50, 215, 441 sawa na asilimia 65. 8 ya kuchanja mifugo 76, 323, 300 huku mifugo 2, 590,200 ikitambuliwa sawa na asilimia 15 ya lengo la kutambua mifugo 17,224,200 nchi nzima.





Maoni
Chapisha Maoni