NARCO YATAKIWA KUONGEZA UZALISHAJI MAZAO YA MIFUGO
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi Dkt. Edwin Mhede ameisisitza Kampuni ya Ranchi za Taifa Nchini (NARCO) kutekeleza maagizo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, wakati wa ufunguzi wa Bunge la 13 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na maelekezo ya Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Balozi Dkt. Bashiru Ally, ya kuleta ufanisi wa Kampuni hiyo na kuzalisha mazao yenye ubora katika sekta ya mifugo hapa nchini.
Dkt. Mhede ametoa rai hiyo leo Februari 05, 2026 Makao Makuu ya NARCO mjini Dodoma wakati wa kikao kazi cha utekelezaji wa maelekezo ya Waziri wa Mifugo na Uvuvi kuhusu utekelezaji wa maagizo ya Rais ya kuongeza ufanisi wa Kampuni hiyo katika kufanya mageuzi ya sekta ya mifugo.
“Kampuni hii inatakiwa iongoze kwa kuzalisha mazao ya mifugo yenye ubora, niwasihi tujitoe kwa nguvu zote katika kutekeleza maagizo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan pamoja na maelekezo ya Waziri wetu, Mhe. Balozi Dkt. Bashiru Ally” alisema Dkt. Mhede.
Aidha, ameitaka NARCO kushirikiana na Bodi ya Nyama Tanzania katika kusimamia ufanisi wa machinjio kuwa bora, kuongeza upatikanaji wa soko la biashara ya nyama ndani na nje ya nchi.
Vile vile Dkt. Mhede aliwahimiza watendaji wa NARCO kuongeza kasi katika kutekeleza majukumu yao kwa kuzingitia Dira ya Taifa ya Maendeleo ya 2050.




Maoni
Chapisha Maoni