MAPINDUZI SEKTA YA KILIMO, MIFUGO NA UVUVI KUKUZA UCHUMI WA KATI WA JUU

Serikali kupitia Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi iko tayari kushiriki kikamilifu katika utekelezaji wa Mpango Kabambe wa Mageuzi ya Shoroba za Kilimo, Mifugo na Uvuvi (AMP 2050) utakaosaidia kuchochea ukuaji wa uchumi wa kati wa juu kwa taifa.

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano wa uhamasishaji wa ukuzaji na uendelezaji wa shoroba za kilimo uliofanyika Februari 12, 2026 mkoani Singida, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Mhe. Rosemary Senyamwile, amesema lengo kuu la mkutano huo ni kujenga uelewa wa pamoja kuhusu mpango huo kwa wataalam wa mikoa na halmashauri, hususan kuhusu dhana ya shoroba za kilimo.

“Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan imeweka msisitizo mkubwa katika mageuzi ya sekta ya kilimo, mifugo na uvuvi kama injini ya kukuza uchumi wa taifa, kuongeza ajira na kuinua maisha ya Watanzania kwa ujumla,” amesema Mhe. Senyamwile.

Aidha, ameongeza kuwa mpango huo unalenga kupunguza gharama za uzalishaji na usafirishaji ili kuongeza thamani ya mazao, kuongeza kipato cha wakulima, wafugaji na wavuvi, pamoja na kuvutia uwekezaji wa sekta binafsi kwa kuzingatia mabadiliko ya tabianchi na kuyaunganisha maeneo yenye uzalishaji mkubwa na miundombinu muhimu kama barabara, reli, bandari, masoko na viwanda vya kuchakata mazao.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Ofisi ya Mageuzi ya Kilimo (ATO), Bi. Elizabeth Missokia, amesema kuwa dhana ya shoroba za kilimo ni moja ya miradi ndani ya mpango kabambe wa mageuzi ya sekta ya kilimo, mifugo na uvuvi, unaounganisha uzalishaji, usindikaji, uchakataji, usafirishaji na uhifadhi pamoja na masoko ili kuharakisha mageuzi ya sekta hizo.

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamwile akichangia jambo wakati majadiliano mara baada ya uwasilishwaji wa Mpango wa Mageuzi wa Shoroba za Kilimo kwenye mkutano wa uhamasishaji wa ukuzaji na uendelezaji wa shoroba za Kilimo, Mifugo na Uvuvi uliofanyika February 12, 1026 mkoani Singida.

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Mhe. Rosemary Senyamule, (katikati) akiwa mgeni rasmi ameongoza mkutano wa uhamasishaji wa ukuzaji na uendelezaji wa shoroba za kilimo, Mifugo na Uvuvi uliofanyika tarehe 12 Februari 2026 mkoani Singida, uliowakutanisha pia Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Mhe. Paulo Chacha, (kulia) na Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, (kushoto) Mhe. Mboni Mhita, kwa lengo la kuimarisha ushirikiano wa kikanda katika kukuza sekta ya kilimo na kuchochea maendeleo ya uchumi.

Mkurugenzi wa Ofisi ya Mageuzi ya kilimo (ATO) Bi. Elizabeth missokia Akiwasilisha hotuba ya Mpango wa Uhamasishaji wa Uzalishaji na Uendelezaji wa shoroba za Kilimo, Mifugo na Uvuvi wakati wa Mkutano wa uhamasishaji wa shoroba za kilimo uliofanyika February 12, 2026, mkoani Singida.

Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Uzalishaji na Maendeleo ya Masoko wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi Ndg. Edson Kilyenyi ameshiriki katika Mkutano wa uhamasishaji na ukuzaji wa uendelezaji wa shoroba za kilimo, Mifugo na Uvuvi kwa lengo la kuleta mageuzi ya sekta hizo ili kukuza uchumi kwa taifa, Mkutano huo umefanyika Februari 12, 2026 mkoani Singida.

Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Idara ya Sera na Mipango wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi Bi. Grace Pahali ameshiriki katika Mkutano wa uhamasishaji na ukuzaji wa uendelezaji wa shoroba za kilimo, Mifugo na Uvuvi kwa lengo la kuleta mageuzi ya sekta hizo ili kukuza uchumi kwa taifa, Mkutano huo umefanyika Februari 12, 2026 mkoani Singida.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

LESENI, VIBALI VYA MAZAO YA MIFUGO NA VYAKULA VYA SAMAKI KUTOLEWA KWA NJIA YA KIELEKTRONIKI

DKT. MHEDE AONGOZA ZOEZI LA UCHANJAJI WA MIFUGO MKOANI IRINGA, WAFUGAJI WAPONGEZA HATUA YA SERIKALI

SERIKALI KURASIMISHA BIASHARA YA MABONDO