KATIBU MKUU WIZARA YA MIFUGO NA UVUVI ARIDHISHWA NA UKAMILIKAJI WA GATI LA TAFICO

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Bi. Agnes Meena, leo Februari 15, amepokea mradi wa  ukarabati wa gati la kuegeshea meli (floating jetty) wa Shirika la Uvuvi Tanzania (TAFICO), uliopo Makao Makuu ya Shirika Ras Mkwavi, Kigamboni jijini Dar es Salaam.

Akipokea mradi huo, Katibu Mkuu ameridhishwa na kukamilika kwa ukarabati wa gati hilo ambalo limekamilika kwa zaidi ya 98%, huku kazi zilizobaki zinatarajiwa kukamilika tarehe 18 Februari 2026.

Ukarabati wa gati hili ni maandalizi ya upokeaji wa meli ya Uvuvi wa bahari kuu ambayo itaendeshwa kwa ubia kati ya sekta binafsi na Serikali . 

Akipokea taarifa ya maandalizi ya mapokezi ya meli ambayo ilihusisha ukarabati wa gati na upatikanaji wa mbia , Bi. Meena amepongeza  kwa hatua iliyofikiwa ya kumpata mbia wa uendeshaji wa meli.

Aidha, amewahimiza watumishi wa Shirika hilo kufanya kazi kwa bidii, weledi na ubunifu ili kuliinua shirika na kulifanya kuwa nguzo muhimu ya maendeleo ya sekta ya uvuvi nchini.

TAFICO inatarajia kupokea meli ya Uvuvi wa Bahari Kuu, meli hiyo na miradi inayotekelezwa inalenga kuongeza thamani ya mazao ya uvuvi, kuimarisha ajira pamoja na kuchochea ukuaji wa uchumi wa buluu nchini.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi Bi. Agnes Meena (katikati) akitoa maelekezo wakati akipokea mradi wa  ukarabati wa gati la kuegeshea meli (floating jetty) wa TAFICO, uliopo Makao Makuu ya Shirika Ras Mkwavi, Kigamboni jijini Dar es Salaam leo Februari 15, 2026. Kushoto kwake waliopo mstari wa mbele ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Uvuvi) Prof. Mohammed Sheikh, na kulia kwake waliopo mstari wa mbele ni Afisa Mtendaji Mkuu wa TAFICO CPA Shaibu Matessa.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi Bi. Agnes Meena (wa pili kushoto) akiongozana na menejimenti ya Shirika la Uvuvi Tanzania (TAFICO), wakati akipokea mradi wa  ukarabati wa gati la kuegeshea meli (floating jetty) wa TAFICO, uliopo Makao Makuu ya Shirika Ras Mkwavi, Kigamboni jijini Dar es Salaam. Ziara hiyo imefanyika leo Februari 15, 2026. Kushoto kwake ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Uvuvi) Prof. Mohammed Sheikh, na kulia kwake ni Afisa Mtendaji Mkuu wa TAFICO CPA Shaibu Matessa.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi Bi. Agnes Meena akisaini kwenye kitabu cha wageni alipotembelea Makao Makuu ya Shirika la Uvuvi Tanzania (TAFICO), yaliyopo Ras Mkwavi–Kigamboni, jijini Dar es Salaam leo Februari 15, 2026, ambapo amepokea mradi wa  ukarabati wa gati la kuegeshea meli (floating jetty) wa TAFICO.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi Bi. Agnes Meena akizungumza na menejimenti ya Shirika la Uvuvi Tanzania (TAFICO), alipokuwa katika ziara ambapo amepokea mradi wa  ukarabati wa gati la kuegeshea meli (floating jetty) wa TAFICO, uliopo Makao Makuu ya Shirika Ras Mkwavi, Kigamboni jijini Dar es Salaam leo Februari 15, 2026.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

LESENI, VIBALI VYA MAZAO YA MIFUGO NA VYAKULA VYA SAMAKI KUTOLEWA KWA NJIA YA KIELEKTRONIKI

DKT. MHEDE AONGOZA ZOEZI LA UCHANJAJI WA MIFUGO MKOANI IRINGA, WAFUGAJI WAPONGEZA HATUA YA SERIKALI

SERIKALI KURASIMISHA BIASHARA YA MABONDO