BI. MEENA AWATAKA WATUMISHI KUWA NA USHIRIKIANO MADHUBUTI

Na. Stanley Brayton, WMUV

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Bi. Agness Meena amewataka watumishi wa Wizara hiyo kuwa na ushirikiano madhubuti na kufanya kazi kwa pamoja ili kuimarisha utendaji kazi na kufikia malengo ya Sekta kwa ufanisi zaidi.

Bi. Meena ametoa wito huo leo Februari 11, 2026 kwenye ofisi ya Makao Makuu ya Wizara iliyopo Mji wa Kiserikali Mtumba Dodoma, wakati wa hafla ya kuwakaribisha Manaibu Makatibu Wakuu wapya wa wizara hiyo.

“Nitumie nafasi hii kuwasihi watumishi wote kuendelea kutoa ushirikiano kwa viongozi ili kufanikisha malengo tuliojiwekea,” amesema Bi. Meena.

Katika hafla hiyo, Bi. Meena amemshukuru aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa wizara hiyo kwa mchango wake katika kuendeleza sekta na kuwapongeza viongozi wapya kwa kuaminiwa kushika nyadhifa hizo muhimu katika wizara.

Aidha aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Uvuvi), Dkt. Edwini Mhede amesema katika kipindi chake alichokuwa hapa Wizarani amejifunza mambo mengi kuhusu sekta za mifugo na uvuvi, akitoa shukrani dhati kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan na viongozi wa Wizara kwa ushirikiano waliompa. 

Pia amesisitiza kuwa walifanya kazi kindugu, n kwa kushirikiana, kusaidiana, na kuahidi kuwa ana imani kubwa na viongozi wapya katika kuendeleza majukumu ya Wizara.

Kwa upande wake Naibu Katibu Mkuu (Mifugo), Dkt. Fabian Madele amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa imani aliyoonesha kwake, na kuahidi kusimamia sekta ya mifugo kwa weledi, kuzingatia misingi ya kisayansi na kufanya kazi kwa ushirikiano na watumishi wote.

Naye Naibu Katibu Mkuu (Uvuvi), Prof. Mohammed Sheikh amesema dhamana aliyopewa ni deni linalopaswa kulipwa kwa utendaji kazi bora katika kutekeleza Dira ya Taifa 2050 na kukuza uchumi wa buluu.

Aidha, Prof. Sheikh amesisitiza kuwa utumishi wa umma ni kama mbio za kupokezana vijiti hivyo ni zamu yao sasa kufanya kazi kwa bidii, umoja na upendo huku wakiondoa majungu na chuki mahali pa kazi ili kujenga mazingira bora ya utendaji.

Akizungumza kwa niaba ya watumishi, Mkurugenzi wa Idara ya Uzalishaji na Maendeleo ya Masoko Nchini, Ndg. Stephen Michael amesema kuwa watumishi wa wizara wataendelea kutoa ushirikiano wa dhati na kufanya kazi kwa kitimu ili kuhakikisha wizara inatekeleza majukumu yake kwa ufanisi.

Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Bi. Agnes Meena (wa kwanza kulia), akizungumza na Watumishi wa Wizara hiyo, mara baada ya kuwasili Manaibu Wakuu wa Wizara hiyo katika Ofisi za Wizara hiyo iliyopo Mji wa Kiserikali - Mtumba, Februari 11, 2025 Dodoma

Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Bi. Agnes Meena (wa pili kushoto), akisalimiana na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Mifugo), Dkt. Fabian Magawa Madele (wa kwanza kushoto), mara baada ya kuwasili katika Ofisi za Wizara hiyo iliyopo Mji wa Kiserikali - Mtumba kama Naibu Katibu Mkuu, Februari 11, 2026 Dodoma.

Aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Dkt. Edwin Mhede (wa tatu kushoto), akimlaki Naibu Katibu Mkuu (Uvuvi), Prof. Mohammed Ali Sheikh (wa pili kushoto), mara baada ya kuwasili katika Ofisi za Wizara hiyo iliyopo Mji wa Kiserikali - Mtumba kama Naibu Katibu Mkuu, Februari 11, 2026 Dodoma.

Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Balozi Dkt. Bashiru Ally Kakurwa (wa kwanza kushoto), akizungumza na Watendaji Wakuu wa Wizara hiyo, mara baada ya kuwasili Manaibu Katibu Wakuu wa Wizara hiyo katika Ofisi za Wizara hiyo iliyopo Mji wa Kiserikali - Mtumba, Februari 11, 2025 Dodoma

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Mifugo), Dkt. Fabian Magawa Madele (katikati), akizungumza na Watumishi wa Wizara hiyo, mara baada ya kuwasili katika Ofisi za Wizara iliyopo Mji wa Kiserikali - Mtumba kama Naibu Katibu Mkuu, Februari 11, 2026 Dodoma.

Picha ni watumishi wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi, wakimsikiliza Katibu Mkuu wa Wizara hiyo (hayupo pichani), wakati wa mapokezi ya Manaibu Katibu Wakuu wa Wizara,  yaliyofanyika katika Ofisi za Wizara iliyopo Mji wa Kiserikali - Mtumba, Februari 11, 2026 Dodoma.

Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Bi. Agnes Meena (katikati mstari wa mbele), akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya Wakurugenzi, Wakuu wa Taasisi na Idara ya Wizara hiyo, mara baada ya mapokezi ya Manaibu Katibu Wakuu wa Wizara hiyo,  yaliyofanyika katika Ofisi za Wizara iliyopo Mji wa Kiserikali - Mtumba, Februari 11, 2026 Dodoma, wa kwanza kushoto ni aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu (Uvuvi), Dkt. Edwin Mhede, wa pili kushoto ni Naibu Katibu Mkuu (Uvuvi), Prof. Mohammed Ali Sheikh, wa pili kulia ni Naibu Katibu Mkuu na Uvuvi (Mifugo), Dkt. Fabian Magawa Madele , wa kwanza kulia ni mwakilishi wa Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu wa Wizara hiyo, Bi. Wamoja Ayubu.

Aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Uvuvi), Dkt. Edwin Mhede (kushoto), akimkabidhi Nyaraka za Utendaji Kazi Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo (Uvuvi), Prof. Mohammed Ali Sheikh (kulia), mara baada ya kuwasili katika Ofisi za Wizara hiyo iliyopo Mji wa Kiserikali - Mtumba, Februari 11, 2025 Dodoma

Aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Uvuvi), Dkt. Edwin Mhede (kushoto), akimkabidhi Nyaraka za Utendaji Kazi Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo (Mifugo), Dkt. Fabian Magawa Madele (kulia), mara baada ya kuwasili kwa mara ya kwanza katika Ofisi za Wizara hiyo iliyopo Mji wa Kiserikali - Mtumba, Februari 11, 2026 Dodoma.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

LESENI, VIBALI VYA MAZAO YA MIFUGO NA VYAKULA VYA SAMAKI KUTOLEWA KWA NJIA YA KIELEKTRONIKI

DKT. MHEDE AONGOZA ZOEZI LA UCHANJAJI WA MIFUGO MKOANI IRINGA, WAFUGAJI WAPONGEZA HATUA YA SERIKALI

SERIKALI KURASIMISHA BIASHARA YA MABONDO