Nav bar

Ijumaa, 28 Machi 2025

KAMATI YA BUNGE YARIDHISHWA NA UTEKELEZAJI WA BAJETI YA WIZARA YA MIFUGO NA UVUVI 2024/2025

Na Hamis Hussein, MLF Dodoma.

⬛️ Yaahidi Kuisemea Wizaya hiyo kuongezewa Fedha

Kamati ya Kudumu ya Viwanda,Biashara, Kilimo na Mifugo, chini ya Kaimu Mwenyekiti wake Mhe. Dkt. Medadi Kalemani Machi 27, 2025 imepokea na kujadili taarifa ya utekelezaji wa Bajeti ya Wizara ya  Mifugo na Uvuvi katika mwaka wa fedha 2024- 2025 na kuridhia mpango na bajeti ya mwaka fedha 2025- 2026.

Akizungumza kwenye kikao hicho Kaimu Mwenyekiti wa Kamati Mhe. Dkt. Medadi Kalemani ameipongeza Wizara ya Mifugo na Uvuvi ambayo licha ya kuwa na bajeti ndogo lakini imeweza kutekeleza miradi ya kimkakati.

" Wizara hii  huwa haipati bajeti kubwa sana ukilinganisha na Wizara zingine lakini imeweza kutekeleza miradi ya kimkakati ambayo inaenda kuleta tija kwa wananchi, hivyo Mhe. Waziri na watumishi wote wa Wizara sisi kamati tutaendelea kuishauri serikali ili iongeze bajeti kwenye sekta hii ya mifugo na uvuvi kwani inatoa utajiri kwa wananchi, lakini pia mtuombee na sisi turudi ili tuendelee kuwasemea  watanzania" alisema Mhe.Dkt. Kalemani.

Aidha kamati hiyo iliiagiza Wizara kuweka mazingira yatakayowafanya wananchi wanaojihusisha na mnyonyoro wa thamani katika sekta za mifugo na Uvuvi waweze kunufaika na kuthaminiwa ili kuonesha umuhimu wa sekta za Mifugo na Uvuvi.

Kwa upande wake Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji alisema kuwa Wizara hiyo imeendelea kufanya vizuri na kuanza kuonekana ya thamani kwa jamii kutokana na usimamizi na ushauri mzuri unaotolewa na kamati ya kudumu ya Viwanda, Biashara, Kilimo na Mifugo hivyo Wizara itaendelea kutekeleza miradi yakuinua kipato cha mwananchi mmoja mmoja na Taifa kwa ujumla.

" Mhe. Mwenyekiti Wizara yetu inafanya vizuri kwa sasa na inaoneka kukua hii nikutokana na Ushauri na maelekezo ya kamati yako, hivyo tutaendelea kufanya kazi kwa weledi kuzikuza sekta hizi, hilo ndilo lengo letu." Alisema Mhe. Dkt. Kiaji.

Naye Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi Prof. Riziki Shemdoe amesema Wizara hiyo itaendelea kutekeleza miradi kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo wa kitaifa na kimataifa na kuwa kama watendaji wa Wizara hiyo wataendelea kukamilisha miradi inayoendelea kutekelezwa ili ianze kutoa matunda kwa watanzania.

Katika mwaka 2024/2025, Wizara ya Mifugo na Uvuvi iliidhinishiwa jumla ya Shilingi Bilioni 460.3 kwa ajili ya kutekeleza majukumu yake, ambapo hadi kufikia Februari 28, 2025, jumla ya Shilingi  Bilioni 40.3 zimepokelewa  kwa ajili ya matumizi ya kawaida, sawa na asilimia 41.48 ya bajeti iliyotengwa,  Shilingi Bilioni 25.5 sawa na asilimia 56.88 ni kwa ajili ya Mishahara (PE) na Shilingi Bilioni 14.8 sawa na asilimia 28.29 ni kwa ajili ya Matumizi Mengineyo (OC).

Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji akizungumza na Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Viwanda, Biashara, Kilimo na Mifugo na Wataalam wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi wakati wa kuwasilisha taarifa ya Utekelezaji wa Bajeti ya Wizara hiyo kwa Mwaka wa fedha 2024/2025 kwenye  Kikao  kilichofanyika Machi 27, 2025 Bungeni Jijini Dodoma
Kaimu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Viwanda, Biashara, Kilimo na Mifugo Mhe. Dkt. Medadi Kalemani akizungumza na Wajumbe wa kamati hiyo na Wataalam wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi wakati wa kupokea taarifa ya Utekelezaji wa Bajeti ya Wizara hiyo kwa Mwaka wa fedha 2024/2025, Kikao hicho kilichofanyika Leo Machi 27, 2025 Bungeni Jijini Dodoma

Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Alexander Mnyeti akizungumza na Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Viwanda, Biashara, Kilimo na Mifugo na Wataalam wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi wakati wa kuwasilisha taarifa ya Utekelezaji wa Bajeti ya Wizara hiyo kwa Mwaka wa fedha 2024/2025 kwenye  Kikao  kilichofanyika Machi 27, 2025 Bungeni Jijini Dodoma
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi Prof. Riziki Shemdoe akifafanua Jambo mbele ya Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Viwanda, Biashara, Kilimo na Mifugo wakati wa kuwasilisha taarifa ya Utekelezaji wa Bajeti ya Wizara hiyo kwa Mwaka wa fedha 2024/2025 kwenye  Kikao  kilichofanyika Machi 27, 2025 Bungeni Jijini Dodoma

Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Viwanda, Bishara, Kilimo na Mifugo Wakismikiliza Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji(aliyesimama) wakati akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa bajeti ya Mwaka wa fedha 2024/2025 na mpango wa bajeti ya mwaka wa fedha 2025/2026 kwenye kikao cha Kamati ya Bunge kilichofanyika Machi 27, 2025 Bungeni, Jijini Dodoma.








Hakuna maoni:

Chapisha Maoni