Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi Prof. Riziki Shemdoe leo tarehe 11 Novemba, 2024 akiwa nchini China katika Jiji la Nanjing, Jimbo la JiangSu ametembele Taasisi ya Jiografia na Limnolojia ya Nanjing (Nanjing Institute of Geography and Limnology, Chinese Academy of Sciences, NIGLAS) ambayo inajihusisha na utafiti kwenye sayansi akua.
Akiwa NIGLAS, Prof. Shemdoe amefanya mazungumzo na Menejimenti ya Chuo hicho na kukubaliana kushirikiana na Tanzania katika kazi za Utafiti wa Mambo ya Uvuvi na ufugaji samaki kiikolojia kupitia TAFIRI. Pia, Shemdoe amezipongeza NIGLAS na TAFIRI kwa kuendeleza mashirikiano ambayo yanaendeleza mahusiano kati ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Jamhuri ya Watu wa China ambayo yaliasisiwa na Mwl. Nyerere na Rais Mao Zedong.
Vilevile, Katibu Mkuu alikutana na kupokea taarifa ya mafunzo ya maabara yaliyotolewa kwa kipindi cha mwezi mmoja kwa watumishi wa kada ya Mafundi Sanifu Maabara kutoka TAFIRI.