Na. Stanley Brayton
Mheshimiwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Philip Isdor Mpango, amezipongeza Sekta za Mifugo na Uvuvi kwa utekelezaji mzuri wa shughuli zake ambazo zimelenga kukuza shughuli za ufugaji na uvuvi kwa kuendana na Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika kuhudumia wananchi na kuwapa maisha Bora.
Akizungumza, Mheshimiwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Philip Isdor Mpango leo Oktoba 8, 2024 katika Ziara yake wilayani Igunga, Mkoani Tabora, Dkt. Mpango amesema Wizara ya Mifugo na Uvuvi inafanya vizuri katika kuhakikisha mifugo bora inapatikana kwa wananchi kwa kutoa pembejeo bora kwa wafugaji na wavuvi, vilevile kutoa mikopo kwa wafugaji na wavuvi pamoja na kuwapatia mbegu bora za vifaranga vya samaki pamoja na madume Bora ya ng'ombe.
Kwa Upande wake, Naibu Waziri wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Mhe. Alexander Mnyeti amesema Serikali kupitia Wizara ya Mifugo imefanya mambo mengi sana kwa watanzania na ata katika Wilaya ya Igunga ikiwa ni kutoa elimu kwa wafugaji na wavuvi.
“tuna fursa ya ufugaji wa samaki kwa njia ya vizimba, na ya utengenezaji wa mabwawa ya kufugia samaki pamoja na kutoa madume Bora ya ng'ombe kama mbegu”, amesema Mhe. Mnyeti
Aidha, Mhe. Mnyeti amesema, Madume Bora ya ng'ombe yalishagawiwa katika baadhi ya wilaya, ikiwemo Wilaya ya Bahi, Serengeti na Bunda.
Vilevile, Mhe. Mnyeti amesema mpango huo ni endelevu hapa nchini, na Wizara inampango wa kusambaza madume hayo Bora ya ng'ombe katika wilaya zote nchini Tanzania ila yaweze kupanda ng'ombe wa kienyeji na kupata ng'ombe wengine walio Bora.
Mheshimiwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Philip Isdor Mpango (aliyeshika bomba la maji), akifungua maji kama Ishara ya Uzinduzi na Upanuzi wa Mradi wa Maji kutoka ziwa Viktoria kwenda Bukene, ni katika Ziara yake ya kikazi Mkoani Tabora, Oktoba 8, 2024, Nzega - Tabora, Wa tatu kulia ni Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Alexander Mnyeti
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni