Na. Martha Mbena
Wizara ya Mifugo na Uvuvi imetaoa elimu kwa wananchi juu ya kichaa cha Mbwa Wilayani Misungwi Mkoani Mwanza ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya siku ya kichaa cha mbwa duniani ambayo yanatarajiwa kufanyika Septemba 28.2024.
Akiongea na wakazi wa kitongoji cha Ng'walo gwa magole kata ya Bulemeji Wilayani hapo Leo (27.09.2024) Mkurugenzi Msaidizi wa afya ya jamii ya Veterinari kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi Dkt. Stanford Ndibalema amewataka wananchi kuzingatia chanjo ya kichaa cha Mbwa ili kuepusha madhara yanayoweza kutokea.
"Huu ugonjwa unaweza kuzuilika iwapo tutaamua kuwachanja Mbwa wetu, hivyo kila mmoja wetu anaemiliki Mbwa anapaswa kumlinda Mbwa huyo dhidi ya ugonjwa huu", Amesema Dkt. Ndibalema.
Aidha, Dkt. Ndibalema amesisitiza umuhimu wa kuwaona wataalam wa Mifugo kwa ajili ya chanjo badala ya kusubiri chanjo ya bure inayotolewa na Serikali
Baadhi ya wazazi na wanafunzi waliofikiwa Na elimu ya kichaa cha Mmbwa wanasema elimu imewasaidia kutambua dalili za Mbwa mwenye kichaa na matibabu ya mtu aliyeng'atwa na Mbwa.
Elimu hiyo imetolewa katika maeneo mbali mbali ya Wilaya ya Misungwi zikiwemo Shule za msingi na sekondari pamoja na wataalam kutoka sekta ya Mifugo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni