Wizara ya Mifugo na Uvuvi kupitia Taasisi ya Utafiti a Mifugo (TALIRI) inaendelea kutoa elimu ya uboreshaji wa mbari za mbuzi wa kienyeji kwa Wafugaji kupitia maonesho ya Kimataifa ya Nanenane yanayoendelea kufanyika Kanda ya ziwa Magharibi katika Viwanja vya Nyamhongolo jijini Mwanza.
Akitoa elimu hiyo kwa wadau waliotembelea kwenye banda la Wizara hiyo Agosti 06,2024. Afisa Mifugo wa Taasisi hiyo Bw. Amos Kisusi amesema madume ya mbuzi 15 ya Boer kutoka Afrika kusini yametumika kuboresha mbari za mbuzi 450 wa kienyeji waliotolewa na serikali.
Bw. Kisusi amesema uboreshaji wa Mbari za Mbuzi aina ya boer ni moja ya miradi ya wizara ya Mifugo na Uvuvi ambao unayooneshwa kupitia viwanja vya maonesho ya kilimo, mifugo na uvuvi Nane Nane jijini Mwanza, ambapo ulianza mwaka 2021 kwa ujenzi wa mabanda bora ya kuhifadhi Mbuzi aina ya Boer.
Aidha, Mbuzi 15 aina ya Boer walipokelewa 2022 kutoka nchini Afrika kusini kwa gharama ya shilingi milioni 42 na wakaanza kupanda majike wa kienyeji na hadi kufikia kuanza kuzaa mwezi Februari, 2024 kupata mbuzi chotara.
Pia, Mbuzi chotara mpaka sasa wanaendelea kukuzwa chini ya uangalizi wa TALIRI huku taratibu za upatikanaji wa vibali vya usambazaji wa mbuzi hao kwa wafugaji nchini kutoka wizarani zikiendelea.
Timu ya wataalamu kutoka Taasisi ya Utafiti wa Mifugo Tanzania Kanda ya ziwa wanaendelea kutoa elimu mbalimbali ya uzalishaji, Utafiti na ufugaji bora wa Mifugo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni