Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Prof. Riziki Shemdoe, amehimiza matumizi ya teknolojia ya Mifugo na Uvuvi kwa wafugaji ili kuweza kuleta tija katika uzalishaji.
Akizungumza, leo Agosti 2, 2024 mkoani Dodoma alipotembelea kwenye Maonesho ya Nanenane ya Kimataifa yanayofanyika Kitaifa mkoani Dodoma, Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Prof. Shemdoe amesema kuwa katika haya maonyesho kuna teknolojia nzuri sana ya ufugaji na uvuvi kwa hiyo wafugaji na wavuvi wote waje kuchukua teknolojia hii ili kuboresha mifugo yao.
"mnakumbuka Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa jana alisema maana halisi ya haya maonesho ni kwamba wakulima waje kuchukua teknolojia" amesema Prof. Shemdoe
Aidha, Prof. Shemdoe alisema haya maonesho ya nanenane ni kwa mara ya kwanza yanaadhimishwa kimataifa hapa mkoani Dodoma na ameweza kutembelea mabanda mbalimbali ya mifugo na uvuvi pamoja na kilimo ikiwa na sehemu ya vipando.
Vilevile Prof. Shemdoe ametoa wito kwa watanzani kutumia siku nane kutembelea maonesho haya ya nanenane ili kujionea teknolojia mbalimbali zinazopatikana katika maonesho haya ambazo zitawasaidia katika shughuli za uzalishaji.
Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Mhe. Jabir Shekimweri, amemshukuru Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwa kutembelea maonesho hayo ya nanenane.
Vilevile Mhe. Jabir amesema, maonesho haya yatawasaidia wananchi wa Tanzania kubadirisha maisha yao kwa kuongeza kipato na kukuza uchimi wa nchi, kwani elimu wanayoipata kwenye maonesho haya yatakuwa na maboresho na mapinduzi makubwa kwao.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni