Mkuu wa Wilaya ya Sengerema
Mhe. Senyi Ngaga akifungua kikao cha kujadili changamoto mbalimbali
zinazowakabili wanufaika wa boti na vizimba na hivyo kuzipati utatuzi, Aidha
amewasihi wanufaika kutumia vifaa hivyo kama ilivyokusudiwa na kurejesha mikopo
yao kwa uaminifu, Februari 24,2024
Mkoani Mwanza.
Mkurugenzi wa Ukuzaji
Viumbe maji Dkt. Nazaeli Madalla akifafanua baadhi ya hoja zilizoibuliwa na wanufaika wa mkopo wa vizimba usio na
riba wakati wa kikao kifupi cha kusikiliza
changamoto mbalimbali za wanufaika hao kilichofanyika Buchosa Mkoani Mwanza, Februari 24,2024
Kaimu Mkurugenzi Msaidizi Ukuzaji Viumbe Maji Baridi, Dkt.
Imani Kapinga akujibu baadhi ya maswali yaliyokuwa yakiulizwa na baadhi ya wanufaika wa mkopo wa vizimba usio na riba (hawapo pichani) wakati wa kikao kifupi cha kusikiliza na
kujibu changamoto zinazowakabili
wanufaika hao kilichofanyika Buchosa
Mkoani Mwanza, Februari 24,2023
Mkurugenzi msaidizi wa
Idara ya Utafiti, Mafunzo na Ugani, (uvuvi) Bw. Anthony Dadu (aliyesimama)
akijibu maswali mbalimbali yaliyojitokeza wakati wa kikao kifupi cha kujadili
changamoto mbalimbali zinazowakabili wanufaika wa mkopo wa vizimba na maboti, Februari 24,2024 Mkoani
Mwanza
Afisa Maendeleo ya Biashara
kutoka Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) Bi. Glacia Marugujo
(katikati) akitoa maelezo kwa wanufaika wa mkopo nafuu usio na riba wa boti na vizima juu ya namna na siku
watakayoanza kurejesha mikopo hiyo
Februari 24,2024 Mkoani Mwanza.
Katibu wa kikundi cha
Sangara - Nyakaliro Ficos Bw. Revocatus Rugaba akieleza changamoto mbalimbali
na kutoa maoni kwa Mkuu wa Wilaya ya Sengerema Mhe. Senyi Ngaga na watendaji
kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Uvuvi) (hawapo pichani) wakati wa kikao
kifupi cha kujadili changamoto hizo na kuzipatia utatuzi, kikao hicho kimefanyika
Buchosa Mkoani Mwanza Februari 24, 2024
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni