Katibu Mkuu Wizara ya
Mifugo na Uvuvi Prof. Riziki Shemdoe
(kushoto) akiongea na sehemu ya wakandarasi walioshinda zabuni za miradi
mbalimbali ya ujenzi ikiwemo ya minada na
majengo kwenye kampasi za LITA (hawapo pichani) ambapo amewasisitiza wakandarasi hao kutekeleza
miradi kwa wakati, kuwasiliana kwa
haraka pindi inapobidi na ushirikishwaji wa karibu wa viongozi wa kisiasa
kwenye maeneo ya miradi, kikao hicho kimefanyika kwenye ukumbi wa NBC Jijini
Dodoma (24.1.2024) kulia ni Naibu katibu
Mkuu (Mifugo) Prof. Daniel Mushi.
Katibu Mkuu Wizara ya
Mifugo na Uvuvi Prof. Riziki Shemdoe (katikati) akisaini mkataba wa makubaliano
ya ujenzi wa soko la upili lililopo kishapu mkoani Shinyanga, Handeni mkoani Tanga na Nzega mkoani Tabora
na mwakilishi wa kampuni ya MACEA Construction Ltd, Bw. Godlove Gandye
(kushoto) kulia ni Naibu Katibu Mkuu (Mifugo) Prof. Daniel Mushi (24.01.2024)
Katibu Mkuu Wizara ya
Mifugo na Uvuvi Prof. Riziki Shemdoe akikabidhi mkataba wa makubaliano ya
ujenzi wa soko la upili la Luaguza lililopo Lushoto mkoani Tanga kwa Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Maruu RPK
Group Ltd , Bw. Rhodes Kimambo wakati wa kikao kifupi cha makabidhiano
kilichofanyika kwenye ukumbi wa NBC Jijini Dodoma (24.1.2024)
Mtendaji Mkuu wa Wakala ya
Mafunzo ya Mifugo (LITA), Dkt. Pius Mwambene (kushoto) akikabidhi mkataba wa
makubaliano ya ujenzi wa ukumbi mmoja wa miadhara wenye uwezo wa kuchukua
wanafunzi 100 na ujenzi wa hostel moja yenye uwezo wa kuchukua wanafunzi 150
kwa Arch. Eliah Mpembeni kutoka kampuni ya KADIVA, Mkataba huo umesainiwa
kwenye ukumbi wa NBC Jijini Dodoma (24.01.2024)
Sehemu ya washiriki wa kikao cha makabidhiano ya mkataba wa makubaliano wa ujenzi miradi ya maendeleo kilichofanyika kwenye ukumbi wa NBC Jijini Dodoma (24.1.2024)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni