Waziri wa Mifugo na Uvuvi,
Mhe. Abdallah Ulega amewaagiza Naibu Katibu Mkuu, Sekta ya Mifugo, Prof. Daniel
Mushi na Katibu Tawala wa Mkoa wa Kagera kuhakikisha kuwa maeneo yote yaliyopo
katika Kampuni ya Ranchi za Taifa (NARCO) mkoani Kagera ambayo hayana mgogoro
yatangazwe kwa ajili ya uwekezaji.
Ulega ametoa maelekezo hayo
wakati wa kikao chake na Viongozi mbalimbali wa
Mkoa wa Kagera kilichofanyika leo Januari 22, 2024 chenye lengo la
kumaliza migogoro iliyopo baina ya wananchi na Kampuni ya Ranchi za Taifa
(NARCO).
Amesema maeneo ambayo
yameshapimwa na ambayo hayana mgogoro yatangazwe ili wawekezaji wenye uwezo
waweze kupewa kwa ajili ya kufanya ufugaji wenye tija.
Sambamba na hayo amewataka
Wataalamu kurejea upya kwenye maeneo yote ambayo yameonekana yana migogoro ili
kutatua changamoto zilizopo na kuwezesha maeneo hayo yaweze kuendelezwa na
wawekezaji wenye uwezo.
Waziri wa Mifugo na Uvuvi,
Mhe. Abdallah Ulega(kulia) akiteta jambo na Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Mhe.
Erasto Sima wakati wa kikao chake na Viongozi mbalimbali wa Mkoa wa Kagera kilichofanyika leo Januari 22,
2024 chenye lengo la kumaliza migogoro iliyopo baina ya wananchi na Kampuni ya
Ranchi za Taifa (NARCO).
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni