Katibu Tawala wa Mkoa wa
Mwanza Bw. Balandya Elikana ameipongeza Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwa kuweka
mkakati wenye tija kwa vijana kwa kuwajengea kuweza kujiajiri kwa kutoa mikopo
isiyo na riba ya pembejeo za vizimba, chakula cha samaki na vifaranga vya
samaki kwa kushirikiana na Benki ya Maendeleo ya Kilimo TADB.
Balandya ameyasema hayo
ofisini kwake mara baada ya kupokea ugeni
kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi ukiongozwa na Afisa Uvuvi Mkuu Bi.
Mkomanile Mahundi na kusema ufugaji kwenye vizimba utasaidia sana katika
uzalishaji wa samaki.
Katika mazungumzo pia
alitoa ushauri mpango huo wa ufugaji kwa njia ya vizimba ufanyike kwa awamu
kutokana na wingi wa vikundi husika kutoka mikoa ya kanda ya ziwa.
"Serikali inayoongozwa
na Mhe. Rais Samia imedhamiria kuwainua kundi la vijana kimaendeleo, mpango huu
wa ufugaji wa kisasa wa samaki wataalamu kutoka wizarani ukiwawekea mazingira
mazuri ya kazi utazidi kuwa na tija kwao kiuchumi", amefafanua Mtendaji
huyo wa Mkoa wakati wa mazungumzo hayo.
Ameiomba Wizara ya Mifugo
na Uvuvi kuweka ushirikiano na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa ili kuhakikisha miradi
hiyo inafanyiwa ufuatiliaji na kuwa endelevu na mwishowe inafikisha ndoto ya
Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan kuona inawakomboa kiuchumi Wananchi hususani
Vijana na wakinamama.
Kwa upande wake Afisa Uvuvi
Mkuu Bi. Mkomanile Mahundi amesema lengo la kuja Mwanza ni kuainisha wanufaika
wa mikopo ya pembejeo za ufugaji Samaki kwa Vizimba na kuwawezesha kukidhi
vigezo vya mkopo wenye masharti nafu na
kushauri pale zitakapo bainika changamoto ili zoezi hilo liwe limekamilika
kabla ya Januari 29 2024.
"Tutapita maeneo yote
Mikoa ya Kanda ya Ziwa ambayo mradi huu wa ufugaji wa samaki kisasa kwa njia ya
vizimba unafanyika ili tujiridhishe kwa kila hatua kabla ya kuwakabidhi
wahusika wote waliokidhi vigezo vya mradi huu",amesisitiza Bi.Mahundi
Mkoa wa Mwanza una jumla ya
vikundi 79 wakiwemo watu binafsi 11, kampuni 6, vijana 13 na vikundi 49.
Afisa Uvuvi Mkuu kutoka
Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Bw. Fredrick
Mussa akitoa elimu na kuelezea faida ya kuomba mikopo ya pembejeo za vizimba
kwa wanufaika (hawapo pichani) wa mkopo wa vizimba na pembejeo zake kwa vyama
vya Ushirika, Vikundi na watu binafsi kwenye
Halmashauri ya Wilaya ya Nyamagana Mkoani Mwanza, Januari 11.2024.
Katibu Tawala Mkoa wa
Mwanza, Bw. Balandya Elikana (katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na maafisa
Uvuvi kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi na Mkoa wa Mwanza mara baada ya kikao
kifupi kilichofanyika ofisini kwake,
lengo likiwa ni pamoja na kueleza nia ya Wizara hiyo kwa
kushirikiana na benki ya maendeleo ya
kilimo (TADB) ya kutoa mkopo wenye masharti
nafuu isiyo na riba kwa vikundi, vyama vya ushirika na watu binafsi
ikijumuisha Pembejeo za vizimba, Chakula cha Samaki Mkoani Mwanza Januari 11.2024.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni