Nav bar

Jumapili, 27 Agosti 2023

UFUGAJI WA SAMAKI CHANZO MBADALA CHA KIPATO KWA WAVUVI - ULEGA

Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega amesema Serikali inaweka msisitizo mkubwa katika ufugaji wa kisasa wa samaki kwa njia ya vizimba ili kuwawezesha wavuvi kuwa na chanzo mbadala cha kipato  na kupunguza utegemezi wa shughuli za uvuvi katika maji ya asili.


Mhe. Ulega ameyasema hayo Agosti 16, 2023 wakati wa kufungua Kongamano la wadau la kujadili Sera, Sheria na kanuni za Uvuvi za kimataifa ili ziweze kutumika katika mabadiliko ya mfumo wa Sekta za Uvuvi Barani Afrika 


Amesema kwamba lengo la Serikali ni kuweka nguvu kubwa katika ufugaji wa samaki ili kuacha maji ya asili yaweze kupumua na kuondoa wasiwasi wa kipato  kwa wavuvi kila siku


"Mtu akiwa na  vizimba vyake  na kufuga samaki vizuri na kuwapeleka sokoni  ana uhakika wa kupata kipato  Alisema Mhe. Ulega


Aidha ameongeza  kuwa katika jitihada hizo za Serikali ni pamoja na kutoa elimu kwa wananchi juu ya kulinda rasilimali za uvuvi huku akiongeza kuwa  ni muhimu wadau wenyewe wakujua ulinzi wa rasilimali ni jambo  lao wenyewe


Halikadhalika Mhe. Ulega amefafanua kuwa Serikali imekuwa ikichukua hatua mbalimbali za kukomesha uvuvi haramu katika maji ya asili iwe baharini au katika maziwa ili kuhakikisha unapungua na kukomeshwa kabisa


Naye Mwakilishi wa Mkurugenzi  wa Taasisi ya AU-IBAR, Dkt. Mohamed Seisay amesema kuwa kongamano hilo la siku tatu kuanzia tarehe 16-18 linahusu kujadili Sera, Sheria na Kanuni za Uvuvi za Kimataifa ili ziweze kutumika katika mabadiliko ya mfumo wa Sekta za Uvuvi Barani Afrika.

Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega (Mb)  akifungua kongamano la wadau la kujadili Sera, Sheria na Kanuni za Uvuvi za Kimataifa ili ziweze kutumika katika mabadiliko ya mfumo wa Sekta za Uvuvi Barani Afrika lililofanyika kwenye Ukumbi wa Peacock hoteli jijini Dar es salaam  Agosti 16,2023.

Sehemu ya wadau wa kongamano la kujadili Sera, Sheria na kanuni za Uvuvi za Kimataifa ili ziweze kutumika katika mabadiliko ya mfumo wa Sekta za Uvuvi Barani Afrika Agosti 16, 2023.

Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe.  Abdallah Ulega (wa pili kulia) akiongea na waandishi wa habari mda mfupi mara baada ya kufungua kongamano la wadau la kujadili Sera,  Sheria na Kanuni za Uvuvi za Kimataifa ili ziweze kutumika katika mabadiliko ya mfumo wa Sekta za Uvuvi Barani Afrika  Agosti 16, 2023.

Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega (katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na wadau wa Uvuvi mara baada ya kufungua Kongamano la kujadili Sera, Sheria na Kanuni za Uvuvi za Kimataifa ili ziweze kutumika katika mabadiliko ya mfumo wa Sekta za Uvuvi Barani Afrika lililofanyika kwenye ukumbi wa peacock hotel jijini Dar es Salaam, Agosti 16,2023.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni