Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya
Mifugo na Uvuvi (Mifugo) Dkt. Charles Mhina ambaye pia ni Mkurugenzi wa Utawala
na Rasilimali Watu (Mifugo), (katikati), akitoa maagizo kwa mkandarasi wa
ujenzi wa mradi wa jengo la makao makuu ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Shirika
la Nyumba la Taifa (NHC) pamoja na mshauri elekezi wa mradi huo Wakala wa
Majengo ya Serikali (TBA), kuhakikisha wanampatia taarifa ya kila wiki juu ya
maendeleo ya mradi huo unaotekelezwa katika Mji wa Serikali Mtumba jijini
Dodoma. Kulia kwa kaimu katibu mkuu ni mbunifu wa majengo kutoka Wizara ya
Mifugo na Uvuvi Bw. Humphrey Killo anayesimamia mradi huo na kushoto kwa kaimu
katibu mkuu ni mbunifu wa majengo kutoka TBA Bw. Weja Ng’olo. (23.02.2022)
Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya
Mifugo na Uvuvi (Mifugo) Dkt. Charles Mhina ambaye pia ni Mkurugenzi wa Utawala
na Rasilimali Watu (Mifugo), (watatu kutoka kulia), akipatiwa maelezo ya ujenzi
wa mradi wa jengo la makao makuu ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi kutoka kwa mmoja
wa wasimamizi wa mradi huo unaotekelezwa na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC)
katika katika Mji wa Serikali Mtumba, jijini Dodoma ambapo kaimu katibu mkuu
huyo ameeleza kutoridhishwa na kasi ya ujenzi huo. (23.02.2022)
Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya
Mifugo na Uvuvi (Mifugo) Dkt. Charles Mhina ambaye pia ni Mkurugenzi wa Utawala
na Rasilimali Watu (Mifugo), (katikati), akiwa ameambatana na baadhi ya
watendaji kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Wakala wa Majengo ya Serikali (TBA)
na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), wakati akikagua ujenzi wa mradi wa jengo
la makao makuu ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi katika Mji wa Serikali Mtumba,
jijini Dodoma baada ya kutoridhishwa na kasi ya ujenzi huo na kuagiza
kuchukuliwa kwa hatua za haraka, ikiwemo ya muda wa kazi kuongezwa ili
kukamilisha mradi huo katika muda wa miezi 24 kama ilivyoainishwa kwenye
mkataba. (23.02.2022)
Muonekanao wa maendeleo ya
ujenzi wa mradi wa jengo la makao makuu ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi katika Mji
wa Serikali Mtumba jijini Dodoma, unaotekelezwa na Shirika la Nyumba la Taifa
(NHC) pamoja na mshauri elekezi wa mradi huo Wakala wa Majengo ya Serikali
(TBA), ambapo Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Mifugo) Dkt. Charles
Mhina ambaye pia ni Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu (Mifugo),
ametembelea na kukagua mradi huo na kukataa ombi la NHC la kuongezewa muda wa
zaidi ya miezi 24 nje ya mkataba ili kutekeleza mradi na kuagiza kuongezwa kwa
muda wa saa za kazi, uwepo wa wafanyakazi zaidi pamoja na vifaa vya kutosha kwa
ajili ya ujenzi. (23.02.2022)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni