Waziri ya Mifugo na Uvuvi, Mhe. Mashimba Ndaki akikata utepe
kuashiria uzinduzi wa Mwongozo wa Upatikanaji, Usimamizi na Uendelezaji wa
Maeneo ya Malisho katika hafla fupi ya kuzindua mwongozo huo iliyofanyika
Mkoani Pwani Disemba 22, 2021. Wakati akizindua Mwongozo huo, Mhe. Ndaki
alisema mwongozo huo ukitekelezwa vizuri utatatua changamoto ya malisho na maji
kwa mifugo na itasaidia kupunguza migogoro ya Wafugaji na watumiaji wengine wa
ardhi.
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Abdallah Ulega (katikati)
akimkabidhi Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Mashimba Ndaki (wa pili kushoto)
nakala ya mwongozo ili awagawie baadhi ya Wakuu wa Mikoa waliohudhuria hafla ya
uzinduzi wa Mwongozo wa Upatikanaji, Usimamizi na Uendelezaji wa Maeneo ya
Malisho iliyofanyika Mkoani Pwani Disemba 22, 2021.
Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Mashimba Ndaki (wa pili kushoto) akimkabidhi Mwenyekiti wa Chama cha Wafugaji Tanzania (CCWT), Bw. Jeremiah Wambura nakala ya Mwongozo wa Upatikanaji, Usimamizi na Uendelezaji wa Maeneo ya Malisho katika hafla fupi ya kuzindua Mwongozo huo iliyofanyika Mkoani Pwani Disemba 22, 2021
Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Mashimba Ndaki (kushoto)
akimkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mhe. Abubakar Kunenge nakala ya Mwongozo wa
Upatikanaji, Usimamizi na Uendelezaji wa Maeneo ya Malisho katika hafla fupi ya
kuzindua mwongozo huo iliyofanyika Mkoani Pwani Disemba 22, 2021.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni