Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Novemba, 2021

TAASISI ZA FEDHA ZAHIMIZWA KUTOA MIKOPO KWA WAVUVI NA WAFANYABIASHARA WA DAGAA

Picha
Taasisi za kifedha nchini zimehimizwa kutoa mikopo kwa wavuvi na wafanyabiashara wa dagaa kwa kuwa zao hilo lina tija kiafya na kiuchumi. Hayo yamesemwa leo (26.11.2021) na Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Abdallah Ulega wakati alipotembelea mwalo wa Igombe wilayani Ilemela mkoa wa Mwanza baada ya kufika kwenye moja ya banda linalotumika kukaangia dagaa na kukutana na wafanyabiashara hao. Naibu Waziri Ulega amesema kuwa umefika wakati wa taasisi za kifedha pamoja na Halmashauri kuanza kuliangalia kundi hilo ambalo likiwezeshwa litaweza kuwahakikishia watanzania kuondokana na utapiamlo lakini pia kuongeza kipato kwa wahusika na taifa kwa ujumla. “Dagaa ni zao la kimkakati kutokana na umuhimu wake kiafya na kiuchumi ndio maana tunaendelea kuzihamasisha taasisi za kifedha kuwakopesha wavuvi na wafanyabiashara wa dagaa ili waweze kuvua dagaa wengi kwa kutumia zana za kisasa, kuwahifadhi katika mazingira mazuri na kusafirishwa katika maeneo mbalimbali ya ndani na nje ya nchi,” alisema ...

ZALISHENI NYAVU KWA KUZINGATIA UBORA - ULEGA

Picha
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Abdallah Ulega amekitaka kiwanda cha kuzalisha nyavu za kuvulia dagaa cha Ziwa Net kuzalisha nyavu hizo kwa kuzingatia ubora.   Naibu Waziri Ulega ameyasema hayo leo (25.11.2021) wakati alipotembelea kiwanda hicho kwa lengo la kuona namna uzalishaji wa nyavu hizo unavyokwenda ambapo uongozi wa kiwanda hicho umetakiwa kuzingatia ubora katika uzalishaji wa nyavu lakini pia kuhakikisha wanazalisha nyavu za kutosha ili wavuvi wasipate shida kuzitafuta.   Kwa upande mwingine Naibu Waziri Ulega amempongeza mwekezaji huyo wa Kiwanda cha Ziwa Net kwa uamuzi wake wa kujenga kiwanda hicho lakini pia kwa kutoa ajira nyingi kwa wanawake ambapo kati ya waajiriwa 18 wanaweke ni 15. Vilevile amewasihi kuhakikisha wanazingatia misingi ya ajira na kuhakikisha hakuna unyanyasaji wa watumishi. Lakini pia amewashauri kuendelea kuwekeza katika utengenezaji wa nyavu za aina nyingine zikiwemo za kuvulia samaki pamoja na nyavu maalum za kutengenezea vizim...

UWEKEZAJI KWENYE DAGAA NI MUHIMU KIAFYA NA KIUCHUMI

Picha
Uwekezaji kwenye zao la dagaa ni muhimu kiafya kwa kuwa utasaidia wananchi kuondokana na utapiamlo lakini pia utawanyanyua wananchi kiuchumi.   Hayo yamesemwa leo (24.11.2021) na Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Abdallah Ulega wakati alipotembelea mialo ya Igabilo na Rushara iliyopo wilayani Bukoba mkoa wa Kagera kwa ajili ya kusikiliza na kutatua kero za wavuvi ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi, Ndugu Shaka Hamdu Shaka.   Naibu Waziri Ulega amesema dagaa watasaidia sana kuondoa utapiamlo kwa kuwa wana protini, madini ya chuma na madini mengine ambayo ni muhimu kwa afya ya binadamu. Pia amesema itawashangaza sana watu endapo maeneo ambayo kuna dagaa wengi watoto wawe na tatizo la utapiamlo. Hivyo wavuvi wamehimizwa kutumia njia bora za uanikaji wa dagaa ikiwa ni pamoja na kuwahifadhi vizuri ili wasipoteze ubora.   Vilevile wavuvi na wafanyabiashara wa dagaa wamehimizwa kuwekeza katika zao hilo ili waweze k...

NAIBU WAZIRI ULEGA AWATAKA WAFUGAJI KULIMA MALISHO

Picha
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Abdallah Ulega amewataka wafugaji hapa nchini kulima malisho kwa ajili ya mifugo yao. Naibu Waziri Ulega ameyasema hayo leo (23.11.2011) wakati alipotembelea shamba la malisho ya mifugo kwenye kitalu cha NARCO ambacho kinatumiwa na Kampuni ya Kahama Fresh wilayani Karagwe mkoa wa Kagera. Akiwa katika shamba hilo lenye ukubwa wa ekari 400, Naibu Waziri Ulega amesema wafugaji wanatakiwa kulima malisho na kuacha kutegemea malisho ya asili peke yake. Lakini pia amesema ipo fursa kubwa kupitia kilimo cha malisho kwa wafugaji na wasio wafugaji kwani kufanya biashara ya malisho ya mifugo kutawawezesha kujinyanyua kiuchumi. Naibu Waziri Ulega ametembelea kuona ujenzi unaoendelea wa kiwanda cha vyakula vya mifugo pamoja na kiwanda cha maziwa, ambapo ameipongeza Kampuni ya Kahama Fresh kwa kuamua kufanya uwekezaji huo. Vilevile ametembelea kuona mifugo inayomilikiwa na Kampuni hiyo ambapo amesema kuwa mwekezaji huyo ameonesha mfano mzuri wa matumizi ya ardhi...

HALMASHAURI ZAHIMIZWA KUZINGATIA MPANGO WA MATUMIZI BORA YA ARDHI

Picha
Halmashauri zote nchini zimehimizwa kuzingatia mipango bora wa matumizi ya ardhi ikiwemo  kuweka njia za Mifugo zitazowawezesha kwenda  kwenye Malisho, maji na kwenye Masoko Ili kuondokana na migogoro isiyo ya lazima baina ya wafugaji na watumiaji wengine wa ardhi. Rai hiyo ilitolewa na  Kaimu Mkuu wa Kitengo cha mazingira Wizara ya Mifugo na uvuvi  Sekta ya Mifugo, Bw. Yusuf Selenge katika mafunzo ya  ufugaji endelevu unaokabili mabadiliko ya tabia nchi yaliyofanyika Mkoani Geita Novemba 15, 2021. Akiongea katika mafunzo hayo alisema kuwa  asilimia kubwa ya migogoro inatokana na baadhi ya vijiji kutokuwa na mipango ya matumizi bora ya ardhi na kusabisha njia za kupitisha mifugo ikitumika kwa matumizi mengine. “hii programu itasaidia sana kwa sababu imehimiza matumizi bora ya ardhi kwa hiyo Halmashauri wanatakiwa kutafuta wafadhiri na mapato yao ya ndani kuweza kutekeleza mpango huo kwa sababu njia za kupitisha mifugo zilikuwepo lakini zimevamiwa kwa ...

WAVUVI WATAKIWA KUKATA BIMA YA JAHAZI

Picha
Waziri  wa Mifugo  na Uvuvi, Mhe. Mashimba Ndaki amewataka wavuvi  kukata bima ya jahazi ili iwasaidie kuwakinga wanapokumbwa na majanga wakati wakitekeleza majukumu yao ya kila siku. Mhe. Ndaki ameyasema hayo wakati akizindua bima ya Jahazi kwa wavuvi iliyoandaliwa na benki ya NMB kwa kushirikiana na Britam Insurance katika tukio lililofanyika jijini Mwanza Oktoba 31, 2021. Amesema siku za nyuma bima ilikuwa inawaangalia wavuvi wakubwa pekee na kwamba kwa sasa NMB na Britam wamekuja na aina mpya ya kuwasaidia wavuvi wadogo na wa kati. "Niwapongeze na kuwashukuru sana benki ya NMB pamoja na washirika wao kuja na hii bima ya jahazi ambayo sasa wavuvi na wote katika Sekta ya Uvuvi wataweza kufanya kazi zao kwa kujiamini kwa kuwa endapo watakumbwa na janga watakuwa na uhakika wa kinga ya vyombo vyao wakitambua kuwa bima ipo na watarejea katika kazi zao," amesema Mhe. Ndaki. Ameongeza kuwa kwa kutegemea bima kunaongeza kujiamini na kujiamini huko kunaongeza ari ya kuf...

SERIKALI YAGAWA VIFARANGA 2600 KWA VIKUNDI VYA KINAMAMA MKURANGA

Picha
Katika jitihada za kuwakwamua kiuchumi wananchi hususan kinamama, Serikali kupitia Wizara ya Mifugo na Uvuvi imegawa Vifaranga 2600 kwa   mashamba darasa mawili   katika kata ya Vikindu na Kimanzichana vilivyopo wilayani Mkuranga, mkoani Pwani. Akizungumza mara baada ya kugawa vifaranga hivyo Novemba 9, 2021,   Kaimu Mkurugenzi Msaidizi kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Idara ya utafiti na   mafunzo, Dkt. Hassan   Mruttu   alisema vifaranga hivyo vitakaa katika mashamba hayo   kwa   wiki nne kabla ya kusambazwa katika vikundi 17 vya Wilaya hiyo. Alisema    pamoja na kuwepo kwa vifaranga hivyo, pia vikundi hivyo vitapewa chakula cha kuvikuza   pamoja na wataalamu wa kusaidia ukuaji wa kuku katika Wilaya hiyo. "Tumepokea vifaranga 2600, tumegawa katika mashamba darasa mawili   katika kikundi cha Kisawani na kikundi cha tujikomboe   hivi vitakaa hapa kwa wiki 4 na baadaye tutavisambaza kwa vikundi 17, ili kuwasaidia wak...

BILIONI 50 KUANZISHA UJENZI WA BANDARI YA UVUVI KILWA MASOKO

Picha
Serikali imetenge fedha shilingi bilioni 50 kwa ajili ya kuanza kutekeleza mradi wa ujenzi wa Bandari ya Uvuvi ambayo itajengwa Wilayani Kilwa mkoani Lindi.   Hayo yamesemwa leo (09.11.2021) na Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi anayesimamia Sekta ya Uvuvi, Dkt. Rashid Tamatamah wakati wa makabidhiano ya eneo hilo la mradi kwa Mshauri Elekezi wa kampuni ya Sering kutoka nchini Italia, kwa ajili ya kukamilisha kandarasi ya upembuzi yakinifu utaopelekea kujulikana kwa gharama za mradi huo na kutangaza zabuni ya ujenzi wa bandari hiyo.   Dkt. Tamatamah amesema kuwa ujenzi wa bandari ya uvuvi ni moja ya mkakati wa serikali katika kuhakikisha inaendelea kukuza sekta ya uvuvi hasa katika kuhamasisha uwekezaji na hivyo kuongeza mchango wa sekta ya uvuvi  katika pato la taifa.   “Ujenzi huu wa bandari ya uvuvi unakwenda sambamba na ununuzi wa meli mbili (2) kubwa za uvuvi  ambazo zitafanya uvuvi katika bahari kuu   lakini serikali pia inalifufua...