Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi mheshimiwa Abdallah Ulega ameiagiza Bodi ya Nyama nchini kuanzisha mfumo utakaosaidia wafugaji kunenepesha mifugo yao ili waweze kunufaika zaidi na fulsa za masoko ya ndani na nje ya nchi kwani mahitaji ya nyama ni makubwa.
Amesema hayo
wakati akizungumza katika mkutano maalumu na wafugaji wa kienyeji, wafugaji wa
kisasa pamoja na taasisi wezeshi za wafugaji wafuge kibiashara ili waweze
kutoshereza soko la ndani na soko kubwa la nje ya nchi katika ukumbi wa Mvuvi
house jijini Dar es salaam.
Mheshimiwa
Ulega alisema elimu ya kutosha iendelee kutolewa ili kuwajengea uwezo wa
kunenepesha mifugo yao hata wafugaji wa kienyeji katika ng’ombe, mbuzi na
kondoo wao wa asili maana taifa limepata fulsa kubwa huko katika nchi za
uarabuni hivyo mahitaji ya nyama ni makubwa.
Alisema
katika halmashauri zote nchini wafugaji wa fundishwe namna moja ya kunenepesha
na kuzalisha kwa wingi mifugo yao huku wakijua soko la ndani na nje ya nchi
linachotaka ili kupata nyama yenye ubora na yenye thamani ya kimataifa
itakayompa mfugaji faida kubwa.
Akizungumzia
wafugaji kukopesheka kwenye mabenki ya mifugo nchini Mheshimiwa Ulega alisema
Wafugaji waingie mikataba na wenye viwanda vya kuchakata nyama kwa namna
wanavyowasambazia mifugo yao ili wapate thamani ya kuweza kukubalika na
kuaminiwa kupata fulsa za fedha katika mabanki hayo.
“Mikataba
watakayopata itakuwa sehemu ya wao kukubalika Wafugaji wapate fedha kwenye
mabanki wanenepeshe mifugo yao wauze kimataifa wapate pesa maana biashara ni
nzuri sana” alisema Mheshimiwa Ulega.
Alisema lengo kubwa
likiwa ni kuwajengea uwezo wafugaji
kuzalisha kiwango
kikubwa cha nyama kitakachoweza kutoshereza mahitaji ya soko la ndani na soko
la nje ya nchi katika ubora wa nyama iliyoandaliwa vyema.
“Ukiandaa
vizuri nyama yako mteja akiiona ni nzuri na yenye ubora utafanya biashara maana
soko lipo” alifafanua.
Hatahivyo
Naibu Waziri huyo alisema hadi sasa viwanda vya kuchakata nyama za ng’ombe,
mbuzi na kondoo nchini bado vinazalisha chini ya viwango vya idadi iliyohitajika
kuzalisha katika viwanda hivyo kutokana na kukosekana kwa idadi kubwa ya mifugo
hiyo hivyo aliwataka watanzania kutumia vyema fulsa hiyo kwa kufuga kwa wingi
ilikuweza kutoshereza soko.
Aidha
Mheshimiwa aliitaka pia bodi hiyo ya nyama kutafuta namna ya kufundisha
wafugaji wa asili wabadilike kwa kufuga kisasa zaidi hata kuachana na ufugaji
wa kuzurulisha mifugo bali uwe ni ufugaji katika ubora na viwango vya kimataifa
katika mashamba yao ya ufugaji.
Naye Afisa
manunuzi wa Tanchoice cha kibaha mkoani Pwani Jabil Mohamed alisema kiwanda
chao kinauwezo wa kuchinja mbuzi 4500 kwa siku na ng’ombe 1000 kwa siku lakini
mpaka sasa wanapata idadi ya mifugo chini ya idadi wanayohitaji kulingana na
uwezo wa kiwanda ambapo wanachinja mbuzi hadi 2000 kwa siku na ng’ombe 150
“Jambo
ambalo uzalishaji wetu bado ni kiwango kidogo sana sawa na asilimia 20 cha
kiwanda chetu hivyo kiwanda hicho ni fulsa kwa wafugaji kwani inaweza kuwatoa
kwenye umasikini hadi mafanikio ya utajiri” alisema Jabil.
Jabil
alisema kiwanda hicho mpaka sasa kina vibali vya kupeleka nyama katika nchi
tano duniani.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni