Kaimu Mkurugenzi Idara ya Uvuvi Bw. Stephen Lukanga amesisitiza uvuvi endelevu ili kuleta faida za kiuchumi kwa Taifa na kwa Wananchi walio Katika mnyororo wa thamani.
Lukanga amesema hayo leo 15.07.2021 kwa niaba ya Mkurugenzi wa Idara ya Uvuvi wakati wa ufunguzi wa warsha ya Mazungumzo juu ya matumizi ya Utafiti Katika kufanya maamuzi ya Usimamizi wa Rasilimali za Uvuvi (science- management Dilogue) uliofanyika Katika Ukumbi wa Mkapa Jijini Dodoma.
Amesema Serikali kupitia Idara za Maendeleo ya Uvuvi imekuwa mstari wa mbele kuhakikisha kuwa Uvuvi Katika Bahari ya Hindi unakuwa endelevu na wa manufaa zaidi .
Bw. Lukanga alieleza kuwa , Serikali ilisaini Barua ya makubalianao na Shirika la Kilimo na Chakula la Umoja wa Mataifa chini ya mpango wa EAF - Nansen kutekeleza Mradi mdogo wa Utekelezaji wa mpango wa Usimamizi wa Samaki wanaopatikana Katika tabaka la juu la maji Katika Ukanda wa Bahari ya hindi.
“Lengo la Mradi ni kusaidia Utekelezaji wa mpango wa Usimamizi wa samaki wanaopatikana katika Tabaka la juu ya maji ulioandaliwa mwaka 2010 mpaka 2013 na Serikali kwa kushirikiana na FAO ili kuimarisha uendelevu wa rasilimali ya samaki wadogo na Dagaa, amesema Lukanga.
Aliendelea kuwa mradi una lengo wa kuimarisha uwezo wa Wizara na wadau wake Katika kutekeleza mpango wa kusimamia samaki kwa kuzingatia mzunguko wa Usimamizi wa Uvuvi Fisheries Management Cycle (CFM) kwa kuzingatia mfumo wa Ikolojia na Mazingira ( Ecosystem Approach to Fisheries Management)
“Niwaombe tushiriki kikamilifu ili kuona namna ambayo tunaweza tukafanya Uvuvi huu kuwa endelevu na kuleta faida za kiuchumi kwa Taifa lakini pia kwa Wananchi walio katika mnyororo wa thamani , amesema Lukanga.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Utafiti wa Uvuvi Nchini (TAFIRI) Dkt. Ismael Kimirei amesema, kazi kubwa ya Taasisi hiyo ni kukuza, kuratibu na kufanya Utafiti ambapo anaamini majadiliano hayo yamelenga , kujenga na kuboresha Tafiti Katika kusimamia Rasilimali za Uvuvi.
Baadhi ya Watendaji Wakuu wa Taasisi, Wakala, Wakurugenzi wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi , Watafiti kutoka TAFIRI na Wawakilishi kutoka WWF, TuNA Alliance wakisikiliza kwa makini hotuba kutoka kwa Kaimu Mkurugenzi Idara ya Uvuvi Bw. Stephen Lukanga kwa niaba ya Mkurugenzi wa Idara ya Uvuvi leo 15.07.2021 katika Ukumbi wa Mkapa, Dodoma.
Afisa Uvuvi Mwandamizi Kitengo cha Uendelezaji wa Rasilimali za Uvuvi Bi. Upendo Hamidu akizungumzia juu ya uboreshaji wa tafiti Katika kufanya maamuzi ya Usimamizi wa Rasilimali za Uvuvi leo 15.07.2021 Ukumbi wa Mkapa, Dodoma.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni