Nav bar

Jumatatu, 1 Julai 2019

UTAYARI WA MATAIFA YETU KATIKA KUPAMBANA NA MAGONJWA YA MIFUGO.




Kwa sasa nchi ya Tanzania inauwezo wa kutengeneza dawa ya kudhibiti baadhi ya magonjwa ya mlipuko katika taasisi ya TVLA iliyopo Kibaha jijini Dar es salam, ikiwemo dawa ya ugonjwa Wa kimeta ambayo imeonekana kuwa tishio kwa Mifugo ,wanyamapori na binadamu.

Alisema hayo Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega kwenye ufunguzi wa zoezi la majaribio ya udhibiti Wa magonjwa ya milipuko katika eneo la mpaka Wa Namanga unaoinganisha nchi ya Tanzania na Kenya ,utakao endeshwa kwa siku nne na wanachama Wa jumuiya iliyofanyika Mpakani Namanga.

Alieleza kuwa ,Wizara yake imejipanga vizuri dhidi ya magonjwa ya mlipuko kwa mifugo, na zoezi hili linaloendelea lipo chini ya umoja Wa afrika mashariki lakini wanashirikiana kwa pamoja katika kuhakikisha utayari Wa nchi wanachama unatekelezeka,hata sasa wamefanikiwa kudhibiti ugonjwa wa Kimeta ambao una athari kwa Mifugo,wanyamapori na binadamu

Alifafanua kuwa,kuna wataalamu wakutosha wanaoshughulikia magonjwa haya pindi yanapo tokea chini ya Ofisi ya Waziri mkuu inayohusika na maafa na kueleza kuwa Mifugo ya Tanzania ni salama kwani wanapatiwa chanjo Mara kwa Mara,lakini pia tuna wataalamu wetu katika vituo hivi vya pamoja (OSBP) na katika maeneo ya mkoani

Alidai kuwa Mifugo mingi ya Tanzania inauzwa Nchi Jirani ya Kenya nakuwataka wananchi jirani wa kenya kuondoa hofu juu ya Mifugo hiyo kwani kabla haijapelekwa huko kibiashara inafanyiwa Ukaguzi na vipimo mbali mbali na wataalamu ,na endapo Mifugo akibainika kuwa na ugonjwa hawezi kusafirishwa kibiashara kwenda nchi nyingine.

Magonjwa haya yanatoka kwa Mifugo kwenda kwa wanyamapori hadi kwa binadamu hususani kimeta,tumejipanga ipasavyo,tunayo taasisi inayojihusisha na utengenezaji wa dawa ya kimeta ikiwemo taasisi ya TVLA iliyopo kibaha; alisema Ulega



Naibu waziri Abdallah Ulega akitoa hotuba yake kwa ufupi kabla ya uzinduzi.




Maongezi kati ya Mawaziri kutoka Tz mara baada ya zoezi hilo kufanyika  katika mpaka wa Tanzania na Kenya, Namanga


Waziri wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Mhe. Adan Mohamed akisalimiana na Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega mara baada ya kiwasili mpakani Namanga.

 

 







Hakuna maoni:

Chapisha Maoni