Waziri wa mifugo na
uvuvi Mhe. Luhaga Mpina (Mb) ateketeza vipande vya nyavu haramu 773 zenye chini
ya mil 10 ambazo zilikutwa katika maeneo ya Kigombe,Moa na Tanga Jiji Mkoani
Tanga.
Kufuatia tukio hilo
la uteketezaji wa nyavu haramu hizo Mhe Waziri wa Mifugo na Uvuvi amesema, jitihada
zinazofanywa na serikali ni kuzuia uvuvi haramu na kulinda rasilimali za
Wavuvi.
“Tutahakikisha
wavuvi wetu wanapata elimu juu ya uvuvi na kufata sheria, kanuni na taratibu za
uvuvi zilizowekwa, alisema mpina.
Pia Waziri Mpina
alisema kuwa tarehe 1/07/2019 kanuni mpya ya uvuvi zitaanza kutumika ambapo itakuwa imeondoa changamoto
ambazo zinazotukabili.
Waziri Mpina
alisema pia, jitihada zinazofanywa na serikali ni kuzuia uvuvi haramu na kulinda
rasilimali za Wavuvi.
“Tunatumia Bil.56
kila mwaka kuagiza Samaki kutoka nje ya Nchi”, alisema Mpina
Waziri Mpina
alisistiza kuwa nyavu zote zenye chini ya milimita 10 zikabidhiwe Wizarani na
nyavu za kuanzia milimita 8 hazitaruhusiwa kuvuliwa na zitatakiwa zichomwe
moto.
“Nyavu hizi ambazo
hazitakiwi zinaua mazalia ya samaki na kuvua samaki wachanga wasioruhusiwa, anaevua
kutumia uvuvi haramu katika mnyoro mzima wa shughuli za uvuvi hatapona”.
alisema Mpina
Mpina alisema, tutaendelea
kupambana na uvuvi haramu Kila mtu afate sheria na taratibu zilizowekwa na tunashirikiana
na viongozi wetu kujua mahitaji na kutembelea wavuvi ili tuwasaidie wavuvi
wetu. - Mpina
Kwa upande wake
Mkurugenzi wa Jiji la Tanga Bw. Daudi Mayeji Wawekezaji uvuvi alisema,
tukizingatia kufuata sheria, kanuni na taratibu zilizopo ili tuwe na uvuvi
wenye tija.
“Natoa elimu kwa wavuvi kuwa,wanavua samaki ambao
hawastahili matokeo yake uzalishaji unakuwa mdogo”, alisema Bw. Daudi Mayeji.
Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mh. Luaga Mpina akiteketeza vipande vya nyavu haramu 773 mkoani Tanga |
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni