|
Haya yalibainishwa
jana na Katibu Mkuu wa sekta ya uvuvi Dkt. Rashidi Tamatama Wakati akifungua mkutano wa kutoa maoni kwa
wadau wa uvuvi toka kanda ya kati Dodoma
kwenye ukumbi ya Holly Cross Jijini Dodoma.
Katibu Mkuu huyo alisema kuwa sheria hiyo mpya ya ukuzaji
viumbe maji itajenga mazingira mazuri kwa wadau wa uvuvi kufanya kazi zao bila
vikwazo.
Aliendelea kusema kuwa sheria mpya itasaidia kujenga serikali
ya awamu 5 ya uchumi wa viwanda vya kati katika sekta ya uvuvi.
Katibu Mkuu huyo aliwaambia wadau hao kuwa serikali itawezesha
sheria hiyo ya ukuzaji viumbe maji ili kufikia mahitaji sera ya Taifa ya uvuvi
ya mwaka 2015 ilivyosema mikakati imeelekezwa kuendeleza rasilimali ya mazao ya
baharini ikiwemo samaki.
Dkt. Tamatama alisema kuwa sera ya Taifa ya Uvuvi pia
inalenga kuendeleza ukuaji viumbe maji ambavyo ni pamoja na kuunda rasilimali
ya samaki pamoja na viumbe wengine wa baharini.
Aidha alisema sheria mpya itasaidia nchi kwenda na mabadiliko
ya sayansi na teknolojia zinazotumika katika sekta ya uvuvi.
Vilevile Katibu Mkuu Dkt. Tamatama amesema sheria mpya
itasaidia kuipatia serikali uhalali wa kufanya kazi ili kuboresha ulinzi wa
rasilimali ya uvuvi na mazao yake.
Hivyo Katibu Mkuu huyo alisema sheria hii inakuja kwa wakati
muafaka, wakati idadi kubwa ya wanajihusisha na ufugaji wa samaki kama chanzo
cha kuongeza kipato cha maisha yao.
Mkutano huo uliwakutanisha wavuvi, wafanyabiashara ya samaki
ambao walitoa maoni yao mbalimbali ili kuboresha rasimu ya sheria hiyo mpya
kabla ya kwenda bungeni kujadiliwa na kupitishwa.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni