Mwekezaji katika sekta ya mifugo
mkoani Mara, Mh. Vedastus Matayo, ambaye pia ni Mbunge wa jimbo la Musoma mjini,
baada ya kutembelewa na Dawati la sekta binafsi kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi ameamua kuanzisha kiwanda cha nyama mkoani hapo ili kuboresha soko la
mifugo katika mkoa huo na ajira
watanzania.
Hayo yalibainishwa hivi
karibuni na Mbunge huyo wakati alipotembelewa na Dawati la sekta binafsi katika maeneo ya shughuli zake za ufugaji Wilayani Sengereti na Bunda, kwa lengo la kuibua na kushawishi kuwekeza kibiashara
kwa Mbunge huyo.
Mbunge huyo aliwambia
wataalam hao wa Dawati kuwa ana mifugo aina, Ng’ombe zaidi ya 2000 aina ya
Borani ambao ndiyo wengi na aina nyingine ya semental ambao ni wachache, mbuzi
zaidi ya 2500 na kondoo zaidi ya 1000, mifugo yote hii iko wilaya za Bunda na
Sengereti.
Aidha aliwaeleza aina ya
ufugaji anaofuga wa kugoresha mifugo hiyo ya asili kwa njia ya uhimilishaji kwa
kuchukua mbegu bora za mifugo toka NAIC Arusha na kuja kuchanganya na ng’ombe
wetu majie wa asili ili kupata ng’ombe chotara mwenye uwezo wa kutoa nyama
nyingi na maziwa mengi kuliko wale wa kienyeji.
Aliwaeleza wanadawati hilo la
sekta binafsi kuwa kwa kufanya hivyo
ameweza zalisha mifugo mingi ambayo soko lake likawa ni changamoto, hivyo
kuhitaji kuwa na kiwanda cha kuchakata nyama mkoa wa Mara.
Akizungumzia soko la mifugo
hiyo baada ya kuizalisha kwa wingi na kuinenepeshamifugo hiyo alisema kuwa
anauza kwa wenyeji wenye mabucha mkoani Mara na wakati mwengine huwauza nchi,
nchini Kenya ng’ombe wa nyama.
Aidha kwa upande wa ng’ombe wa
maziwa ambapo chotara hutoa maziwa mengi kiasi kuliko wale wa asili hufanya
matumizi ya familia yake na wafanyakazi katika shughli zake za ufugaji na
kilimo.
Kutokana na rasilimali hiyo
kubwa aliyokuwanayo bwana Matayo ya mifugo na soko la mifugo hiyo ni changamoto
kutegemea mkoa wa Mara tu na nchi jirani, dawati la sekta binafsi walimshauri
kuanzisha kiwanda cha kuchakata nyama ili rasilimali ya mifugo mingi aliyo nayo
ipate soko katika kiwanda hicho.
Vilevile wataalam wa dawati
walisema akianzisha kiwanda atazalisha bidhaa zitokanazo na nyama na kuziuza
kwa bei yenye manufaa kwa vile atakuwa ameongeza thamani badala ya kuuza
malighafi ya ng’ombe hai au mifugo hai, Mh. Matayo alikubaliana nao na
kuahidiwa atapatiwa mkopo toka Banki ya maendeleo ya kilimo (TADB) na watashirikiana
naye kuandaa andiko la mkopo huo wenye riba nafuu.
Mh. Mbunge wa Musoma mjini Mh. Vedastus Mathayo akiwa ofisini kwake akiongea na wataalamu wa dawati la sekta binafsi ambao hawaonekani pichani. |
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni