Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Agosti, 2018

UZINDUZI WA MAONESHO YA NANENANE KANDA YA KASKAZINI KATIKA VIWANJA VYA THEMI - ARUSHA.

Picha
Mgeni rasmi katika ufunguzi alikuwa Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Luhaga Mpina ambapo alipata fursa ya kujionea shughuli za mbalimbali za maonesho hayo yaliyofanyika katika viwanja vya Themi - Arusha tarehe 05/08/2018 #Nimetembelea mabanda na kujionea shughuli mbalimbali, nawapongeza sana kwa kazi nzuri, nimefurahishwa na maonesho kutoka Halmashauri na mashamba darasa, Alisema - Mpina #Vilevile kwa ufugaji bora mnaofanya , nimeona kwenye (paredi) kuna ng'ombe wanaotoa hadi lita 28, hongereni kwa kazi nzurii , Alisema - Waziri #Kauli mbiu yetu ya leo ni Wekeza katika Kilimo,Mifugo na Uvuvi kwa maendeleo ya viwanda, tukae tujiulize tunawekeza nini katika Sekta ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi na tunachangamoto zipi, Alieleza - Waziri #Aidha, kati ya ng'ombe mil 30 .5, ng'ombe mil 4 na laki 4 zote zinatoka ukanda wa kaskazini ambapo ni zaidi ya asilimia 10 ya ng'ombe wanatoka ukanda huu, Alieleza - Mpina #Pia kati ya Kondoo mil. 5.3 kondoo mil ...

KATIBU MKUU UVUVI DKT. RASHID ADAM TAMATAMAH AFANYA ZIARA WILAYANI MUSOMA.

Picha
Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi Sekta ya (Uvuvi) Dr. Rashid Tamatama amefanya ziara Wilayani Musoma Mkoani Mara katika kiwanda cha samaki cha Musoma Fish Processors. Akiongea na wafanyakazi katika kiwanda hicho, Dkt Tamatama amesema kuwa rasilimali ya uvuvi imepungua kwa kiwango kikubwa sana kitu ambacho sio kizuri kwa mustakabali wa maisha ya baadaye. Kipato cha mwananchi mmoja mmoja kimepungua kwa kiwango kikubwa na pia kumekuwa na ulaji wa wastani wa samaki ambao ni mdogo sana kwa Watanzania. alisema. Aidha, Katibu Mkuu Uvuvi Dkt.Tamatama alisisitiza kuwa hakuna malighafi za samaki zinazokuja kiwandani kwa ajili ya uchakataji hivyo kwa kutokuwa na malighafi hizo kunarudisha nyuma nguvu ya kufikia Tanzania ya Viwanda. Sisi kama Wizara yenye dhamana tumeliona hilo ndio maana tumekuja na operesheni mbalimbali ambazo zimeonyesha Mafanikio makubwa sana, kwani ukiangalia samaki waliopo viwandani na wanaoliwa na wananchi huko mtaani ni wakubwa na wan...

WAFUGAJI WAKUMBUSHWA KUFUGA KISASA

Picha
Wafugaji Mkoani Mwanza wametakiwa kufuga kisasa ikiwa ni pamoja na kuwa na  mifugo ya kutosha ili kuweza kupata tija na kufikia uchumi wa viwanda.                                                                                           Akiongea na wadau mbalimbali wa mifugo katika mnada wa Nyamatara Wilayani Misungwi Mkoani  Mwanza hivi karibuni, Katibu Mkuu Wizara ya  Mifugo na Uvuvi, Profesa Elisante Ole Gabriel amewataka wafugaji kujifunza mbinu bora za ufugaji ili sekta ya mifugo iweze kutoa mchango stahiki katika upatik...

Wizara imejipanga kudhibiti utoroshaji wa mazao ya mifugo na uvuvi- Mhe. Ulega; Simiyu.

Picha
Utoroshwaji  wa mazao ya  Mifugo na  Uvuvi kwenda nje ya Nchi bila kibali  pamoja na matumizi ya zana haramu za uvuvi vimetajwa kuwa ni baadhi ya changamoto kubwa zinazokwamisha juhudi za Wizara ya Mifugo na Uvuvi kuhakikisha kuwa sekta za Mifugo na Uvuvi   kuchangia mchango mkubwa katika pato la Taifa. Hayo yalibainishwa jana na Naibu Waziri wa mifugo na uvuvi Abdallah Ulega wakati wa ufunguzi wa maonesho ya nanenane kitaifa, yaliyofanyika katika viwanja vya Nyakabindi mjini Bariadi. Ulega alisema Wizara yake inachangia asilimia 30 tu katika uchumi wa Nchi wakati inauwezo mkubwa wa kuwekeza na kuchangia pato la Nchi kwa kiwango kikubwa. “Mchango wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi katika pato la Nchi ni mdogo sana ukilinganisha na sekta yenyewe, lakini sababu kubwa zinazokwamisha na kusababisha hayo ni wananchi wenyewe ambao baadhi yao wamekuwa wakitorosha mazao ya mifugo na bahari kwenda nje ya nchi bila kibali “Alisema Alisema kwa sas...