Naibu
Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega lifanya Ziara yake katika Wilaya
za Kibaha na Bagamoyo ya kuwatembelea wadau wa Ukuzaji viumbe kwenye maji
ambapo walipata fursa ya kueleza shughuli wanazozifanya pamoja na changmoto
wanazozikabili, hivyo lengo la ziara hiyo ni kukagua shughuli zilizopo katika
Sekta ya Uvuvi.
Naibu
Waziri alianza ziara yake kwa kuwatembelea na kuongea na wamiliki pamoja na
wafanyakazi wa Shamba la Ufugaji wa Samaki la Ruvu Wilaya ya Kibaha Kata ya
Mbwawa ambapo alipata fursa a kusikiliza shughuli zao na changamoto
zinazowakabili ikiwemo upatikanaji wa Chakula cha samaki.
Meneja
wa Shamba la Ruvu Bw. Kumbo alisema katika taarifa yake tatizo kubwa
linalowakabili ni upatikanaji wa chakula cha kuku pamoja na suala la
umeme."
"Tunashindwa
kumudu gharama za umeme ni kubwa sana kwa mwezi mmoja gharama yake ni milioni 3,
vilevile katika chakula cha samaki tunalazimika kuagiza nje ya nchi kwakuwa
chakula cha hapa hakina kiwango kinachotakiwa badala yake samaki hutumia muda
mrefu kuvuna".
Aliendelea
kusema tunatakiwa kuvuna samaki kwa Mwaka mara 2 , tukitumia chakula cha hapa
tunavuna mara 1 kwa mwaka na samaki anachukua muda wa miezi 9 mpaka kukua
lakini tukiagiza tunavuna mara mbili, samaki wanatumia miezi 6 mpaka kuku, tunataka tuwekeze katika
ufugaji huu lakini formula ndo tatizo letu kubwa alisisitiza
Mhe.
Ulega alisema vikwazo vya namna hii tutaviondo, tutaona ni namna gani ya kuweza
kupata chakula bora hapa kwetu sio mpaka tuagize, pia suala la umeme kuanzia
sasa naagiza Meneje wa Tanesco waje kushughulikia umeme hadi niwe nimepata
majibu wamefikia wapi.
Pia
Mhe. Ulega alipata fursa ya kuwatembelea na kuongea na Wanachama wa Chama cha
Ukulima na Umwagiliaji (CHAURU) kilichopo Ruvu na akapata fursa ya kuongea na
wamiliki wa mabwawa ya samaki ambapo kilio chao kikubwa kilikuwa ni namna ya
upatikanaji wa vifaranga vya samaki na masoko.
Bi.
Anzelina Masawe mmoja wa mmiliki wa mabwawa ya samaki alisema pia suala la elimu juu ya ufugaji
bora wa samaki wamekosa, hivyo aliomba wasaidiwe kupatiwa utaalamu zaidi wa
kufuga samaki na pia upatikananji wa vifaranga vya samaki umekuwa ni washida.
"Tunatakiwa
kuvuna Tani laki 7 za samaki kwa mwaka lakini uwezo wetu wa Tanzania ni Tani
laki 3.5, kwahiyo kuna upungufu wa Tani laki 3.5 ambapo zinahitajika, kwahiyo
ni fursa kwetu kuzalisha kwa wingi na kwa upande wa vifaranga wenzetu wa FETA
wanavifaranga wanauza shilingi 50 mkachukue kwa ajili ya kufuga alisistiza Mhe.
Ulega".
Naibu
Waziri alitembelea pia kiwanda cha kuzalisha vyakula vya kuku na samaki
inachoitwa Hill group, kilichopo Mapinga Wilaya ya Bagamoyo. Kampuni hiyo
inajihusisha na kutengeneza viroba vya kupakia bidhaa za viwanda na vilevile
utengenezaji wa vyakula vya mifugo kwa kutumia mashine za kisasa zaidi ambapo alifurahishwa na kiwanda hicho kwa
kuwa na tekinolojia ya juu zaidi
Meneja
wa kampuni hiyo Bw. Hillary Shoo alisema wanazalisha Tani 18 kwa saa moja kwa
chakula cha mifugo na Tani 1 kwa chakula cha samaki kinachoelea juu ya maji
ambapo kinatumia muda wa dakika 15 ili samaki aweze kula.
Aliendelea
kusema Meneja kuwa shida inayowakabili ni elimu ya watengenezaji wa vyakula
bora (Feed Millers) pia kwenye operesheni zinazoendelea faini imekuwa tatizo
kuna viwanda vimefungwa, imeathiri wenye mitaji midogo ambapo wanatakiwa kulipa
faini ndani ya masaa 24 kitu ambacho ni kipo nje ya uwezo wao.
"Nafahamu
eneo hili la chakula cha mifugo ni nyeti na katika moja ya azimio tuliojiwekea
ni eneo la ufugaji samaki na kuku, asilimia 80 ya Watanzania ni wafugaji wa
kuku katika Sekta hii ya ufugaji haifanyi vizuri sana, kilio kikubwa ni
upatikanaji wa vifaranga bora alisema Naibu Waziri".
Hivyo, sisi tumejipanga
vizuri na tumevipa nguvu vituo vyetu vya kuzalisha na kutotolesha vifaranga
Naliendele - Mtwara, Kibinzi - Kigoma, Feta - Mbegani na Nyegezi mwanza na
ukiacha hivi vikundi pia tunao watu binasi wa kuweza kutusaidia katika Sekta
yetu.
Mhe. Naibu Waziri akiongea na wafanyakazi wa shamba la ufugaji
wa Samaki la Ruvu Kata ya Mbawa Wilaya ya Kibaha alipotembea kuona shughuli zao
za uzalishaji
|
Mhe. Ulega akiwa na Meneja wa Ruvu Fish Farm Bw. Kumbo
akiwa amefuatana na Mkirugenzi Msaidizi Ukuzaji viumbe kwenye maji Bi. Ritha
wakikagua shamba na akipewa maelezo ya shughuli wanazozifanya
|
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni