Mhe.Waziri Luhaga Mpina akiwa na Katibu Mkuu Mifugo Dkt. Maria Mashingo akikata utepe kuashiria kupokelewa kwa Madume hayo ya Mbegu |
Maelekezo
ya Mhe. Waziri wakati alipokuwa akipokea madume ya ng'ombe bora 11 ya
mbegu katika Kituo cha Uzalishaji Mifugo kwa Chupa (NAIC) Arusha.
1.Amemshukuru
na kumpongeza KMM kwa kazi kubwa ya kuhakikisha utoshelevu wa mbegu za
AI kwa kuwepo kwa jumla ya madume bora 26 hadi sasa yenye uwezo wa
kuzalisha jumla ya dozi 3,120,000 kwa mwaka.
2.Amemuagiza
KMM kuandaa mpango maalum wa kuhimilisha Ng'ombe Milioni moja wa
maziwa.Mpango huo uanze kutekelezwa katika bajeti ya mwaka
huu(2018/19).
3.Pia Mhe.
Waziri amemuagiza KMM kufanya tathmini ya kuona kama kuna haja au
umuhimu wa kuagiza maziwa na mazao yake nje ya nchi.Tathimini hiyo
inatakiwa kukamilika katika kipindi cha wiki mbili kuanzia sasa.
4.Aidha
Mhe. Waziri amemuagiza KMM kufanya tathmini ya kuona kama maziwa na
mazao yake yanayoingizwa nchini yanaingia kwa kufuata taratibu zote za
kisheria. Tathmini hiyo pia ifanyike ndani ya wiki mbili kuanzia sasa.
5.Mhe.
Waziri ameonya wafanyabiashara wote Wanaoingiza bidhaa za maziwa na
mazao yake kwa njia za magendo, kuacha mara moja.Serikali itafanya
ukaguzi na itachukua hatua kali za kisheria kwa mfanyabiashara yoyote
atakayebainika.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni