Naibu Waziri wa
Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Mhe. Abdalah Hamis Ulega ambaye ni Mbunge wa Jimbo
la Mkuranga ameiambia kamati ya kudumu ya Bunge ya Kilimo Mifugo na Maji kuwa, Serikali
ina mpango wa kuifanya sekta ya Mifugo na Uvuvi kuwa na mchango mkubwa katika
pato la Taifa.
Naibu Waziri Hamisi Ulega
ameyasema hayo leo Mkoani Kigoma mbele ya Kamati ya kudumu ya Bunge ya Kilimo
Mifugo na Maji, ilipokuwa katika ziara ya kutembelea chuo cha wakala wa Elimu na Mafunzo ya Uvuvi
(FETA) kampasi ya kigoma jana.
Mhe. Ulega amesema
Wizara yake ina Mkakati wa kulinda rasilimali za Mifugo na Uvuvi, kwa kuimarisha
uvuvi wa bahari kuu na kuitoa sekta hiyo kwenye kuchangia kiasi na shilingi Bilioni 19
kwa mwaka katika pato la taifa hadi
kufikia kuchangia zaidi ya shilingi Bilioni 50 kwa mwaka.
“Tunaweza kufikia
malengo haya kwanza kwa kuimarisha uvuvi wa Bahari kuu kwa kuhakikisha kwanza
tasisi yetu ya kusimamia uvuvi wa bahari kuu inakuwa na nguvu kwa kuweka vizuri
sheria na kanuni zetu za uvuvi ikiwa ni pamoja na kufufua shirika letu la
TAFICO, Alisema Ulega.”
Sambamba na hilo,
Ulega alisema Serikali ina mkakati wa kuwa na Meli ambayo itakuwa na uwezo wa
kwenda kuvua na kuchakata mazao ya samaki, jambo ambalo litakwenda sambamba na
ufunguaji wa viwanda vya uchakataji wa mazao ya uvuvi.
Naibu Waziri Ulega
pia alisema serikali ina lengo la kuhamasisha uwekezaji katika sekta ya Uvuvi kupitia mafunzo, utafitu na elimu ya ugani kupitia vyuo vya Feta , ili
kuweza kuwa na wataalam wa kutosha
pamoja na kuipa nguvu wakala hiyo ili kuweza kutoa wataalam kwani mpaka sasa sekta ya uvuvi ina uhaba wa wataalam na kuongeza kwa kusema
kuwa kwa upande wa utafiti serikalii ina mkakati mkubwa wa kuweza kuiwezesha
TAFIRI kwa kuipa kazi maalum za tafiti akitolea mfano wa uelewa mdogo wa baadhi
ya wavuvi kuhusiana na zana halali za uvuvi.
Akizungumzia suala
la kuingiza samaki aina ya vibua na sato kutoka nje ya nchi, Ulega alisema, “Ukiangalia
kwa makini sioni sababu ya kwanini tutoe mathalani kiasi cha shilingi Bilioni
50 kwa mwaka tuwapelekee wavuvi wengine na tuingize tani elfu 20 na zaidi kuleta hapa ndani za samaki
ambao sisi wenyewe tunao.” Alisisitiza Ulega.
“ Ipo Mikakati kwa
serikali ya kuwatengenezea wafanya biashara ya samaki mazingira mazuri ili pesa
hiyo iwekezwe hapa nchini.” Alisema.
Awali akitolea
mfano wa ulinzi wa rasilimali za uvuvi Ulega alisema “Tumefanya ulinzi wa
rasilimali za uvuvi katika ziwa Victoria kwa muda mfupi tu ikiwa ni pamoja na
ulinzi wa utoroshwaji wa Mazao ya Uvuvi
nje ya nchi na tumeingiza kiasi kikubwa cha fedha.” Alisema.
Kwa Upande wake
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi kutoka Sekta ya Uvuvi Dkt. Yohana
Budeba alisema kuwa njia ya ufugaji wa samaki wa kisasa kupitia chuo cha FETA
kitatengeneza wataalam na kuongeza ajira na kupatikana samaki wengi na
kupelekea mchango mkubwa wa sekta ya uvuvi katika uchumi wa taifa hili.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni