Waziri
wa Mifugo na Uvuvi Mhe Luhaga Joelson Mpina amesema kuwa mnada wa pugu
utakarabatiwa na kuwa mnada wa kimataifa utakaokuwa unahudumia
wafanyabiashara kutoka nchi yoyote Africa na duniani kwa ujumla.
Tanzania
Mungu ametujalia kuwa na tunu ya Rasilimali ng'ombe,Nchi zilizoendelea
wanajivunia vitu vyao,Mfano viwanda,ifike wakati na Sisi tujivunie
Rasilimali ng'ombe tuyoliyopewa Mungu Bure.
"Haiwezekani
Sisi Tanzania tuwe wa pili africa kuwa na Mifugo mingi,tukitanguliwa na
nchi ya Ethiopia halafu tukose kuwa na mnada wa kimataifa"
Mpina
ameyasema hayo Leo alipofanya ziara ya kukagua eneo la mnada huo
lililovamiwa na wananchi na kujionea hali halisi ya uvamizi wa eneneo
hilo.
Pia baada ya
kuzungu na kukagua eneo la mnada huo na kushuhudia uvamizi mkubwa
uliofanyika katika eneo hilo,Mhe.Mipina ameunda timu maalumu itakayopita
nyumba baada ya nyumba kuchunguza na kuhoji uhalali wao wa kuwepo
katika eneo la Serikali na kujiridhisha ni nani aliyewauzia maeneo hayo
wananchi hao.
Aidha
Waziri Mpina amepiga marufuku ujenzi wa aina yoyote ile usifanyike
katika eneo hilo mpaka hapo serikali itakapotoa ripoti ya uchunguzi huo
ambapo utafanyika ndani ya mwezi mmoja kuanzia sasa.
Jumla ya kaya Elfu tano (5,000) za wavamizi hao zimetambuliwa na zinakadiliwa kuwa na watu elfu 22,8000.
Vilevile
baadhi ya Wafanyabiashara na wafugaji waliokuwepo mnadani hapo,
wamemweleza Mhe Waziri wa Mifugo na Uvuvi kuwa mnada huo unakabiliwa na
changamoto nyingi ikiwepo uchakavu wa Miundombinu ya kutunzia
Mbuzi,Ukosefu wa Maji,Ubovu wa barabara iendayo mnadani hapo na uhaba wa
maeneo ya kuchungia mifugo kutokana na Eneo la mnada huo kwa kiasi
kikubwa kuvamiwa na wananchi.
Katika
hatua nyingine Katibu Mkuu Mifugo Dkt Maria Mashingo amesema kuwa
wamefa nikiwa kuipata hati ya mnada huo baada ya kuitafuta kwa muda
mrefu sana.
"Eneo la
mnada wa upili wa Pugu lina ekari 1,900,kutokana na uvamizi wa eneo
hilo, mnada huo kwa sasa unakadiliwa kuwa na eneo lililobaki kwa ajili
ya matumizi sahihi ya mnada ni asilimia 25 tu.Hati ya eneo la mnada huo
ilitolewa mwaka 1939 na serikali ya wakati huo"Alisema
Awali
Waziri Luhaga Mpina alifika mnadani hapo majira ya saa kumi alfajiri
akiambatana na Katibu Mkuu Mifugo Dkt. Maria Mashingo na baadhi ya
Maafisa kutoka Wizarani.Kazi ya kwanza aliyoanza nayo mara tu baada ya
kufika mnadani hapo ni kukagua Vibali (Movement Permit) katika makundi
ya ng'ombe yote yalikuwepo kwa wakati huo.
Waziri
mpina akiwa katika mnada wa Mbuzi Pugu alifanikiwa kumkamata
mfanyabiashara mmoja wa Mbuzi aliyejulika kwa jina la Zacharia Mabula
(43) aliyekwepa kulipia ushuru wa Mbuzi 112 kati ya Mbuzi 228 aliokuwa
nao.Kwa kutumia sheria taratibu na kanuni zinazoendesha mnada
huo,mfanyabiashara huyo amepigwa faini ya Tsh.800,000/=
|
Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe, Luhaga Mpina kushoto akiwa na Katibu Mkuu Mifugo Dkt. Maria Mashingo wakiangalia malisho ya ng'ombe katika mnada wa Pugu
|
|
Mhe. Waziri wa Mifugo na Uvuvi Luhaga Mpina akiangalia mbuzi alipotembelea mnada wa Pugu ivi karibuni.
|
|
Mhe. Waziri wa Mifugo na Uvuvi Luhaga Mpina akiangalia ng'ombe akiwa mnadani
|
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni