Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Luhaga Mpina amewataka wafugaji nchini kutembea kifua mbele kwa kumpata yeye kama Waziri mwenye dhamana ya Mifugo, Mpina ameyasema hayo jana aliposhiriki katika zoezi la kupiga chapa Mifugo katika Kijiji cha Kyelwa kilichopo katika kata ya Katerero Halmashauri ya Wilaya Bukoba mkoani Kagera, na kuwataka viongozi kuzingatia maadili wakati wa utekelezaji wa zoezi hilo ili kuepuka hujuma na ubaguzi kwa wafugaji.
Waziri Mpina alipofika katika kata ya Katerero aliwakuta wafugaji
wamejitokeza kwa wingi kuunga mkono zoezi la upigaji chapa katika mifugo yao na
kushiriki zoezi hilo kwa kuonyesha msisitizo.
Waziri Mpina aliwataka wafugaji kuleta
mifugo yao kupigwa chapa na kusisitiza kwamba zoezi hilo ni la manufaa na faida kwa
wafugaji kwani litaweza kuwasiadia kuepuka maambukizi ya magonjwa ya wanyama
kwa mifugo yao kwa kutokuchanganyikana na mifugo mingine sambamba na kusaidia
upotevu wa mifugo.
Akiongea
katika zoezi hilo diwani wa kata ya Katerero Bw. Nuru Abdul Kabendera alisema
kuwa, amefurahishwa na ziara ya Waziri Mpina katika kata ya katerero kwani ni
mara ya kwanza kwa kata hiyo kupata ugeni kutoka katika ngazi ya juu ya
serikali na kumuomba Mpina kupitia Wizara yake kutatua changamoto inayoikabili
kata hiyo la josho la kuoshea ng’ombe
ambapo Waziri Mpina amehaidi kuitatua.
Katika
hatua nyingine Waziri Mpina ametembelea mapori ya Burigi yaliyopo wilayani
Biharamulo ambapo ameupongeza uongozi wa mkoa kwa uperasheni iliyofanyika ya
kuondoa mifugo katika mapori tengefu na hifadhi za misitu ambapo amewashuhudia
wanyama pori ambao tayari wamerejea katika mapori hayo huku mkuu wa wilaya hiyo
Bi Saada Malunda akiwataka wananchi wa wilaya hiyo kutoa ushirikiano katika
zoezi la kuondoa mifugo.
Aidha,
Mpina amewataka wakuu wa Mikoa ya mipakani kuwasilisha kwake taarifa ya
uondoshwaji wa mifugo katika mikoa yao mara baada ya kukamilika kwa zoezi hilo
la oparesheni ondoa mifugo.
Waziri
Mpina amemaliza ziara yake ya siku mbili mkoani kagera kubwa akiwa ameagiza
mifugo yote iliyokamatwa kutoka nje ya nchi itaifishwe na kupigwa mnada haraka
sana kwa mujibu wa sheria.
Waziri Mpina na baadhi ya viongozi
wa wilaya ya Bukoba wakielekea katika zoezi la upigaji chapa ng'ombe katika
kata ya katerero kijijini Kyelwa jana.
|
Katika picha inaonekana sehemu ya ng'ombe aliyepigwa chapa katika kata ya katerero kijijini Kyelwa jana |
Mpina akiongea na wanahabari mara baada ya ukaguzi wakati wa oparesheni ondoa mifugo katika sehemu ya pori la Bugiri Biharamulo, Kulia ni Mkuu wa Wilaya hiyo Bi Saada Malunde. |
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni