NAIBU WAZIRI WIZARA YA MIFUGO NA UVUVI MHE.ABDALLA HAMISI ULEGA AWASILI MAKAO MAKUU YA WIZARA MJINI DODOMA.
Kwa mara ya kwanza tangu ateuliwe na Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt.John Pombe Magufuli,Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdalla Hamisi Ulega amewasili makao Makuu ya Wizara,ofisini kwake Mjini Dodoma na kupokelewa na Viongozi Waandamizi wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi.
Katika adhima ya kutimiza kwa Vitendo ule Usemi wa "HAPA KAZI TU" mara tu baada ya kuapishwa kushika nyadhifa hizo,Viongozi hao wawili wa ngazi ya juu kabisa Wizarani yaani Waziri wa Mifugo na Naibu waziri,wamekuwa nje ya ofisi wakishughulika na changamoto za wafugaji na Wavuvi.
Awali Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe Abdalla Ulega alifanya ziara katika Mikoa minne ambayo ni Tanga,Kilimanjaro,Arusha na Mara, lengo ikiwa ni kuangalia changamoto mbalimbali za Mifugo inayoingia nchini kutoka nchi Jirani kinyume cha Sheria.
Mhe Abdallah Ulega akisalimiana na Katibu Mkuu Uvuvi Dkt.Yohana Budeba pamoja na Afisa Habari Mwandamizi Bw. John Mapepele. Baada ya kuwasili Makao Makuu Dodoma |
Mhr Abdallah Ulega akizungumza na baadhi ya Wakurugenzi na watumishi baada ya kuwasili ofisini kwakwe Dodoma Makao Makuu |
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni