Waziri anayeshughlia masuala ya Mifugo
na Uvuvi Mhe. Luhaga Mpina amekutana na Waziri wa Uwekezaji wa Oman Mhe. Salim
Al Ismail na kujadili suala zima la uwekezaji wa viwanda katika Sekta ya Mifugo
na Uvuvi.
Katika Mazungumzo hayo Waziri Mpina amemueleza Waziri huyo wa uwekezaji wa Oman kuwa
Tanzania imekuwa ikizalisha nyama kwa kiasi cha tani 36 kwa siku na imekuwa
ikifanya biashara kwa kuuza tani za nyama ambazo hazijakatwa katika nchi za
falme za kiarabu ikiwemo Oman.
Wakati umefika sasa kwa nchi hizi mbili
kushirikiana kwa pamoja katika Sekta hii kwa Oman kuwekeza katika Viwanda vya
ndani vya nyama kwa kuendeleza viwanda vilivyopo na hata kujenga Viwanda vipya,
akitolea mfano ujenzi wa kiwanda cha nyama cha Ruvu ambao umefikia 51%
kukamilika.
“Tunataka viwanda vyote vya nyama vya ndani vikidhi mahitaji
na kuweza kuuza nyama nje ya nchi”. Alisema Mpina.
Kwa upande wake Waziri Salim Al Ismail alipoelezwa kuhusu
viwango na madaraja mbali mbali ya nyama nchini na mmoja wa mtaalam kutoka
wizara hiyo, alisema kuwa Oman ipo tayari kuwekeza katika sekta ya viwanda vya
nyama na kuisaidia Tanzania kutafuta soko la Marekani kupitia Oman kwani nchi
hiyo ya Falme za kiarabu ina cheti na
kibali kilichothibitishwa na mamlaka ya chakula na dawa cha Marekani.
“Tunaweza
kuchukua nyama kutoka Tanzania na kuingiza Marekani bila kulipa Ushuru,
tunapaswa kuwa na vyeti halali ili kuweza kupata soko katika nchi nyingine,
Alisema Waziri Ismail.”
Waziri Ismail aliendelea kusema kuwa, Makampuni Binafsi
kutoka Oman yapo tayari kufanya biashara katika eneo hili hivyo ni wakati wa
Tanzania sasa kuonyesha utayari.
“Hizi bidhaa za nyama ni lazima zitoke kwenu sababu sisi
hatuna maji wala majani ya kulisha mifugo kama ngombe, mbuzi na kondoo ambao
huchinjwa kwa wingi baada ya Hijja. Alisisitiza.”
Kwa Upande wa Sekta ya Uvuvi Waziri Huyo wa Oman alisema Oman
imenunua teknolojia ya kisasa ya uwekezaji katika fukwe ya Bahari kutoka Texas
Marekani, Teknolojia inayojulikana kitaalam kama Shrim farming inayoruhusu uzalishaji wa chakula cha samaki
wavuliwao katika maji marefu bila kuharibu mazingira.
Alisema Tenkolijia hiyo inaweza kutumika katika uwekezaji wa Fukwe
ya bahari ya Hindi akitolea mfano eneo la bagamoyo kwa kuzingatia tathmini ya
athari ya mazingira na ujenzi wa miundombinu ya barabara ili kuwasaidia wavuvi
wadogo.
Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt Yohana Budeba (Sekta ya Uvuvi) Alisema ni furaha yake kuona
wafanya biashara wa Oman wanakuja kuwekeza Tanzania au kushirikiana na wavuvi
wa ndani kwani kuna samaki wengi wa kutosha kumudu viwanda vya kuchakata na kuwezesha biashara kubwa ya samaki.
|
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni