WAZIRI MPINA ACHOMA
NYAVU KUKOMESHA UVUVI HARAMU
NA MWANDISHI MAALUM
KIGOMA
Waziri wa Mifugo na uvuvi Luhaga Mpina ameteketeza nyavu
zinazotumika katika uvuvi haramu zilizokamatwa Mkoani Kigoma zenye thamani ya
shilingi Milioni thelalini na moja kuashiria kuanza rasmi kwa zoezi hilo katika
serikali hii ya awamu ya tano.
Akiongea mara baada ya kuteketeza nyavu hizo hizo mapema leo,
Mpina alionyesha kushangazwa na suala la uvuvi haramu kuwa sugu “kwa nini vita
hii haina mwisho? Lazima yawezekana mbinu zinazotumika ni dhaifu ama silaha
zinazotumika ni duni, ifike mahala suala hili
liwe historia”. Alisema Mpina.
Akitoa Maelekezo kwa viongozi wa Mikoa ambayo shughuli hizi
zinafanyika, Mpina aliwataka viongozi hao wawe na jukumu la kulinda rasilimali
za taifa ikiwa ni mapoja na Bahari, Maziwa na mito.
“kama nitashindwa kushughulia suala zima la uvuvi haramu,
niitaaachia dhamana hii niliyopewa na Mheshimiwa Rais, na mpaka kufikia hatua
hiyo lazima wengi watakuwa wamejuruhiwa.” Alisisitiza Mpina.
Akiwa katika ziara ya Oparesheni Maalum ya Ondoa Mifugo
kutoka katika mikoa ya mipakani na nchi jirani akiwemo Mkoani kigoma, Mpina Pia
alitembea mwalo mpya wa Kibirizi Mjini Kigoma na kumtaka Afisa Mifugo na Uvuvi
na Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigoma kushughulikia changamoto za mitambo wa
kugandisha barafu inayokikabili kikundi shirikishi cha rasilimali za uvuvi
mwaloni hapo pamoja na suala la kuwauzia dagaa wafanya biashara
wanaozisafirisha nje ya nchi. Waziri Mpina Pia alitembelea chuo uvuvi mjini
Kigoma.
Zoezi la opareshini ondoa mifugo na kukomesha rasmi uvuvi
haramu limeanza rasmi kwa viongozi wa Wizara husika wakiongozwa na mawaziri
Luhaga Mpina na Abdalah Ulega kuingia kazini katika mikoa inayokabiliwa na
changamoto hizo.
Katika Picha Nyavu zinazotumika katika uvuvi haramu zenye thamani ya shilingi milioni 31 zikiteketea kwa moto kuashiria kuanza rasmi kwa zoezi la kupambana na uvuvi haramu nchini. |
Katika picha Waziri wa Mifugo na Uvuvi Luhaga Mpina akiwasha moto kuteketeza nyavu zinazotumika katika uvuvi haramu Mjini Kigoma |
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni