Nav bar

Alhamisi, 7 Septemba 2017

WATAALAMU WA MIFUGO WATEMBELEA MKOA WA KAGERA KWA AJILI YA KAZI MAALUM YA KUAINISHA NA KUPIMA ENEO LA MWISA TAREHE4/09/2017

                             ENEO LA MWISA II KUAINISHWA NA KUPIMWA
Wataalamu wa mifugo kutoka Wizara ya Kilimo Mifugo na Uvuvi (Idara kuu ya Mifugo) wamewasili Mkoani kagera kwa ajili ya kazi maalum ya kuainisha na kupima eneo la Mwisa II.

Eneo la Mwisa II linakadiriwa kuwa na hekta zisizopungua 50,000 ni miongoni mwa maeneo yanayoangukia chini ya ukanda wa ufugaji ambao unaanzia mpakani mwa nchi ya Uganda hadi katika pori la akiba la Burigi katika ziwa Burigi  Wilaya ya Muleba na Karagwe Mkoani Kagera.

Ili kuhakikisha kazi hii ya Uainishaji na upimaji wa eneo la Mwisa II inafanyika kwa ufanisi mkubwa wataalamu kutoka Wizara ya Kilimo Mifugo na Uvuvi (Idara kuu ya Mifugo) watashirikiana na Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya makazi, OR - TAMISEMI (Mkoa na Wilaya) pamoja na NARCO.

Wizara ya Kilimo Mifugo na Uvuvi kupitia Idara yake kuu ya Mifugo inafanya kila linalowezekana kuhakikisha inatafuta maeneo kwa ajili ya wafugaji na kutoa elimu kwa wafugaji kufuga kwa tija, lengo ikiwa kupunguza migogoro ya Wakulima na wafugaji na hatimaye kuinua uchumi wa nchi na mtu mmoja mmoja kwa ujumla.

Awali Naibu Waziri wa Kilimo Mifugo na Uvuvi Mhe. William Tate Ole Nasha June 2017 alifanya ziara Mkoani Kagera na kuagiza eneo la Mwisa II lipimwe ili ligawiwe katika mfumo wa vitalu (Blocks) ili wapewe wafugaji wa Kitanzania watakaokuwa wameunda vikundi au Ushirika.


Moja ya Bicon zilizowekwa kuonyesha mpaka wa eneo la Mwisa II katika baadhi ya vijiji Wilayani Muleba


Wataalam wakishauriana sehemu nzuri ya kuchimbia BICON


Bi. Grace Mwaigomole kutoka Idara ya DPM akichimba shimo kwa kutumia sululu kwa ajili ya kuweka BICON katika eneo la Mwisa II Wilayani Muleba


Moja ya BICON iliyowekwa katika kijiji cha Kiteme kwa ajili ya mpaka wa eneo la wafugaji mwisa II


Baadhi ya maeneo ya kijiji cha Kiteme ambayo timu ya wataalamu ilifika kuyabainisha na kupima katika Wilaya ya Muleba

kazi za fildi zinahitaji ushirikiano mkubwa sana, hapa pia BICON itawekwa katika kijiji cha kasharara Wilaya Muleba

Ng'ombe aina ya Ankole waliopo katika tarafa ya Kimwani Wilayani Muleba

Hili ni birika la kunyweshea Mifugo maji, lililotengenezwa kienyeji na wafugaji, maarufu kwa jina la Kyeselelo lipo katika kijiji cha kakoma Wilayani Muleba


Bw. Basil Mataba akichimba shimo kwa ajili ya kuweka BICON katika kijiji cha kasharara
Hakuna maoni:

Chapisha Maoni