Nav bar

Jumatano, 27 Septemba 2017

KATIBU MKUU WIZARA YA KILIMO MIFUGO NA UVUVI (MIFUGO) DKT MASHINGO AFANYA ZIARA MKOANI TABORA KATIKA MNADA WA UPILI IPULI TAREHE 23/09/2017

 Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Mifugo na Uvuvi  (Mifugo)  Dkt. Maria Mashingo afanya ziara katika mnada wa upili Ipuli Manispaa ya Tabaora (Secondary Market).Lengo kubwa la ziara hiyo ilikuwa kujiridhisha na changamoto zilizopo katika mnada huo ambapo Manispaa ya Tabora wanaomba uhamishiwe eneo lingine.

Aidha Manispaa ya Tabora imeomba mnada wa Ipuli uhamishiwe eneo lingine  kwa sababu eneo ulipo sasa umezungukwa na makazi ya watu.Vile vile  Manispaa ya Tabora  imependekeza mnada huo urudishwe kuwa mnada wa awali ili uendeshwe na Manispaa ya Tabora.

Septemba 22 mwaka huu Katibu Mkuu Mifugo alifanya kikao na Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe .Agrey Mwanry kujadili namna bora ya kuweza kuuhamisha mnada huo na kuupeleka nje kidogo ya mji wa Tabora,lengo ikiwa ni kuuboresha mnada huo ambao kwa sasa umezungukwa na Makazi ya watu.

Awali katibu Mkuu Mifugo alikutana na kujadiliana na Mkurugenzi wa Manispaa ya Tabora Maeneo  bora ya kuhamishia mnada huo.Katibu Mkuu alishauri Manispaa ya Tabora iwasiliane na Wizara ili iweze kushauri maeneo hayo ya kuhamishia mnada yatakapokuwa tayari.  

Katibu Mkuu wizara ya Kilimo Mifugo na Uvuvi (Mifugo) Dkt Maria Mashingo akikagua Mnada wa Upili Ipuli akiwa pamoja na wafanyakazi  wa zone Veterinary Centre (ZVC) na Tanzania Veterinary laboratory Agency (TVLA) kanda ya Mgharibi Tabora na wawakilishi Ofisi ya RAS na Manispaa ya Tabora



Baadhi ya ng'ombe aina ya Anko walioonekana katika mnada wa Upili wa Ipuli Tabora

Katibu Mkuu Mifugo Dkt Maria Mashingo Kulia akiwa na Dkt Japheti Nkangaga (kushoto mwenye koti jeupe) katika mnada wa Ipuli wakati wa kikao na wafanyakazi wa Wizara,OR-TAMISEMI, ofisi ya RAS Tabora na Manispaa.




Katibu Mkuu Mifugo Dkt.Maria Mashingo  akiendesha kikao na kutoa ufafanuzi wa baadhi ya hoja zilizojitokeza wakati wa kikao hicho katika mnada wa upili Ipuli katika Manipaa yaTabora.















Hakuna maoni:

Chapisha Maoni