Nav bar

Alhamisi, 15 Desemba 2016

UTARATIBU WA KUPATA HUDUMA IDARA YA UKUZAJI VIUMBE KWENYE MAJI


 IDARA YA UKUZAJI VIUMBE KWENYE MAJI

Idara ya Ukuzaji Viumbe kwenye Maji ina jukumu la kuratibu mazingira rafiki ya uwekezaji kwa kutoa miongozo mbalimbali kutegemea na aina za uwekezaji. Taratibu za uwekezaji zitafuata miongozo na taratibu zilizopo kulingana na viwango vilivyopo nchini na kimataifa pamoja na kuzingatia hifadhi ya mazingira na uendelezaji wa rasilimali za uvuvi (Fisheries Investment Guidelines and  The Environmental management Act).
1.0 Mchango wa Idara ya Ukuzaji Viumbe kwenye Maji katika uwekezaji
 Idara ina wajibu wa kutoa ushauri juu ya mambo mbalimbali katika uwekezaji ambayo ni pamoja na;
  1. Taratibu za kufuata kabla ya uwekezaji;
  2. Sheria zilizopo;
  3.  Eneo linalofaa kwa uwekezaji;
  4. Aina ya viumbe wanaofaa kufugwa/kulimwa kwa kufuata kanuni za .uvuvi na "FAO code of conduct for transfer of species" (1988); na
  5. Teknolojia sahihi ambazo hazina athari kwa mazingira, zinazofaa kiuchumi na zinazokubalika katika jamii
2.0 Sekta au taasisi zingine za kupata taarifa na ushauri juu ya uwekezaji
Uwekezaji katika ukuzaji viumbe kwenye maji unajumuisha sekta na taasisi nyingi kutegemea na mradi au uwekezaji husika  kama:
1.    Idara ya misitu- kuangalia athari katika misitu hasa jamii ya mikoko na misitu mingine
2.    Idara ya wanyamapori (athari katika hifadhi za wanyama)
3.    Idara ya malikale kuangalia athari katika kumbukumbu na tamaduni zilizohifadhiwa (culture and archeologicals)
4.    Sekta ya mazingira  (NEMC) –tathmini ya athari za mazingira (EIA)
5.    Kituo cha uwekezaji   (TIC) – kupata leseni za biashara ,ardhi kwa ajili ya biashara na motisha kwa ajili ya biashara kwa wawekezaji kwenye miradi mikubwa Mamlaka ya bandari (TPA) – tahadhari ya mwingiliano wa maeneo na usalama wa maji
6.     Idara ya ardhi –  upatikanaji wa hati miliki za ardhi
7.    Serikali za mitaa – upatikanaji wa eneo pamoja na sheria ndogo zilizopo.
8.    Mamlaka ya maji – kibali cha kutumia maji.
9.    Idara ya masoko - kupata taarifa za masoko
10. Taasisi za utafiti – kupata taarifa zilizofanyiwa tafiti husika
3.0 Taratibu za kupata vibali na leseni za mazao yatokanayo na viumbe wanaokuzwa kwenye maji
Vibali na leseni zote za mazao yatokanayo na viumbe wanaokuzwa kwenye maji zinatolewa na Mkurugenzi wa Idara ya Ukuzaji Viumbe kwenye Maji, chini ya Sheria ya uvuvi Na. 22 ya mwaka 2003 na Kanuni za uvuvi za mwaka 2009; kama ifuatavyo:-
• Leseni za biashara ya kuuza mazao yatokanayo na viumbe wanaokuzwa kwenye maji. Utolewaji wa leseni hizi umegawanywa katika sehemu kuu mbili (2)
Sehemu ya kwanza
  1. Leseni zinazotolewa na Serikali za Mitaa (Local Government). Leseni hizo ni kama ifuatavyo.-
  2. Leseni za biashara ya kuuza mazao yatokanayo na viumbe wanaokuzwa kwenye maji ndani ya nchi,
Sehemu ya Pili
 Leseni zinazotolewa na Serikali Kuu (Central Government licence). Leseni hizo ni:
  1. leseni za kusafirisha nje ya nchi mazao yatokanayo na viumbe wanaokuzwa kwenye maji
  2.  Leseni za kuingiza nchini mazao yatokanayo na viumbe wanaokuzwa  kwenye maji (kutoka nchi za nje) ikiwa ni mpango na vibali vitatu vya:
(i)   Kusafirisha nje ya nchi samaki hai kama; Kaa, Kamba koche, Samaki wa mapambo, Mwani na mazao mengine ya viumbe wakuzwao kwenye maji
(ii)  Kuingiza samaki hai ambao hawana asili ya Tanzania kama ; Blue gill sun fin (Catollioperca marcothira), "Chinese carps" na jamii nyingine
(iii) Kuingiza nchini samaki au mazao yatokanayo na ukuzaji viumbe kwenye maji (Aquaculture products)
·         Pia wizara hutoa Leseni maalum kwa ajili ya usafirishaji wa mazao ya Ukuzaji viumbe kwenye maji kwa muda maalum kwa sababu za:
1.    Utafiti
2.    Matumizi ya nyumbani (chini ya kilo 7) na
3.     Mafunzo

Mahitaji muhimu kwa raia wa Tanzania;-                                                         
1.    Barua ya utambulisho kutoka kwa Afisa ukuzaji viumbe kwenye maji Wilaya au Manispaa,
2.    Leseni hai ya kukusanya mazao yatokanayo na viumbe wanaokuzwa kwenye maji iliyotolewa na Wilaya au Manispaa
3.    Formu ya maombi ya leseni ya biashara ya mazao yatokanayo na viumbe wanaokuzwa kwenye maji
4.     Leseni ya Biashara inayotolewa chini ya Sheria ya kutoa leseni za Biashara (Business Licensing Act),
5.    Namba ya utambulisho ya kulipa kodi (Tax Identification Number)
6.    Uthibitisho wa uraia (hati ya kusafiria au cheti cha kuzaliwa au kitambulisho cha utaifa ) wa mmiliki/wamiliki wa kampuni,
7.    Cheti cha kuandikishwa kilichotolewa kwenye kumbukumbu (Certificate of Registration and Extract from Register), or
8.     Hati ya makubaliano na hati ya ubia (Memorandum of Understanding and Articles of Associations), na
9.     Cheti cha ushiriki (Certificate of Incorporation)


Nyaraka zinazohitajika katika kupata leseni kwa asiye raia ni pamoja na;-
  1. Barua ya utambulisho kutoka kwa Afisa Uvuvi/ Ukuzaji viumbe kwenye maji wa Wilaya au Manispaa,
  2.  Uthibitisho wa uraia (cheti eha kuzaliwa au hati ya kusafiria "passport"),
  3. Kibali halali cha kufanya kazi nchini (valid work permit) 
  4. Fomu ya maombi ya leseni ya biashara ya mazao yatonayo na ukuzaji viumbe kwenye maji,
  5. Leseni hai ya Biashara inayotolewa chini ya Sheria ya kutoa leseni za Biashara (Business Licensing Act),

Wizara inazidi kuwakumbusha wadau wote wa sekta ya uvuvi kuwa kwa mujibu wa Sheria ya uvuvi Na. 22 ya mwaka 2003 na Kanuni zake za mwaka 2009 "leseni zote zinafikia ukomo wake kila tarehe 31 Disemba ya kila mwaka na kuhuwishwa kwa hiyari kufikia tarehe 30 Machi ya mwaka unaofuata zaidi ya hapo mteja atalazimika kulipa faini ya asilimia  50 (50%) ya gharama za leseni husika.
Kumbuka yapo Maelezo ya nyongeza kwa muombaji/ waombaji ambao sio raia wa Tanzania,
• Andiko la Mradi na uwezekano wa mradi kutekelezwa (Project write up & feasibility study)  Taarifa ya tathmini ya athari za Mazingira (EIA report).
* Cheti kutoka taasisi ya uwekezaji Tanzania (TIC certificate).
* Taarifa ya tathimini ya athari za kimazingira (environment impact assessment report),
* Kibali halali cha kufanya kazi nchini (Valid work permit)  na,
* Uhakiki wa mazingira yanayoendana na shughuli za uvuvi (A proof on the value of physical environment relevant to fisheries activities).


Hatua za kufuata unapotaka  kuanza ufugaji  wa samaki (Small scale Aquaculture establishment)
Maombi hufanyika kwa kujaza fomu  5 na 7 (First schedule) na kibali kitatolewa kwa fomu QA/APP/01 (First schedule)
Hatua za kufuata unapotaka kuanza ufugaji mkubwa wa samaki (Large scale aqua farmers)
Hatua ya kwanza ni lazima mwekezaji aombe kibali cha kufanya hivyo kwa kujaza Fomu 7 (First schedule) na baada ya ofisi kuridhika, kibali kitatolewa kwa form QA/APP/13 (First schedule)
Mfugaji  samaki ataomba ushauri wa kitaalam katika kuchagua eneo linalofaa kwa shughuli za ukuzaji viumbe kwenye maji kwa kuzingatia kanuni za ufugaji samaki na miongozo yake.
Taarifa ya tathimini ya athari za kimazingira (EIA) itafanyika kwa uwekezaji mkubwa kwa kuhusisha taasisi za serikali zilizopewa mamlaka ya kusimamia shughuli hizo kisheria.
Mwekezaji haruhusiwi  kutumia vichochezi kama beta agonists kwa ajili ya kuongeza ukuzaji samaki.
Mfugaji wa samaki awe na kibali cha matumizi ya maji kutoka mamlaka ya maji husika
Mfugaji awe na hati ya kumiliki ardhi

Hatua za kufuata kwa kufuga samaki kwenye Vizimba (Cage culture)
Mwekezaji apeleke maombi kwa Katibu Mkuu,
Maombi yafanyike kwa kujaza Form 7 (First schedule) kibali kitatolewa kwa QA/APP/14 baada ya kufanya tathmini ya athari za mazingira na taarifa kutolewa.
(EIA ifanyike)         



Uwekezaji wa Mwani (Seaweed)
Mwekezaji katika kilimo cha mwani anatakiwa:
  1. Apate kibali toka serikali za mitaa/Kijiji
  2. Atafute eneo linalofaa
  3. Atumie mbegu ambazo hazijaathirika na magonjwa
  4. Afuate mwongozo wa kuendeleza kilimo cha mwani

FOMU ZINAZOTUMIKA KATIKA SHUGHULI ZA UKUZAJI VIUMBE KWENYE MAJI
Application for a license for fishing or dealing in fish or fishery products
(fin fish, crustaceans, seaweed, Aquarium fish etc) - Form 3(a)
Application for export license for fish and fish products - Form 3(c)
Application for permit to construct / renovate /adapt a fish establishment – Form 5
Application for certificate of transportation of fish and fish products - Form 6
Application for permit to establish of commercial/large scale aqua farm - Form 7
Register of aqua famers – Form 8
Evident of poisoned fish Form – 9
Compounding offence Form – 11
Seizure Form – 12
Application for disposal of fishery products Form – 13(a)  


LICENCE /PERMIT / CERTIFICATE

QA/APP/01 – Certificate of approval for fish or aquaculture establishment
QA/APP/02 – Health certificate
QA/APP/03 – Sanitary certificate covering  fish and fishery products
QA/APP/04 – Permit for movement of fish and fishery products
QA/APP/05 – Permit for export of fish and fishery products
QA/APP/07 – Certificate of ownership for fish and fishery products
QA/APP/11 – License for fishing or dealing in fish and fishery products
QA/APP/12 – Permit for import of fish and fishery products
QA/APP/13 – Permit for large scale aqua farming 

Dkt.  C.G Mahika
 DAQ





Maoni 4 :

  1. Naomba kupata form za kuombea kibali cha kuuza kaa nje ya Nchi

    JibuFuta
  2. Je kuna liseni na vibali va kusafirisha pembe za ng'ombe zilizo chini ya ton moja

    JibuFuta
  3. Je kuna liseni na vibali va kusafirisha pembe za ng'ombe zilizo chini ya ton moja

    JibuFuta
  4. Je ni gharama ipii kwenye kupata lesen ya kusafrishaa dagaa kutoka Mwanza to Arusha

    JibuFuta