Nav bar

Jumatatu, 25 Januari 2016

MKUTANO WA TATHMINI NA UBORESHAJI WA MAKUSANYO YA MADUHULI YALIYO CHINI YA WIZARA MKOANI MWANZA TAREHE 25/01/2016


Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Mifugo na Uvuvi Dkt. Yohana Budeba anayeshughulikia Sekta ya  uvuvi akifungua mkutano wa tathmini na uboreshaji wa makusanyo ya maduhuli yaliyo chini ya Wizara Mkoani Mwanza kushoto ni Katibu Mkuu Sekta ya Mifugo Dkt. Maria Mashingo akifatiwa na Bi. Anunciata Njombe Mkurugenzi wa Usimamizi na Uendeshaji wa Masoko kulia ni Bi. Ng'anisa Mhasibu Mkuu wa Wizara 

 Dkt. Kayuni kutoka Idara ya Huduma za Mifugo akitoa mada juu ya udhibibti wa magonjwa ya mifugo kwa washiriki wa mkutano huo.

Bw. Leonard Basil kutoka Idara ya Uzalishaji na Masoko akitoa mada juu ya  usimamizi na uendeshaji wa Masoko ya Mifugo  kwa washiriki wa mkutano huo 

Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali watu Bi. Tabu Chando akiwasilisha mada juu ya haki na wajibu  wa watumishi wa umma katika utekelezaji wa majukumu yao


 Bw. Shilago Masele kutoka Kitengo cha Mhasibu Mkuu wa Wizara akitoa mada juu ya ukusanyaji wa maduhuli ya serikali kwa mujibu wa sheria za fedha


Bw. Majaliwa Mwesigwa kutoka Kitengo cha Teknolojia Habari na Mawasiliano akitoa mada juu ya ukusanyaji wa maduhuli kwa njia ya kisasa ya Kielectroniki


Mkaguzi wa Mkuu wa ndani wa Wizara Bw. Costantino Nyilawila akitoa mada juu ya mambo yanayojitokeza kwenye ukaguzi wa shughuli za ukusanyaji wa maduhuli serikalini

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni