Nav bar

Jumatano, 27 Januari 2016

SAMAKI WALIOHARIBIKA KUTOKA KAMPUNI YA SUNRISE FOOD COMPANY KILO 1853 WAHARIBIWA KATIKA DAMPO LA PUGU KINYAMWEZI TRH 26/01/2016

Konteina  lililohifadhi samaki walioharibika likifunguliwa kwa ajili ya kupakiza samaki na kuwapeka Dampo kwa ajili ya kuharibiwa.






Samaki wakipimwa  kutoka kwenye konteina tayari kwa kupakiwa kwenye trekta kuelekea Pugu kinyamwezi Dampo

Wa kwanza kutoka kushoto ni Afisa Uvuvi Manispaa ya Kinondoni Bw.Sijali Juma, katika ni Bi. jovice mkuchu na anaefata ni Bw.John komakoma wakaguzi wa Samaki kutoka Wizarani wakiangalia kwa makini samaki wakipimwa.






Samaki wakishushwa kwenye Trekta katika  Dampo la Pugu kinyamwezi tayari kwa kuharibiwa



Afisa Uvuvi  Manispaa ya kinondoni,Jovice Mkuchu na Afisa kutoka Sunrise Food Company wakijadiliana jambo wakati wa kuharibu Samaki hao katika Dampo la Pugu Kinyamwezi.



Samaki hao wakisagwasagwa katika dampo la Pugu Kinyamwezi



Jumanne, 26 Januari 2016

YAMAMOTO PRIZE WINNER BY JAPAN INTERNATIONAL FISHERIES RESEARCH SOCIETY (JIFRS) JULY, 2012


 A Certificate of JIFRS (Japan International Fisheries Research) YAMAMOTO PRIZE Award was given to Ms. Lilian Ibengwe at IIFET 2012 Dar Es Salaam Conference. Recognition for “Outstanding work in the Development of Strategies for Responsible Fishery Management in Tanzania”, UNU-FTP Research Project, Titled “Reducing Post-Harvest Losses of the Artisanal Dagaa (Rastrineobola Argentea) Fishery in Lake Victoria Tanzania: A Cost and Benefit Analysis”.




Jumatatu, 25 Januari 2016

MKUTANO WA TATHMINI NA UBORESHAJI WA MAKUSANYO YA MADUHULI YALIYO CHINI YA WIZARA MKOANI MWANZA TAREHE 25/01/2016


Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Mifugo na Uvuvi Dkt. Yohana Budeba anayeshughulikia Sekta ya  uvuvi akifungua mkutano wa tathmini na uboreshaji wa makusanyo ya maduhuli yaliyo chini ya Wizara Mkoani Mwanza kushoto ni Katibu Mkuu Sekta ya Mifugo Dkt. Maria Mashingo akifatiwa na Bi. Anunciata Njombe Mkurugenzi wa Usimamizi na Uendeshaji wa Masoko kulia ni Bi. Ng'anisa Mhasibu Mkuu wa Wizara 

 Dkt. Kayuni kutoka Idara ya Huduma za Mifugo akitoa mada juu ya udhibibti wa magonjwa ya mifugo kwa washiriki wa mkutano huo.

Bw. Leonard Basil kutoka Idara ya Uzalishaji na Masoko akitoa mada juu ya  usimamizi na uendeshaji wa Masoko ya Mifugo  kwa washiriki wa mkutano huo 

Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali watu Bi. Tabu Chando akiwasilisha mada juu ya haki na wajibu  wa watumishi wa umma katika utekelezaji wa majukumu yao


 Bw. Shilago Masele kutoka Kitengo cha Mhasibu Mkuu wa Wizara akitoa mada juu ya ukusanyaji wa maduhuli ya serikali kwa mujibu wa sheria za fedha


Bw. Majaliwa Mwesigwa kutoka Kitengo cha Teknolojia Habari na Mawasiliano akitoa mada juu ya ukusanyaji wa maduhuli kwa njia ya kisasa ya Kielectroniki


Mkaguzi wa Mkuu wa ndani wa Wizara Bw. Costantino Nyilawila akitoa mada juu ya mambo yanayojitokeza kwenye ukaguzi wa shughuli za ukusanyaji wa maduhuli serikalini

MKUU WA KITENGO CHA TEHAMA BW. BAKARI MAIGE KUSTAAFU KAZI TAREHE 29/01/2016


Mkuu wa kitengo cha Tehama Bakari Maige wa tatu kutoka kulia akiwa katika picha ya pamoja na wakurugenzi wengine wa wizara ya Kilimo,Mifugo na Uvuvi 
Mkuu wa kitengo cha Tehama Bakari Maige katika ubora wake



Jumatatu, 18 Januari 2016

NAIBU WAZIRI WA KILIMO MIFUGO NA UVUVI ATEMBELEA KIJIJI CHA ZUGIMLOLE WILAYA YA URAMBO NA KALIUWA TAREHE 15/01/2016

Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo Mifugo na Uvuvi Mhe.William Tate Ole Nasha akiwa katika ofisi ya Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua na aliyesimama ni Katibu Tawala wa Wilaya akitoa maelezo. 

Wanakijiji wakisaliomiana na Naibu Waziri Mhe.William Tate Ole Nasha katika kijiji cha Zugimlole Wilaya ya Kaliuwa

Naibu Waziri Mhe.William Tate Ole Nasha akizungumza na wanakijij kuhusu suala la ukataji wa miti ovyo kunapoteza uoto wa asili

Bw. Hamisi Kasere mwanakiji wa Zugimlole akieleza kero yake kutaka kuongezewa eneo kwasababu ya uwingi wa watu kwa sasa

Mkulima wa kijiji cha Zugimlole Bw. Amos Kasanga akitoa kero zake kwa Mhe Naibu Waziri juu ya mbolea ya ruzuku

Bi. Chiku Kapufi Mwanakijiji akizungumzia swala la mbolea ziwe zinafika kwa wakati


MHE NAIBU WAZIRI KATIKA ZIARA YAKE ALIPOTEMBELEA WILAYA YA MLELE NA KIJIJI CHA MWANKULU TAREHE 12 - 13/01/2016

Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo Mifugo Uvuvi Mhe.William Tate Ole Nasha akisaini kitabu cha Wageni katika ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Mlele.

Mkuu wa Wilaya ya Mlele Bw. Issa Suleiman akisoma taarifa fupi kwa Naibu Waziri Mhe. William Tate Ole Nasha 

Wanakijiji wakisikiliza kwa makini maelezo kutoka kwa Naibu Waziri Mhe. William Tate Ole Nasha

Naibu Waziri Mhe.William Tate Ole Nasha akitoa fursa kwa Wanakijiji kueleza kero zao bila hofu yoyote

Bw. Eleman Katala Mkulima Wilaya ya Mlele akieleza kero yake kuhusu malipo ya dola hawana utaalamu huo 

moja kati ya njia ya kuelekea kijiji cha Mlele ambapo daraja limekatika na wananchi wanapata tabu ya kuvuka kutokana na kasi kubwa ya maji

Bw. Innko Afisa Kilimo wa Mkoa akijitambulisha kwa Wananchi wa Kijiji cha Mwankulu Wilaya ya Mpanda
Naibu Waziri Mhe.William Tate Ole Nasha akizungumza na wanakijij na kuwaahidi kushughulikia migogoro sugu ya Wafugaji na Wakulima na kero mbalimbali hasa Vyama vya Ushirika

Bw. Nasonga ligima mwanakijiji wa Mwankulu akiomba kijiji kipatiwe  bwana shamba wa kuweza kuwasaidia katika shughuli zao za kilimo

Mkulima Bi. Yunis Moses akitoa ushauri kwa Watendaji juu ya upatikanaji wa mbegu bora pamoja na mbolea ya ruzuku  kwa wakati.