Nav bar

Ijumaa, 20 Novemba 2015

MAONESHO YA UVUVI YALIYOFANYIKA KITAIFA MKOA WA TANGA TAREHE 19/11/2015 KATIKA VIWANJA VYA TANGAMANO

Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi Dkt. Yohana Budeba akiwasili katika viwanja vya tangamano kwa ajili ya ufunguzi rasmi wa maonesho ya uvuvi

Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi Dkt. Yohana Budeba akisaini kitabu cha wageni alipowasili katika viwanja hivyo

Mkuu wa Wilaya ya Pangani Bi. Regina Njonjo akisaini kitabu cha wageni

Bi. Merisiana Sebastian Afisa Uvuvi Mkuu akimuelezea Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi Dkt. Yohana Budeba sera ya uvuvi

Bw. Fredric Francis Afisa uvuvi I akimuelezea Katibu Mkuu Dkt. Yohana Budeba kuhusu sera za ufugaji wa samaki

Bw. Omari Mohamed Afisa Mfawidhi akimuelezea Katibu Mkuu Dkt. Yohana Budeba kuhusu masuala ya ukuzaji na uzalishaji wa vifaranga vya samaki na viumbe maji

Bw. Ramadhani  Mwiga mdau kutoka Feri Dar akimuelezea Katibu Mkuu  Dkt. Yohana Budeba mazao yanayovunwa kutoka Baharini

Majongoo bahari (Sea cucumber) na Mwani (sea weed) katika ubora wake

Mdau akimuonesha mmoja wa  washiriki zao la mwani baada ya kuvunwa

Katibu Mkuu Dkt. Yohana Budeba akiangalia dagaa waliokaushwa na jua

Katibu Mkuu akiangalia samaki mbalimbali wanaofugwa kama vile kambale, sato na sangara

Patroba Matiku kutoka TAFIRI akimuonesha Katibu Mkuu Mashine aina ya CTD inayotumika kupima kina cha maji (Depth), kiwango cha jotoridi la maji na kiwango cha chumvi kwenye maji

Picha ya samaki aina ya SILIKANTi anayepatikana Kigombe Tanga

Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi Dkt. Yohana Budeba kushoto kwake ni  Dkt Herbert Lyimo Mkurugenzi wa Utafiri na Ugani akifatiwa na Bi. Mboni Ngaza Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Tanga kulia kwake Bi. Regina Njonjo Mkuu wa Wilaa ya Pangani wakiwa kwenye maandalizi ya ufunguzi

Vikundi vya ngoma kutoka Tanga

Bi Regina Njonjo Mkuu wa Wilaya ya Pangani akimkaribisha mgeni rasmi

Katibu Mkuu Dkt. Yohana Budeba akitoa hotuba kwa Wananchi waliohudhuria kwenye siku ya Mvuvi

Mpemba Asili asilia kutoka pemba akighani shairi  kwa ajili ya kuhamasisha na kuelimisha juu utunzaji wa rasilimali za uvuvi katika siku ya Mvuvi

Watoto wa shule wakiburudika na nyimbo mbalimbali


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni