Mpendwa Msikilizaji wa vipindi vya redio vya Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi Wizara inaomba radhi kwa vipindi vyake kutowepo hewani kwa kipindi cha mwaka mmoja, hii imetokana na sababu zilizo nje ya Wizara.
Aidha Kitengo cha Mawasiliano Serikalini kinakualika tena katika kuperuzi vipindi vya redio vya mwaka 2014/2015 ambavyo vitaanza kurushwa mapema mwezi Desemba. Hata hivyo vipindi vya redio vyote ambavyo viliwekwa hapo awali vinarejeshwa ili uendeelee kujielimisha kwa mafundisho mbalimbali.
Pia vipindi vya Miaka 50 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar vitajumuishwa ndani ya Blog ili kukupa uhondo na kukuhabarisha Mpenzi Msikilizaji na Mdau wa Sekta za Mifugo na Uvuvi KARIBU
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni