Nav bar

Ijumaa, 27 Mei 2011

MAKABIDHIANO YA BOTI ZA MRADI WA MACEMP CHUO CHA UVUVI MBEGANI

Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi Mhe. Dkt David Mathayo David pamoja na meza kuu wakimsikiliza Mkurugenzi wa Maendeleo wa Halmashauri ya Mkuranga akitoa neno la shukurani baada ya kumkabidhiwa Boti. Hayupo pichani)
Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhe. akimkaribisha Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi Mhe. Dkt David Mathayo David  Mkoa wa Pwani wakati wa kukabidhi boti 14kwa Halmashauri za Bagamoyo, Lindi, Mkinga, Mkuranga n.......pamoja na Kitengo cha Bahari na Maeneo Tengefu (MPRU) Aprili 6 2011. 

Boti zilizotolewa na Mhe Waziri  zikifanyiwa majariio kama zinafanya kazi kwenye Bahari ya Hindi pembeni mwa Chuo cha Maendeleo ya Uvuvi Mbegani.

Hii  ni kati ya Boti 14 zilizokabidhiwa na Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi kwa Halmashauri 5 na Kitengo cha Bahari na Maeneo Tengefu (MPRU)

MAREHEMU SHAFII MWINYI -DEREVA

MAREHEMU SHAFII MWINYI ENZI YA UHAI WAKE ALIKUWA DEREVA WA NAIBU KATIBU MKUU WAKATI WA ZIARA YA WAZIRI CHUO CHA UVUVI MBEGANI KUKABIDHI BOTI ZA MRADI WA MACEMP

WAZIRI AZINDUA BODI YA VETERINARY TANZANIA

Msajili wa Baraza la Vetenari Tanzania Dkt Theresia Ponela Mlelwa akitoa maelezo kwa Waziri Mhe. Dkt David Mathayo David

Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi Mhe. Dkt David Mathayo David akitoa Hotuba ya Uzinduzi wa Baraza la Vetenary Aprili 6 2011 New Africa Hotel Dar-es-salaam

Wajumbe na waalikwa siku ya Uzinduzi wa  Baraza la Vetenary wakimsikiliza Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi hayupo kwenye picha ambao ulifanyika  New Africa Hotel.Aprili 2011

Picha ya pampja ya Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi Mh.Dkt Davidi Mathayo david alipozindua Baraza la Veterinary 2011 New Africa Hotel Dar es Salaam.
Waziri wa Maendeleo ya Mjfugo na Uvuvi Mhe. Dkt David Mathayo David akikabidhi cheti kwa Mjumbe aliyemaliza muda wake Aprili 6 2011 
Mhe. Waziri akimkabidhi cheti cha kumaliza muda wa ujumbe katika picha  kama   mjumbe wa Bodi ya Vetenerinary Tanzania 
 

Dkt Masuruli akitoa maelezo ya Bango lililopo kwenye picha kwa Waziri Dkt David Mathayo David siku ya uzinduzi wa Baraza la Vetenary April 6 2011


Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi Mhe. Dkt David Mathayo David akitoa Hotuba ya Uzinduzi wa Baraza la Vetenary Aprili 6 2011 New Africa Hotel Dar-es-salaam

Alhamisi, 26 Mei 2011

ZARA YA WAZIRI CHUO CHA MIFUGO TENGERU I

Mhe Waziri akiliangalia Trekta linalotumiwa na Chuo cha Mifugo Tengeru, ambalo lina umri wa miaka 46 na bado linafanya kazi bila matatizo yoyote . Pembeni mwa tractor ni Mwalimu David Maleshi wa LITI Tengeru akitoa maelezo kuhusu Tractor hilo.
Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi Dkt David Mathayo David akimsikiliza Mmiliki wa Kiwanda cha Ngozi cha Himo Tanneries Bw Uiso alipotembelea kiwanda hicho tarehe 24/03/2011 na wa kwanza kushoto kwa waziri ni Mkuu wa Wilaya ya Moshi Mhe Musa Samizi.
Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi Mhe. Dkt David Mathayo David akiwa katika picha ya pamoja na uongozi wa Chuo cha Mifugo Tengeru.

Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi Mhe. Dkt David Mathayo David  akisalimiana na Uongozi wa Chuo cha Mifugo Tengeru (LITI - Tengeru) tarehe 28/03/2011 alipotembelea Chuo hicho.
Mwalimu wa vifaa na mashine zinazotumika kwa kilimo  David Maleshi akielezea jambo kuhusu vifaa na mashine hizo kwa Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi Mhe. Dkt David Mathayo David.  

ZIARA YA WAZIRI KIWANDA CHA NGOZI HIMO - TANNERIES MOSHI

Mmiliki wa Kiwanda cha ngozi cha Himo Bw Uiso akitoa maelezo kwa kuonyesha mashine zinzzotumika katika usindikaji wa ngozi, pembeni yake ni Waziri Mhe. Dkt David Mathayo David.
Mhe Waziri alipoingia eneo la ushonaji wa bidhaa za ngozi katika kiwanda cha ngozi Himo.Kwenye picha ni mmoja wa washonaji bidhaa za ngozi akionyesha kazi zake kwa Waziri.


Bw Uiso (kulia kwa waziri)  akionyesha ngozi liliyosindikwa na kuongezwa dhamani kwa Mhe. Waziri Dkt David Mathayo David (katikati) na Mkuu wa Wilaya ya Moshi Mhe Mussa Samizi.

Sehemu ya ushonaji bidhaa za ngozi katika kiwanda cha Himo.
Mhe. Waziri akionyeshwa mfumo wa Maji taka katika Kiwanda cha Himo Tanneries.

Jumatano, 25 Mei 2011

WAZIRI ATEMBELE MACHINJIO YA NYAMA YA MJI MDOGO WA HIMO - MOSHI

WAZIRI WA MAENDELEO YA MIFUGO NA UVUVI MHE. DKT DAVID MATHAYO DAVID AKIMUULIZA MASWALI YA KIUTENDAJI MSIMAMIZI WA MACHIJIO YA HIMO MWENYE KOTI JEUPE

 Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi Mhe. Dkt David Mathayo David akiongea na Mkaguzi wa nyama Mkuu wa Machinjio ya Kisasa  ya Mji Mdogo wa Himo. 

WAZIRI ATEMBELEA MCHINJIO YA MJI MDOGO WA HIMO - MOSHI

Mhe. Waziri akitoa maelekezo kwa Mkaguzi Mkuu wa Machinjio ya Himo 

Jumapili, 22 Mei 2011

ZIARA YA WAZIRI WA MAENDELEO YA MIFUGO NA UVUVI NAIC USA-RIVER ARUSHA

 DKT MOLLEL KATIKA PICHA ,MTAALAMU WA KUTOA MBEGU AKIONYESHA CHOMBO MAALUM KINACHOTUMIKA KUKINGA MBEGU ZA MADUME BORA TAYARI KWA KUPELEKWA MAABARA KWA UCHUNGUZI NA KUHIFADHIWA KWENYE MITUNGI KWA AJILI YA KUHAMILISHA.

PICHA NI MADUME BORA YANAYOTUMIKA KUZALISHA MBEGU BORA ZA KUHIMILISHIA NG'OMBA MAJIKE  YAPO  USA RIVER NJE KIDOGO YA MJI WA ARUSHA
MTAALAMU WA KUTOA MBEGU KWENYE MADUME BORA AKIKINGA MBEGU HIZO KWENYE CHOMBO MAALUM KWA KUTUMIA UTAALAM WA DUME LINGINEAMBAPO, DUME ANAYETOLEWA MBEGU HUDHANI NI JIKE LA NGOMBE HIVYO HUPANDA NA MTAALAM ANAKINGA KABLA HAJAMFIKIA YULE DUME MWINGINE.
MTAALAMU WA MAABARA YA KUHIFADHI MBEGU BORA ZA MADUME BIBI MARY SHIO  AKITOA MAELEZO KWA WAZIRI WA MAENDELEO YA MIFUGO NA UVUVI  MHE DKT DAVID MATHAYO DAVIDALIPOTEMBELEA KITUO HICHO

DKT MOLLEL NA BIBI MARY SHIO WANAONEKANA KATIKA PICHA  DKT MOLLEL ANAFUNGUA MFUNIKO WA KIMIMINIKA CHA HEWA BARIDI YA NITROJENI ILI KUMUONYESHA WAZIRI HAYUPO PICHANI

MKUU WA KITUO CHAMADUME BORA YA  UZALISHAJI MBEGU  ZA NG'OMBE DKT CHARLES MAKUNDI AKITOA MAELEZO KWA WAZIRI WA MAENDELEO YA MIFUGO NA UVUVI MHE. DKT DAVID MATHAYO DAVID ALIPOTEMBELEA KITUO HICHO
WAZIRI WA MAENDELEO YA MIFUGO NA UVUVI MHE. DKT DAVID MATHAYO DAVID AKIPATA MAELEZO KUTOKA KWA DKT CHARLES MAKUNDI MKUU WA KITUO CHA UZALISHAJI MBEGU BORA ZA MADUME CHA NAIC ARUSHA

WAZIRI ZIARA BWAWA LA NYUMBA YA MUNGU- WILAYA YA MWANGA

Mhe. Dkt David Mathayo David akichoma nyavu ambazo ni haramu za makokoro, ambazo huharibu mazingira ya mazalia ya samaki na kuvua samaki wachanga na hata mayai ya samaki.

 
WAZIRI WA MAENDELEO YA MIFUGO NA UVUVI AKIONGEA NA MWENYEKITI WA KIJIJI CHA  NYUMBA YA MUNGU MWANGA KUHUSU TUHUMA ANAZOTUHUMIWA NA WANAKIJIJI KUHUSIKA NA UVUVI HARAMU

Baadhi ya mitwimbwi ambayo wavuvi wa Bwawa la Nyumba ya Mungu huitumia katika shughuli zao za uvuvi.