Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Septemba, 2024

WIZARA YA MIFUGO NA UVUVI YATOA ELIMU YA KICHAA CHA MBWA KWA WANANCHI

Picha
Na.  Martha Mbena Wizara ya Mifugo na Uvuvi imetaoa elimu kwa wananchi juu ya kichaa cha Mbwa Wilayani Misungwi Mkoani Mwanza ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya siku ya kichaa cha mbwa duniani ambayo yanatarajiwa kufanyika Septemba 28.2024. Akiongea na wakazi wa kitongoji cha Ng'walo gwa magole kata ya Bulemeji Wilayani hapo Leo (27.09.2024) Mkurugenzi Msaidizi wa afya ya jamii ya Veterinari kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi Dkt. Stanford Ndibalema amewataka wananchi kuzingatia chanjo ya kichaa cha Mbwa ili kuepusha madhara yanayoweza kutokea. "Huu ugonjwa unaweza kuzuilika iwapo tutaamua kuwachanja Mbwa wetu, hivyo kila mmoja wetu anaemiliki Mbwa anapaswa kumlinda Mbwa huyo dhidi ya ugonjwa huu", Amesema Dkt. Ndibalema. Aidha, Dkt. Ndibalema amesisitiza umuhimu wa kuwaona wataalam wa Mifugo kwa ajili ya chanjo badala ya kusubiri chanjo ya bure inayotolewa na Serikali  Baadhi ya wazazi na wanafunzi waliofikiwa Na elimu ya kichaa cha Mmbwa wanasema  elimu  imewasaidia k...

SERIKALI KUFANYA UTARATIBU WA KUWEZESHA UPATIKANAJI WA CHANJO ZA KICHAA CHA MBWA ZA KUTOSHA NCHINI

Picha
Na. Martha Mbena Serikali kwa kushirikiana na mashirika ya Kimataifa tayari imeanza kufanya utaratibu wa kuwezesha upatikanaji wa chanjo za kutosha ili Mbwa na paka wengi wapate Chanjo dhidi ya kichaa Cha Mbwa. Hayo yamesemwa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi anayeshughulikia sekta ya Mifugo  Ndug. Abdul Mhinte alipokuwa anafunga kilele Cha maadhimisho ya siku ya Kichaa Cha Mbwa Duniani yaliyofanyika Kitaifa Katika Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi Mkoani Mwanza Septemba 28.2024. Mhinte amesema katika jitihada za kutokomeza ugonjwa huo Serikali inaratibu upatikanaji wa chanjo za kutosha kwa ajili ya kuchanja Mbwa na paka ambapo kwa kuchanja zaidi ya idadi ya 70% ya Mbwa na Paka kwa miaka mitano mfululizo tunaweza kutokomeza kabisa ugonjwa huo Nchini. "Pamoja na hatari kubwa ya ugonjwa huu, ni kwamba unaweza kuzuilika kwa asilimia mia Moja na tunaweza kutokomeza iwapo tutaweza kuwachanja Mbwa na Paka wetu na kuwatunza vizuri", amesema Mhinte.   Aidha, Septe...

MNYETI AGAWA MADUME BORA YA NG’OMBE 40 KWA WAFUGAJI SERENGETI NA BUNDA

Picha
Na. Stanley Brayton Naibu Waziri wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Mhe. Alexander Mnyeti amekabidhi madume bora 20 ya ng’ombe wa nyama kwa vikundi vya wafugaji wa kijiji cha Nyichoka Wilayani Serengeti na madume Bora 20 kwa vikundi vya wafugaji wa kijiji cha Mariwanda Wilayani Bunda, ili iwasaidie kuzalisha kizazi chenye uwezo wa kutoa nyama nyingi zaidi ya wale wa asili waliopo hapa nchini.  Akikabidhi, madume hayo Bora ya Ng'ombe kwa vikundi vya wafugaji katika hafla fupi zilizofanyika leo Septemba 27, 2024 Wilayani Serengeti na Bunda mkoani Mara, Naibu Waziri wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Mhe. Mnyeti amesema kuanzia mwaka wa fedha 2022/2023 Wizara ya Mifugo na Uvuvi imekuwa ikitekeleza mpango wake wa kuleta mabadiliko katika Sekta ya Mifugo, ambapo mpango huo umegusa nyanja mbalimbali za uzalishaji wa mifugo ili kuhakikisha ukuaji wa uhakika wa uzalishaji wa mifugo na mazao yake ili kukidhi ongezeko la soko la ndani na nje ya nchi. “mpango huu unahusisha kuboresha mbari za mifugo, u...

PROF. SHEMDOE ASHIRIKI UVUNAJI SAMAKI MRADI WA KISOKO

Picha
Na. Stanley Brayton Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Prof. Riziki Shemdoe, ameshiriki shughuli za uvunaji wa samaki aina ya Sato katika Vizimba vilivyopo eneo la Kisoko ili kushuhudia  hali ya Samaki hao ikiwemo ukubwa wake na shughuli za uuzaji wa Samaki hao ulivyofanyika katika eneo hilo. Akizungumza, leo Septemba 25, 2024 mkoani Mwanza alipotembelea eneo hilo la Mradi wa Ukuzaji Samaki kwa njia ya Vizimba, Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Prof. Shemdoe amesema samaki hawa walikuwa wadogo sana, ila leo hii wanavunwa wakiwa wakubwa kiasi cha kwamba wanafaa kuingia sokoni na kuliwa. "hii mbegu ya samaki ilikuwa ndogo sana na haishikiki, ila leo hii tunavuna ikiwa kitu ambacho tunakiona hapa kwa mara ya kwanza, na hii yote ni Shukrani kwa Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuona umuhimu wa kutoa fedha ili ziweze kutumiwa na Vijana hawa wa Jenga Kesho Iliyo Bora - BBT katika uzalishaji huu wa bidhaa za uvuvi" amesema Pro...

TANGA YAJIPANGA KUONGEZA UZALISHAJI WA SAMAKI

Picha
Na Edward Kondela Mkoa wa Tanga unajikita kuongeza kiwango cha uzalishaji wa samaki na mazao mengine ya baharini, ili kuzinufaisha jamii zake kupitia shughuli hizo zinazohusiana na Uchumi wa Buluu. Mkuu wa Mkoa huo, Mhe Balozi Dkt. Batilda Burian, ameyasema hayo (18.09.2024) kwenye mkutano ulioandaliwa na Wizara ya Mifugo na Uvuvi, kwa ajili ya kujadili masuala ya uhifadhi wa bahari kwa vizazi na maendeleo ya sekta hiyo Mkoani Tanga. Amesema uvuvi ni moja ya sekta muhimu mkoani humo, hususan kwenye wilaya za Tanga, Pangani, Mkinga na Muheza ambapo takwimu zinaonesha kuwepo jumla ya wavuvi 13,336 na vyombo vya uvuvi vilivyosajiliwa 1,922.  Mhe Balozi Dkt. Burian ametoa mfano kuwa, mwaka 2023/2024 samaki waliouzwa mkoani humo walikuwa na thamani ya Shilingi Bilioni 47.208, zilizowezesha ukusanyaji ushuru uliofikia takriban Shilingi Milioni 951.7 huku wakulima wa mwani wakifikia 5,300. Ameongeza kuwa uzalishaji wa zao hilo la baharini umefikia tani 3,000 kwa thamani ya takribani Shili...

RASILIMALI ZA BAHARI ZATAJWA KUWA ONGEZEKO PATO LA TAIFA

Picha
Na. Edward Kondela Katibu Tawala Mkoa wa Dar es Salaam Dkt. Toba Nguvila amesema Sekta ya Uvuvi ikisimamiwa vyema kupitia rasilimali za Bahari ya Hindi, sekta hiyo itaweza kuimarisha pato la taifa kupitia kupitia mnyororo wa thamani. Dkt. Nguvila amesema hayo leo (19.09.2024) jijini Dar es Salaam wakati akimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Bw. Albert Chalamila, kwenye ufunguzi wa mkutano uliohusisha kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa pamoja na viongozi wa wilaya za Ilala, Kigamboni, Temeke na Kinondoni zenye maeneo yenye bahari. Amesema kuwa mnyoyoro huo wa thamani unaohusisha wadau wa Sekta ya Uvuvi wakiwemo wavuvi wenyewe, kwenye masoko na wachakataji wa mazao ya uvuvi utakuwa na tija kwa kuhakikisha ulinzi wa rasilimali za uvuvi unazingatiwa ili kupata fedha nyingi kupitia biashara ya mazao hayo. “Samaki wanaovuliwa wakiwa wadogo kwenye soko hawaingii hivyo hauwezi kupata hesabu yao kwenye pato la taifa, hii inamaanisha ni uvuvi haramu lakini tukilinda rasimali za uvuvi vyem...

WATAALAMU KUANDAA MFUMO WA UFUATILIAJI WA TAARIFA ZA MASOKO YA MIFUGO

Picha
Na. Stanley Brayton - WMUV Wataalamu Wizara ya Mifugo na Uvuvi wamekutana kwa ajili ya kujadili Mifumo inayopendekezwa katika kuanzisha Kitengo cha Ufuatiliaji wa Taarifa za Masoko ya Mifugo na Mazao yake ikiwa ni njia mojawapo ya kuwasaidia wafugaji na wafanyabiashara wa mifugo kujua nini kinatokea katika masoko, pamoja na kuisaidia serikali kufanya maamuzi kuhusiana na masoko ya mifugo. Akizungumza, leo Septemba 04, 2024, mkoani Morogoro katika kikao cha kujadili Mifumo inayopendekezwa katika kuanzisha Kitengo cha Ufuatiliaji wa Taarifa za Masoko ya Mifugo na Mazao yake, Mkurugenzi Msaidizi Mazao ya Mifugo, Usalama wa Chakula na Lishe, Dkt. Nyamizi Bundala, amesema mafunzo haya yana lengo la kujengeana uwezo kuhusu taarifa za masoko ya mifugo na mazao yake ikiwemo, upatikanaji, uchakataji na uwasilishawaji wa taarifa hizo sambamba na uanzishwaji wa dawati/kitengo mahususi kitakacho shughulikia taarifa za masoko ya mifugo na mazao yake. "Mafunzo haya yamekuja wakati muafaka na ya...