Sehemu ya Wavuvi na
Wafanyabiashara wa mazao ya samaki wa soko la Kilumba wakimsikiliza Waziri wa
Mifugo na Uvuvi, Mhe. Abdallah Ulega (hayupo pichani) alipowatembelea
kuzungumza nao Januari 29, 2024 kuhusu ujio wa Mhe. Rais na hafla ya Ugawaji
Boti na Vizimba kwa Wavuvi wa Ziwa Viktoria tukio litakalofanyika katika uwanja
wa Nyamagana, jijini Mwanza Januari 30, 2024. Mgeni rasmi wa tukio hilo ni Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Waziri wa Mifugo na Uvuvi,
Mhe. Abdallah Ulega akiongea na Wakina mama ambao ni Wafanyabiashara wa samaki
wa Kamanga Feri alipowatembelea kuzungumza nao leo Januari 29, 2024 kuhusu ujio
wa Mhe. Rais na hafla ya Ugawaji Boti na Vizimba kwa Wavuvi wa Ziwa Viktoria
tukio litakalofanyika katika uwanja wa Nyamagana, jijini Mwanza Januari 30,
2024. Mgeni rasmi wa tukio hilo ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Pichani ni sehemu ya
Vizimba vinavyotarajiwa kugawiwa kwa wavuvi wa Ziwa Victoria.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni