Watumishi wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi, wakifurahia kombe la kupata Ushindi wa pili kwa Upande Taasisi za Utafiti ambapo Taasisi ya TAFIRI (Tanzania Fisheries Research Institute) iliyokuwa chini ya Wizara imepata Ushindi huo,,kwenye kilele cha maonesho ya sikukuu ya wakulima (Nanenane) Kanda ya ziwa Magharibi jijini Mwanza, tarehe 08.08.2023.
Muonekano wa Kombe la Ushindi wa pili kwa upande wa Taasisi za Utafiti lililotolewa kwa Taasisi ya Utafiti wa Mifugo Tanzania kwenye Maonyesho ya Nanenane Kanda ya Ziwa Magharibi yaliyofanyika Jijini Mwanza. (08.08.2023)
Watumishi wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi, wakifurahi kwa pamoja kupata makombe mawili ya Ushindi, Ikiwa Taasisi ya TAFIRI (Tanzania Fisheries Research Institute)imepata ushindi wa pili na Taasisi ya TALIRI (Tanzania Livestock Research Institute) imepata ushindi wa tatu, kwenye maonesho ya sikukuu ya wakulima (Nanenane) Kanda ya ziwa Magharibi jijini Mwanza, tarehe 08.08.2023.
Afisa Utafiti Mifugo, Magreth Mgani (kulia) akitoa maelezo kwa baadhi ya wananchi kuhusu huduma za chanjo za mifugo zinazotolewa na Wakala ya Maabara ya Veterinari Tanzania wakati walipotembelea Banda la Wizara ya Mifugo na Uvuvi lililopo kwenye Viwanja vya Maonesho ya Nanenane Ipuli mkoani Tabora. (08.08.2023)
Afisa Mifugo, Jonathan Mwiru (wa kwanza kushoto) akimuelezea mmoja wa wananchi kuhusu shughuli zinazofanywa na Kituo cha Mifugo Kanda ya Magharibi wakati alipotembelea Banda la Wizara ya Mifugo na Uvuvi lililopo kwenye Viwanja vya Maonesho ya Nanenane katika viwanja vya Ipuli mkoani Tabora. Anayemfuatia ni Afisa Biashara Mkuu, Yusuph Mwakatobe kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi. (08.08.2023)
Daktari Mtafiti Mifugo kutoka TVLA Kigoma, Dkt. Emmanuel Kitundu (kushoto) akiwaelezea baadhi ya wananchi namna mtego wa mbung’o unavyofanya kazi wakati walipotembelea Banda la Wizara ya Mifugo na Uvuvi lililopo kwenye Viwanja vya Maonesho ya Nanenane vya Ipuli mkoani Tabora. (08.08.2023)
Wataalam kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi (kulia)wakiendelea kutoa elimu juu ya shughuli zinazofanywa na Wizara hiyo kwenye siku ya Kilele cha Maonesho ya Nanenane Kanda ya Magharibu katika Viwanja vya Ipuli mkoani Tabora. (08.08.2023)
Viongozi kutoka Taasisi za Wizara ya Mifugo na Uvuvi na Taasisi nyingine wakiwa wameketi kwenye Jukwaa Kuu wakati wa kuhitimisha Maonesho ya Nanenane Kanda ya Magharibi yaliyofanyika kwenye Viwanja vya Ipuli mkoani Tabora. Wa kwanza kulia ni Afisa Mfawidhi Bodi ya Nyama Kanda ya Magharibi, Joseph Kulwa akifuatiwa na Daktari wa Mifugo ZVC, Dkt. Adelina Mkumbukwa. (08.08.2023)
Afisa Mfawidhi Bodi ya Nyama Kanda ya Magharibi, Joseph Kulwa akitoa salam za Wizara ya Mifugo na Uvuvi wakati wa kilele cha Maonesho ya Nanenane Kanda ya Magharibi yaliyofanyika kwenye Viwanja vya Ipuli mkoani Tabora. (08.08.2023)
Afisa Mfawidhi Bodi ya Nyama Kanda ya Magharibi, Joseph Kulwa (kulia) akipokea Cheti na Kombe la Ushindi wa Pili kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Mhe. CGF(Rtd). Thobias Andengenye ambapo Wizara ya Mifugo na Uvuvi imepata baada ya kushiriki kikamilifu kwenye Maonesho ya Nanenane Kanda ya Magharibi yaliyofanyika kwenye Viwanja vya Ipuli mkoani Tabora. (08.08.2023)
Watumishi wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi wakiwa kwenye picha ya pamoja huku wakiwa wameshikilia Cheti cha Ushiriki, Cheti cha Ushindi wa Pili na Kikombe cha Ushindi wa Pili mara baada ya kuhitimishwa kwa Maonesho ya Nanenane Kanda ya Magharibi yaliyofanyika kwenye Viwanja vya Ipuli mkoani Tabora. (08.08.2023)
Hili ndilo Kombe la Mshindi wa Pili walilopata Wizara ya Mifugo na Uvuvi katika Maonesho ya Nanenane Kanda ya Magharibi yaliyofanyika kwenye viwanja vya Ipuli mkoani Tabora. (08.08.2023)
Mkufunzi kutoka Wakala ya Vyuo vya Mafunzo ya Mifugo Tanzania (LITA) Dkt. Samwel Ngulwa (kushoto) akieleza huduma zinazotolewa na LITA ikiwa ni pamoja na elimu, kwa wadau waliotembelea banda la Wizara ya Mifugo na Uvuvi wakati wa maonesho ya kimataifa ya Wakulima Nanenane kwenye viwanja vya Themi jijini Arusha Agosti 08, 2023.
Mteknolojia wa chakula kutoka Bodi ya Maziwa Tanzania kanda ya Kaskazini (TDB), Bi. Christerbel Swai (kushoto) akitoa elimu ya umuhimu wa unywaji wa maziwa kwa wadau waliotembelea banda la Wizara ya Mifugo na Uvuvi wakati wa maonesho ya kimataifa ya Wakulima Nanenane kwenye viwanja vya Themi jijini Arusha Agosti 08,2023.
Afisa Mifugo kutoka kituo cha Taifa cha Uhimisha NAIC, Bi. Patricia Ngoda akitoa elimu ya uhimilishaji na mbegu bora za mifugo kwa wadau waliotembelea banda la Wizara ya Mifugo na Uvuvi wakati wa maonesho ya kimataifa ya Wakulima Nanenane kwenye viwanja vya Themi jijini Arusha Agosti 08,2023.
Msaidizi Utafiti kutoka Taasisi ya Utafiti wa Mifuto Tanzania (TALIRI) ,Bw. Jackson Godfrey akitoa elimu ya aina mbalimbali za malisho na mbegu na umuhimu wa kustawisha malisho kwa wadau waliotembelea banda la Wizara ya Mifugo na Uvuvi wakati wa maonesho ya kimataifa ya Wakulima Nanenane kwenye viwanja vya Themi jijini Arusha Agosti 08,2023
Afisa Mauzo kutoka kampuni ya HUSAM Butchery Equipment, Bw. Husein Rashid (kushoto) akitoa elimu ya umuhimu wa vifaa vya kukatia nyama kwenye mabucha na majumbani kwa wadau waliotembelea banda la Wizara ya Mifugo na Uvuvi wakati wa maonesho ya kimataifa ya Wakulima Nanenane yanayofanyika kwenye viwanja vya Themi jijini Arusha Agosti 08,2023
Afisa Mfawidhi kutoka Kituo cha Uchunguzi wa Magonjwa ya Mifugo kanda ya kaskazini (ZVC), Dkt. Raphael Mwampashi (kushoto) akitoa elimu juu ya magonjwa mbalimbali ya mifugo kwa wadau waliotembelea banda la Wizara ya Mifugo na Uvuvi wakati wa maonesho ya kimataifa ya Wakulima Nanenane kwenye viwanja vya Themi jijini Arusha, Agosti 08,2023
Kaimu Meneja wa Wakala ya Maabara ya Veterinari Tanzania (TVLA) Dkt. Lowenya Mushi (kushoto) akitoa elimu ya chanjo zinazotolewa na Wakala hiyo kwa wadau waliotembelea banda la Wizara ya Mifugo na Uvuvi wakati wa maonesho ya kimataifa ya Wakulima Nanenane kwenye viwanja vya Themi jijini Arusha Agosti 08,2023.
Timu ya Wataalam kutoka Wakala ya Mafunzo ya Mifugo nchini (LITA) kampasi ya Morogoro na wataalam wengine wa Wizara wakifurahia ushindi wa nafasi ya pili ambao taasisi hiyo imeupata kwa upande wa Wakala na Taasisi za Mafunzo wakati wa kilele cha Maadhimisho ya Sikukuu ya Wakulima, Wafugaji na Wavuvi (NaneNane) kanda ya Mashariki mkoani Morogoro Agosti 08,2023.
Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Utafiti wa Mifugo Tanzania (TALIRI) Prof. Erick Komba akisaini kitabu cha wageni alipotembelea banda la Wakala ya Maabara ya Veterinari Tanzania (TVLA) lililopo ndani ya mabanda ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi kujifunza kazi mbalimbali za kimaabara zinazofanywa na wakala kwenye maonesho ya Kimataifa ya Nanenane katika uwanja wa John Mwakangale Mkoa wa Mbeya Agosti 8, 2023.
Meneja wa Maabara Kuu ya Veterinari wa Wakala ya Maabarala ya Veterinari Tanzania (TVLA) Dkt. Geofrey Omarch (kushoto) akitoa maelezo kwa Mkurugenzi wa utawala (Mifugo) Dkt. Charles Mhina (wa tatu kulia) kuhusiana na huduma za kimaabara za kiveterinari zinazotolewa na wakala alipotembelea banda la TVLA Katika viwanja vya Nane Nane Morogoro Agosti 6, 2023.
Mtaalamu wa Maabara wa Wakala ya Maabara ya Veterinari Tanzania-TVLA wa kituo cha Mtwara bwana Salimu Mveyange (kulia) akitoa elimu kwa wadau wa Mifugo walipotembelea banda la TVLA lililopo ndani ya Mabanda ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi kujifunza shughuli mbalimbali za Kimaabara zinazotolewa na Wakala kwenye maonesho ya Nanenane uwanja wa Ngongo Lindi Agosti 8, 2023.
Katibu Mkuu Wizara Mifugo na Uvuvi Prof. Riziki Shemdoe Agosti 09, 2023 amekutana na kufanyamazungumzo na Uongozi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Bodi ya Maziwa Tanzania pamoja na wadau wa kiwanda cha Maziwa cha mkoani Njombe kwa ajili yakutafuta mustakabali wa maendeleo ya kiwanda hicho ilikiweze kuendelea kuzalisha maziwa ambapo kwenye kikao hicho wajumbe kwa pamoja wamekubaliana kuweka kando tofauti zao zilizokuwa zinakwamisha maendeleo ya kiwanda hicho
Mkufunzi na Mteknolojia wa samaki, Bi. Shilya Sonda (wapili kulia), kutoka Wakala wa Elimu na Mafunzo ya Uvuvi (FETA-Nyegezi) akimuonesha mdau aliyetembelea banda la Wizara ya Mifugo na Uvuvi, bidhaa zilizotengenezwa kwa samaki (Fish boll na Fish Samosa) ili mdau huyo aweze kununua na kupata radha ya samaki, kwenye kilele cha maonesho ya sikukuu ya wakulima (Nanenane) Kanda ya ziwa Magharibi jijini Mwanza, tarehe 08.08.2023.
Wadau wa sekta ya Mifugo waliotembelea banda la Wizara ya Mifugo na Uvuvi, wakimsikiliza kwa makini Mtaalamu wa Uhimishaji Nguruwe, kutoka MR PIG Tanzania, Dkt. Baguma Egbert, aliyekuwa akiwapa elimu ya uhimishaji Nguruwe na namna watakavyoweza kupata faida kupitia ufugaji Nguruwe, kwenye kilele cha Maonesho ya sikukuu ya wakulima (Nanenane) Kanda ya ziwa Magharibi jijini Mwanza, tarehe 08.08.2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega (Mb) katika kiwanja cha ndege cha Songwe kilichopo Mkoani Mbeya, wakati alipowasili kwa ajili ya kilele cha Sikukuu ya Kimataifa ya Wakulima (Nanenane) hapo kesho katika viwanja vya John Mwakangale. (07.08.2023)
Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega (Mb) akibadilishana mawazo na Mhe. William Lukuvi ambaye ni mmoja washauri wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika masuala ya Siasa na Uhusiano wa Jamii, wakati wakisubiri kuwasili kwa Mhe. Rais katika kiwanja cha ndege cha Songwe kilichopo Mkoani Mbeya kwa ajili ya kilele cha Sikukuu ya Kimataifa ya Wakulima (Nanenane) hapo kesho katika viwanja vya John Mwakangale. (07.08.2023)
Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega (Mb) akibadilishana mawazo na Waziri wa Kilimo Mhe. Hussein Bashe walipowasili katika kiwanja cha ndege cha Songwe kilichopo Mkoani Mbeya kwa ajili ya kumpokea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa ajili ya kilele cha Sikukuu ya Kimataifa ya Wakulima (Nanenane) hapo kesho katika viwanja vya John Mwakangale. (07.08.2023)

Waziri Mkuu Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Mizengo Peter Pinda akipata maelezo kutoka kwa Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Maabara ya Veterinari Tanzania Dkt. Stella Bitanyi kuhusiana na kazi mbalimbali za kimaabara zinazofanywa na Wakala hasa katika utoaji wa huduma za uchunguzi wa Magonjwa ya Wanyama, Uzalishaji wa Chanjo za Mifugo, utafiti wa magonjwa ya Wanyama, uhakiki wa ubora wa vyakula vya mifugo, Usajili na uhakiki wa ubora wa viuatililu wa dawa za mifugo pamoja na mafunzo kwa wahitimu wa ngazi mbalimbali za elimu alipotembelea banda la TVLA kwenye maonesho ya Kimataifa ya Nanenane yanayoendelea katika uwanja wa John Mwakangale Mkoa wa Mbeya Agosti 7, 2023.
Meneja wa shamba la Mabuki, Bi. Lini Mwala akitoa elimu kwa wadau kuhusu faida za Mitamba inayotolewa kwenye shamba hilo, kupitia chombo cha Televishen cha Channel ten (Channel 10) kwenye maonesho ya sikukuu ya wakulima (Nanenane) Kanda ya ziwa Magharibi jijini Mwanza, tarehe 07.08.2023.
Afisa Mfawidhi wa kituo cha ukuzaji viumbe maji Nyengedi Lindi Bw.Robert Nicolaus wa pili toka kushoto akitoa maelezo ya ufugaji wa samaki katika mabwawa kwa Mkuu wa Wilaya ya Nanyumbo Bi Mariam Chaurembo wa tatu kutoka kushoto (mwenye Hijab)ambapo alielezwa kuwa idadi ya vifaranga vya samaki katika Bwawa inategemeana na ukubwa wa bwawa mfano bwawa hili lina ukubwa mita 5x10 vifaranga watakao wekwa katika bwawa ni150.Chakula cha vifaranga ni jambo muhimu katika ufugaji wa samaki katika Mabwawa kifaranga anakula kulingana na uzito wake kati ya asilimia 5 hadi kumi ya uzito wake.(07.08.2023)
Mkunfunzi ufugaji viumbe maji kutoka FETA kampasi ya Mtwara Mikindani Bi. Salma Chatto (kulia) akitoa maelezo ya fursa zilizopo kwa watanzania kwenye biashara ya samaki wa mapambo kwa Mkuu wa wilaya ya Nanyumbu Bi. mariyam Chaurembo wa (tatu) kutoka kushoto, Katika banda la maenesho ya Nanenane Kanda ya kusini, Viwanja vya Ngongo Mkoani Lindi ( 7/08/2023.)

Jennifer Simbua Mhifadhi Maendeleo ya Jamii katika Hifadhi ya Bahari ya Ghuba ya Mnazi na Maingilio ya Mto Ruvuma (kushoto) akimueleza Mh. Mkuu wa Wilaya ya Nanyumbu Bi Mariam Chaurembo mwenye (Hijab kulia) aliyetembelea banda la maonesho ya nanenane kanda ya kusini viwanja vya Ngongo Lindi, juu ya samaki aina ya silikanti ambaye alitoweka kabisa katika uso wa dunia takribani miaka milioni 66 iliyopita. Silikanti ni Miongoni mwa samaki ambao wanatakiwa kufanyiwa utafiti wa kina ili kuweza kujua sababu za kutoweka kwake na kurejea tena miaka ya hivi karibuni. Aidha, Mhifadhi alimfahamisha Mh. Mkuu wa wilaya juu ya msimu wa Nyangumi ambao umeanza mwezi wa 7 na utadumu hadi Mwezi Novemba na hivyo kumualika atembelee Hifadhi kujionea Nyangumi.(07.08.2023).

Mkuu wa Wilaya ya Nanyumbo Bi Mariam Chaurembo mwenye Hijab akiongea na wataala wa Mifugo na Uvuvi mara tu baada ya kumaliza kutembelea mabanda ya maonesho ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi ambapo ameitaka kutacuta jawabu la Mifugo inayotoka maeneo mengine ya nchi kuingia Kanda ya Kusini ambapo kumekuwa na ugomvi ya kusini mwa nch8omvi kati ya wahamiaji na wenyeji. (07.08.2023)
Afisa Mfawidhi Bodi ya Nyama Kanda ya Magharibi, Joseph Kulwa (wa pili kulia) akimueleza Katibu Tawala Mkoa wa Kigoma, Ndg. Albert Msovela kuhusu kazi zinazofanywa na Wizara ya Mifugo na Uvuvi wakati alipotembelea Banda la Wizara hiyo lililopo kwenye Maonesho ya Nanenane katika viwanja vya Ipuli mkoani Tabora. (07.08.2023)
Meneja wa Wakala ya Maabara ya Veterinari Kanda ya Magharibi, Dkt. Qwari Bura (kulia) akimueleza Katibu Tawala Mkoa wa Kigoma, Ndg. Albert Msovela (kushoto) kuhusu shughuli zinazofanywa na Taasisi hiyo wakati alipotembelea Banda la Wizara ya Mifugo na Uvuvi lililopo kwenye Viwanja vya Nanenane Ipuli mkoani Tabora. (07.08.2023)
Katibu Tawala Mkoa wa Kigoma, Ndg. Albert Msovela (kushoto) akimuuliza swali Daktari wa Mifugo kutoka TVLA, Dkt. Denice Luwumba mara baada ya kuonyeshwa moja ya chanjo za mifugo zinazolishwa na Wakala ya Maabara ya Veterinari Tanzania wakati alipotembelea Banda la Wizara ya Mifugo na Uvuvi lililopo kwenye Maonesho ya Nanenane katika viwanja vya Ipuli mkoani Tabora. (07.08.2023)
Afisa Mtekinolojia wa Chakula kutoka Bodi ya Nyama – Bw. Edgar Mamboi (kulia) akimueleza Katibu Tawala Mkoa wa Kigoma, Ndg. Albert Msovela (kushoto) kuhusu umuhimu wa kutumia mashine za kukatia nyama kwenye maduka ya nyama wakati alipotembelea Banda la Wizara ya Mifugo na Uvuvi lililopo kwenye Viwanja vya Nanenane Ipuli mkoani Tabora. (07.08.2023)
Mhasibu kutoka Kituo cha Kanda ya Magharibi (ZVC), Bi. Salama Hamad (kushoto) akiwaeleza baadhi ya wananchi waliotembelea Banda la Wizara ya Mifugo na Uvuvi lililopo kwenye Viwanja vya Nanenane Ipuli mkoani Tabora, kuhusu shughuli zinazofanywa na ZVC. (07.08.2023)
Watumishi wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi (kushoto) wakitoa maelezo kuhusu shughuli zinazofanywa na Wizara hiyo kwa baadhi ya wananchi walitembelea Banda ya Wizara hiyo lililopo kwenye Viwanja vya Nanenane Ipuli mkoani Tabora. (07.08.2023)
Afisa Mifugo kutoka Kituo cha Uhimilishaji - NAIC, Bi. Happy Mlima (kushoto) akitoa elimu ya uhimilishaji kwa mdau aliyetembelea banda la Wizara ya Mifugo na Uvuvi wakati wa maonesho ya kimataifa ya Wakulima Nanenane yanayoendelea kufanyika kwenye viwanja vya Themi jijini Arusha, Agosti 07,2023.
Afisa Masoko kutoka Bodi ya Maziwa nchini Bw. Hamis Kiimbi (kushoto) akimpa elimu ya usindikaji Maziwa mmoja wa wadau wa Tasnia hiyo Bw. Nnko Ebeneza aliyefika kwenye banda la Mifugo na Uvuvi lililopo kwenye Viwanja vya NaneNane Nzuguni jijini Dodoma leo Agosti 06, 2023.
Siku moja baada ya kutolewa taarifa ya uwepo wa kuku aina ya Brahama kwenye Banda la Wizara ya Mifugo na Uvuvi, watu wengi wamefika bandani hapo kwa ajili ya kushuhudia kuku hao kama wanavyoonekana pichani baadhi ya watu wakiwaangalia leo Agosti 06, 2023.
Afisa Uvuvi Mkuu kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi Bw. Nelson Mbawala (kulia) akimueleza mmoja wa wananchi waliofika kwenye Banda la Wizara hiyo lililopo Viwanja vya NaneNane Nzuguni jijini Dodoma Bw. Ngowi Tumsifu umuhimu wa lishe inayotokana na zao la Mwani leo Agosti 06, 2023.
Daktari Mtafiti Mifugo kutoka TVLA Tabora, Dkt. Denice Luwumba (kushoto) akimueleza mmoja wa wananchi waliofika kwenye Banda la Wizara hiyo lililopo Viwanja vya NaneNane Ipuli mkoani Tabora kuhusu umuhimu wa matumizi ya chanjo za mifugo (06.08.2023)
Afisa Mifugo kutoka Bodi ya Nyama – Tabora, Simon Butawantemi (kulia) akimueleza mmoja wa wananchi waliofika kwenye Banda la Wizara hiyo lililopo Viwanja vya NaneNane Ipuli mkoani Tabora Bi. Mwajuma Hamis kuhusu huduma zinazotolewa na Bodi ya Nyama Tanzania (06.08.2023)
Daktari wa Mifugo kutoka ZVC Tabora, Dkt. Kijida Polisi (kulia) akimsikiliza mmoja wa wananchi waliofika kwenye Banda la Wizara hiyo lililopo Viwanja vya NaneNane Ipuli mkoani Tabora aliyetaka kujua kuhusu huduma zinazotolewa na ZVC. (06.08.2023).
Afisa Uvuvi Msaidizi kutoka Kituo cha Ukuzaji Viumbe Maji Mwamapuli – Igunga, Wilbard Mapindo (kushoto) akiwaeleza wananchi waliofika kwenye Banda la Wizara hiyo lililopo Viwanja vya NaneNane Ipuli mkoani Tabora kuhusu ufugaji bora wa samaki. (06.08.2023)
Afisa Malisho Msaidizi kutoka Shamba la Malisho ya Mifugo la Vikuge Bw. Elieza Naftali (katikati) akimpa Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi Dkt. Charles Mhina (kulia) maelezo ya malisho yaliyopandwa kwenye banda la Wizara ya Mifugo na Uvuvi lililopo kwenye Viwanja vya Maonesho ya NaneNane mkoani Morogoro leo Agosti 06, 2023.
Mtàalam wa Maabara toka wakala ya Maabara yaVeterinari Tanzania Kanda ya Kusini (TVLA) Bi Irene Haule (kulia mwenye kofia ya bluu.)akitoa maelezo kwà Wananchi waliotembelea banda la Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwa lengo la kujifunza tekinolojia sahihi za kuzalisha mifugo bora yenye tija kwenye banda la maonesho ya nanenane Viwanja vya Ngongo Mkoani Lindi Mtaalam huyo amewaeleza wananchi hao kuwa taasisi imewez.a kufanya uchunguzi na utambuzi wa magonjwa ya Mifugo,utengenezaji na uzalishaji wa chanjo na uhakiki wa ubora wa vyakula vya mifugo.(06.08.2023)

Mkaguzi wa Maziwa kutoka Halmashauri ya Jiji la Mbeya Bi. Witnes Mwiwa (wa kwanza kulia) akiwakabidhi Maziwa yaliyosindikwa Maafisa wa Bodi ya Maziwa Tanzania (kushoto) alipotembelea banda la Bodi ya Maziwa Tanzania kwenye maonesho ya Kimataifa ya Wakulima, Wafugaji na Wavuvi (Nanenane) yanayoendelea katika viwanja vya John Mwakangale mkoani Mbeya leo Agosti 6, 2023 ambapo pamoja na mambo mengine ametoa changamoto anazokumbana nazo wakati akitekeleza majukumu yake ya ukaguzi wa maziwa.
Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Utafiti wa Mifugo Tanzania (TALIRI) Prof. Erick Komba akiweka saini katika kitabu cha wageni mara baada ya kutembelea banda la Bodi ya Maziwa Tanzania kwenye maonesho ya Kimataifa ya Wakulima, Wafugaji na Wavuvi (Nanenane) yanayoendelea katika viwanja vya John Mwakangale mkoani Mbeya leo Agosti 6, 2023 ambapo ameshauri kuendelea kuweka nguvu ya pamoja kuhakikisha kuwa Tasnia ya Maziwa inaingia kwenye mfumo rasmi.
Mteknolojia Wa Chakula kutoka Bodi ya Maziwa Tanzania Bw. Kennedy Daniel (kushoto) akitoa maelezo kwa mdau juu ya upatikanaji wa mashine inayotumika kukamulia maziwa ambayo ni moja ya vifaa vinavyopatikana kwenye kampuni ya Bajuta inayojihusisha na uuzaji wa pembejeo za mifugo alipotembelea banda la Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwenye maeonesho ya Kimataifa ya Wakulima, Wafugaji na Wavuvi yanayoendelea katika viwanja vya John Mwakangale mkoani Mbeya leo Agosti 6, 2023.
Afisa Mauzo kutoka kampuni ya HUSAM Butchery Equipment, Bw. Salim Mbarouk (kushoto) akitoa elimu ya umuhimu wa vifaa vya kukatia nyama kwenye mabucha na majumbani kwa wadau waliotembelea banda la Wizara ya Mifugo na Uvuvi wakati wa maonesho ya kimataifa ya Wakulima Nanenane yanayoendelea kufanyika kwenye viwanja vya Themi jijini Arusha Agosti 06,2023.
Mtaalamu wa nyanda za malisho kutoka Taasisi ya Utafiti wa Mifugo Tanzania (TALIRI) Bw. Makayi Ngabo (kulia) akitoa elimu ya aina za malisho na umuhimu wake kwa mifugo kwa wadau waliotembelea banda la Wizara ya Mifugo na Uvuvi wakati wa maonesho ya kimataifa ya Wakulima Nanenane yanayoendelea kufanyika kwenye viwanja vya Themi jijini Arusha Agosti 06,2023.
Afisa Mifugo kutoka Kituo cha Uhimilishaji cha Taifa (NAIC) Bi. Florida Shayo (kushoto) akitoa elimu ufugaji bora wa ng'ombe kwa wadau waliotembelea banda la Wizara ya Mifugo na Uvuvi wakati wa Maonesho ya Kimataifa ya Wakulima Nanenane yanayoendelea kufanyika jijini Arusha Agosti 06, 2023.
Wadau wa Uvuvi wakiangalia na kupata elimu ya Bwawa la kufugia samaki lisilohamishika, kutoka kwa kijana aliyepata Mafunzo ya ufugaji samaki kwenye Mabwawa kutoka Wakala wa Elimu na Mafunzo ya Uvuvi Tanzania (FETA- Kampasi ya Nyegezi) wakati wa maonesho ya sikukuu ya wakulima (Nanenane) Kanda ya ziwa Magharibi jijini Mwanza, tarehe 06.08.2023.
Kijana kutoka Wakala wa Elimu na Mafunzo ya Uvuvi Tanzania (FETA), Mr. Lameck Maendeka, anayesimamia mtambo wa kikaushia Dagaa kwa njia ya solar, ambaye alipata ujuzi huo kutoka Wakala wa Elimu ya Mafunzo ya Uvuvi (FETA - kampasi ya Nyegezi) akitoa elimu ya jinsi ya uandaaji wa wadaa waliokausha kwa njia ya Solar kwa wadau waliotembelea banda la Wizara ya Mifugo na Uvuvi, kwenye maonesho ya sikukuu ya wakulima (Nanenane) Kanda ya ziwa Magharibi jijini Mwanza, tarehe 06.08.2023.

Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Maabara ya Veterinari Tanzania-TVLA Dkt. Stella Bitanyi akitoa elimu kwa wanafunzi wa shule ya Sekondari Mpemba iliyopo Wilaya ya Tunduma mkoa wa Songwe waliotembelea banda la TVLA kujifunza kazi mbalimbali za kimaabara zinazofanywa na TVLA hususani katika utoaji wa huduma za kiuchunguzi wa Magonjwa ya Wanyama, utafiti wa magonjwa ya Wanyama pamoja na Uzalishaji wa Chanjo za wanyama kwenye maonesho ya Kimataifa ya Nanenane yanayoendelea katika uwanja wa John kwenye Mwakangale Mkoa wa Mbeya Agosti 5, 2023.
Meneja wa Wakala ya Maabara ya Veterinari Tanzania-TVLA kituo cha Sumbawanga Dkt. Rajabu Mlekwa akitoa elimu kwa wadau wa Mifugo waliotembelea banda la TVLA kujifunza matumizi sahihi ya chanjo dhidi ya Homa ya Mapafu ya Ng’ombe (BOVIVAC-CBPP) inayozalishwa na TVLA kwenye maonesho ya Kimataifa ya Nanenane yanayoendelea katika uwanja wa John kwenye Mwakangale Mkoa wa Mbeya Agosti 5, 2023.
Afisa Mifugo Mtafiti mwandamizi wa Wakala ya Maabara ya Veterinari Tanzania-TVLA Dkt. Ronald Benju akifanya uchunguzi kupitia upasuaji wa Mzoga wa kuku ulioletwa na Mfugaji ili kutambua Magonjwa yaliyo sababisha vifo vya kuku wake alipotembelea banda la TVLA lililopo kwenye maonesho Nanenane yanayoendelea katika uwanja wa Nyamhongolo uliopo Mkoa wa Mwanza Agosti 5, 2023.
Fundi Sanifu Maabara Mkuu wa Wakala ya Maabara ya Veterinari Tanzania-TVLA bwana Ally Fussah akitoa elimu kwa wadau wa mifugo waliotembelea banda la TVLA kujifunza namna ya kuwadhibiti wadudu aina ya Mbung'o wanaobeba vimelea vinavyosababisha ugonjwa wa Nagana Kwa mifugo na malale kwa binadamu kwa kutumia vitambaa vyenye dawa kwenye maonesho ya Kimataifa ya Nanenane yanayoendelea katika uwanja wa John kwenye Mwakangale Mkoa wa Mbeya Agosti 5, 2023.
Mkurugenzi wa Heifer International hapa nchini Bw. Mark Tsoxo (wa tatu kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Watumishi wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi pamoja na wadau walio katika mnyororo wa thamani wa maziwa alipowatembelea kwenye maonesho ya Kimataifa ya Wakulima, wafugaji na Wavuvi yanayoendelea katika viwanja vya John Mwakangale mkoani Mbeya leo Agosti 5, 2023.
Mkurugenzi wa Heifer International nchini Bw. Mark Tsoxo (katikati) akiwa na Maafisa wa Bodi ya Maziwa Tanzania leo Agosti 5, 2023 ametembelea banda la Bodi ya Maziwa kwenye maonesho ya Wakulima, Wafugaji na Wavuvi (Nanenane) katika viwanja vya John Mwakangale Mkoani Mbeya na kuahidi kushirikiana na Bodi hiyo bega kwa bega katika kuimarisha Tasnia ya Maziwa hapa nchini.
Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya Bodi ya Maziwa Tanzania Prof. Zackaria Masanyiwa akifuatilia maelezo toka kwa Mteknolojia wa Chakula toka Bodi ya Maziwa Tanzania Bw. Israel Mwingira namna bodi hiyo inavyokumbana na changamoto na kuzitafutia ufumbuzi katika kutekeleza majukumu yake ya kuisimamia Tasnia ya Maziwa hapa nchini alipotembelea banda la Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwenye maonesho ya Wakulima, W afugaji na Wavuvi yanayoendelea katika viwanja vya Nzuguni kanda ya kati Dodoma leo Agosti 5, 2023.
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe David Silinde akifuatilia kwa makini maelezo ya namna ya vifaa maalumu vya kupimia maziwa vinavyotumika kutambua maziwa yasiyofaa kwa matumizi ya binadamu toka kwa Mteknolojia wa Chakula toka Bodi ya Maziwa Tanzania Bw. Israel Mwingira (wa kwanza kushoto) alipotembelea banda la Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwenye maonesho ya Wakulima, wafugaji na Wavuvi (Nanenane) yanayoendelea katika viwanja vya Nzuguni kanda ya kati Dodoma leo Agosti 5, 2023.
Mteknolojia wa Chakula toka Bodi ya Maziwa Tanzania Bw. Kennedy Daniel akimuongoza mdau wa maziwa hatua kwa hatua namna ya kujisajili kwenye mfumo wa MIMIS ili kutambulika miongoni mwa wadau walioko kwenye mnyororo wa thamani wa maziwa alipotembelea banda la bodi hiyo kwenye maonesho ya Kimataifa ya Wakulima, wafugaji na Wavuvi (Nanenane) yanayoendelea katika viwanja vya John Mwakangale mkoani Mbeya leo Agosti 5, 2023.
Mteknolojia wa Chakula toka Bodi ya Maziwa Tanzania Bw. Kennedy Daniel akionesha chombo maalumu cha kuhifadhia maziwa wananchi waliofika katika banda la bodi hiyo kwenye maonesho ya Kimataifa ya Wakulima, Wafugaji na Wavuvi yanayoendelea katika viwanja vya John Mwakangale mkoani Mbeya leo Agosti 5, 2023.
Prof. Gabriel Shirima kutoka Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia - Nelson Mandela akiongea na wafugaji walioleta mifugo pamoja na wananchi walioenda kuangalia gwaride la Mifugo wakati ufunguzi wa gwaride hilo kwenye maonesho ya kimataifa ya Wakulima Nanenane yanayoendelea kufanyika kwenye viwanja vya Themi jijini Arusha Agosti 05, 2023.
Kaimu Meneja wa Wakala ya Maabara ya Veterinari Tanzania (TVLA) Dkt.Rowenya Hamza Mushi akitoa elimu ya matumizi ya aina mbalimbali za chanjo zinazozalishwa na wakala hiyo kwa wadau waliotembelea banda la Wizara ya Mifugo na Uvuvi wakati wa maonesho ya kimataifa ya Wakulima Nanenane yanayoendelea kufanyika kwenye viwanja vya Themi jijini Arusha Agosti 05,2023.
Mkufunzi kutoka Wakala ya Vyuo vya Mafunzo ya Mifugo Tanzania (LITA) Dkt. Samwel Ngulwa (kushoto) akieleza huduma zinazotolewa na LITA ikiwa ni pamoja na elimu, kwa wadau waliotembelea banda la Wizara ya Mifugo na Uvuvi wakati wa maonesho ya kimataifa ya Wakulima Nanenane yanayoendelea kufanyika kwenye viwanja vya Themi jijini Arusha Agosti 05, 2023.
Baadhi ya Wananchi wa Mkoa wa Lindi wakiwa katika banda la Wizara ya Mifugo na Uvuvi la maonesho ya nanena kanda ya Kusini viwanja vya Ngongo Mkoani Lindi wakijifunza tekinolojia ya kutengenenza bidhaa zitokanazo na Ngozi ambazo ni pamoja na viatu bora vilivyo tengenezwa kwa Ngozi toka kiwanda cha Msophe Elinaza Shoes kilichopo jijini Dar es Salaam.(05.08.2023)
Afisa Uvuvi Mkuu Msaidizi toka Wizara ya Mifugo na Uvuvi Bi Yasinta Magesa akitoa maelezo ya tekinolojia mbalimbali za Uvuvi za kuboresha Uvuvi na kuwa wenye tija na kuongeza kipato kwa Mvuvi na kuchangia kikamilifu pato laTaifa mdau wa Uvuvi , kwa mdau wa Uvuvi wa Lindi aliyetembelea banda la maonesho ya Nanenane la Wizara ya Mifugo na Uvuvi akitoa mafunzo kwa mdau huyo ya Umuhimu wa Uchakataji wa mazao ya UVUVI na matumizi sahihi ya nyavu za Uvuvi.(05.08.2023)

Mhifadhi kutoka kituo cha Hifadhi za Bahari na Maeneo Tengefu Bw.Mustafa Issa akitoa maelezo ya Samaiki aina ya Silikanti kwa mdau aliyetembelea banda la Wizara ya Mifugo na Uvuvi Kanda ya Kusini Viwanja vya maonesho ya Nanenane Ngongo akielezwa historia ya Samaki huyo aliyetoweka na kugundulika katika Bahari ya Hindi maeneo ya Tanga ,Mtwara na Mafia zaidi ya miaka milioni 400 samaki huyo ana umuhimu wa historia , Utalii na Utafiti kugundua aina nyingine za samaki kama huyo wapo maeneo mengine katika maenwo yetu ya Uvuvi ya bahari ya Hindi.(05.08.2023)
Baadhi ya wanafunzi kutoka shule mbalimbali jijini Mbeya wamekuwa sehemu ya wanaohudhuria Maonesho ya Kimataifa ya Wakulima (Nanenane) yanayofanyika katika viwanja vya John Mwakangale ambapo leo hii wamefika katika banda la Wizara ya Mifugo na Uvuvi katika Wakala ya Elimu na Mafunzo ya Uvuvi Tanzania (FETA) ili kupata elimu ya ufugaji samaki. (05.08.2023)
Baadhi ya wanafunzi kutoka shule mbalimbali jijini Mbeya wametembelea banda la Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwa mmoja wa wadau anayejishughulisha na ufugaji wa nguruwe katika Maonesho ya Kimataifa ya Wakulima (Nanenane) yanayofanyika katika viwanja vya John Mwakangale. (05.08.2023)
Baadhi ya wananchi wakiingia na kutoka katika moja ya mabanda ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi ili kupata elimu na huduma mbalimbali wakati wa Maonesho ya Kimataifa ya Wakulima (Nanenane) yanayofanyika katika viwanja vya John Mwakangale jijini Mbeya. (05.08.2023)
Baadhi ya wananchi wakiingia na kutoka katika moja ya mabanda ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi ili kupata elimu na huduma mbalimbali wakati wa Maonesho ya Kimataifa ya Wakulima (Nanenane) yanayofanyika katika viwanja vya John Mwakangale jijini Mbeya. (05.08.2023)
Wananchi wakiwa kwa mmoja wa wadau wa ufugaji kuku ili kujifunza zaidi juu ya ufugaji bora wa kuku walipotembelea moja ya mabanda ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi ili kupata elimu na huduma mbalimbali wakati wa Maonesho ya Kimataifa ya Wakulima (Nanenane) yanayofanyika katika viwanja vya John Mwakangale jijini Mbeya. (05.08.2023).
Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega (Mb) akihojiwa na mmoja wa watangazaji wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) wakati wa kuandaa kipindi maalum juu ya Maonesho ya Kimataifa ya Wakulima (Nanenane) yanayofanyika katika viwanja vya John Mwakangale jijini Mbeya. (05.08.2023).
Mtaalamu wa Uhimilishaji wa Nguruwe Dkt. Baguma Egbert (wanne kulia) kutoka MR PIG Tanzania, akimuonyesha Mgeni rasmi Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Kagera Mhe. Isaya Tendega kifaa kinachotumika kuhimilisha Nguruwe wakati akitoa elimu juu ya uhimilishaji wa Nguruwe na faida zake katika kuboresha Mbali za Nguruwe kwenye mashamba, alipoenda kutembelea banda la Wizara ya Mifugo na Uvuvi, kwenye maonesho ya sikukuu ya wakulima (Nanenane) yenye kauli mbiu " Vijana na wanawake ni msingi Imara wa Mifumo endelevu ya Chakula" ambayo yanaendelea katika Viwanja vya Nyamuhongoro vilivyopo Jijini, Mwanza, tarehe 05.08.2023.

Afisa Mtafiti Mifugo Mwandamizi Dkt. Ronald Benju kutoka Wakala ya Maabara ya Veterinari Tanzania (TVLA) akitoa elimu ya chanjo ya Mgonjwa mbalimbali ya wanyama na kuelezea faida ya chanjo hizo kwa Mgeni rasmi Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Kagera, Mhe. Isaya Tendega,alipoenda kutembelea banda la Wizara ya Mifugo na Uvuvi, kwenye maonesho ya sikukuu ya wakulima (Nanenane) Kanda ya ziwa Magharibi, jijini Mwanza, tarehe 05.08.2023.
Pichani ni moja ya vivutio vikubwa kwenye banda la Wizara ya Mifugo na Uvuvi hapa Nzuguni jijini Dodoma ambao ni kuku aina ya Brahama wenye asili ya Saudi Arabia na kwa pamoja wanauzwa shilingi milioni 1. Ni kuku wa pili kwa ukubwa Ulimwenguni ambao hufikia mpaka uzito wa kilo 7, Ni kuku wa mapambo na biashara na ni rahisi kufuga kwa sababu hufugwa kwa njia za asili kama kuku wengine. Kuku Jike anaanza kutaga mayai akiwa na umri wa miezi 6 na hutaga mayai yasiyopungua 20. Huweza kuishi mazingira yoyote.
Watumishi wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi(waliovaa sare) wakitoa elimu juu ya huduma wanazozitoa katika sekta ya Mifugo kwa wadau waliotembelea banda la Wizara hiyo kwenye maonesho ya sikukuu ya wakulima (Nanenane) yenye kauli mbiu "Vijana na wanawake ni msingi Imara wa Mifumo endelevu ya Chakula" katika Viwanja vya Nyamuhongoro vilivyopo Kanda ya ziwa Magharibi, jijini Mwanza, tarehe 05.08.2023.
Daktari wa Wanyama kutoka Bodi ya Nyama Kanda ya ziwa, Dkt. Msomi Anthony akitoa elimu kwa wadau Kupitia Chombo cha Habari cha (Star TV,) juu ya bidhaa za nyama zenye ubora na kuhakikisha kulinda Afya ya mlaji, kwenye maonesho ya sikukuu ya wakulima (Nanenane) Kanda ya ziwa Magharibi jijini Mwanza, tarehe 05.08.2023.
Wadau wa sekta ya Mifugo wakiwa kwenye banda la Wakala wa Maabara ya Veterinari Tanzania (TVLA) kwa ajili ya kupata elimu juu ya huduma zitolewazo na Wakala hiyo, kwenye viwanja vya Nyamuhongoro vilivyopo Kanda ya ziwa Magharibi, jijini Mwanza, tarehe 05.08.2023.
Katika hatua ya kuwaandaa wafugaji na wajasiriamali wajao kwenye tasnia mbalimbali za sekta ya Mifugo Wizara ya Mifugo na Uvuvi kupitia Bodi ya Maziwa imetoa elimu kuhusu umuhimu na utunzaji wa bidhaa ya maziwa kwa wanafunzi wa Shule ya awali na msingi mchepuo wa kiingereza ya Modern ambapo pichani ni Mteknolojia wa Chakula kutoka Bodi hiyo Bw. Israel Mwingira akitoa elimu hiyo Agosti 04, 2023 kwenye Viwanja vya NaneNane Nzuguni jijini Dodoma.

Watoto wa shule ya Jacaranda primary School iliyopo Kisesa Mwanza wakipata elimu juu ya chanjo ya kichaa cha Mbwa na Magonjwa ya wanyama wafugwao nyumbani na kusisitizwa kwenda kuwaambia wazazi wao jinsi ya kutunza wanyama wa nyumbani, elimu hiyo wameipata kutoka kwa Dkt. Subira Samweli wa Kituo cha Uchunguzi wa Magonjwa ya wanyama (ZVC- Mwanza) na Dkt. Pius wa baraza la Veterinari Tanzania (RVCT-Mwanza) Bunga, wakati watoto hao walipofika katika Mabanda ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwenye sikukuu ya wakulima (Nanenane) Kanda ya Magharibi, Mwanza, tarehe 04.08.2023.
Watumishi wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi wakiwa kwenye picha ya pamoja kwenye maonesho ya sikukuu ya wakulima (Nanenane) Kanda ya ziwa Magharibi, Jijini Mwanza, tarehe 04.08.2023.
Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe Abdallah Ulega akiweka saini kwenye kitabu cha wageni mara baada ya kutembelea na kupata maelezo ya kina kutoka kwa maafisa wa Bodi ya Maziwa namna wanavyoendelea kutoa elimu kwa wananchi juu ya umuhimu wa urasimishaji wa Tasnia ya Maziwa hapa nchini kwenye maonesho ya Kimataifa ya Wakulima, Wafugaji na Wavuvi(Nanenane) yanayoendelea katika viwanja vya John Mwakangale Jijini Mbeya siku ya tarehe 04, Agosti 2023.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Uvuvi) Bi. Agness Meena akifurahia jambo na maafisa wa Bodi ya Maziwa Tanzania na kuwapongeza kwa kazi nzuri wanayoifanya ya kuendelea kuwaunganisha wadau wa maziwa hapa nchini alipotembelea banda la bodi hiyo kwenye maonesho ya Kimataifa ya Wakulima, Wafugaji na Wavuvi (Nanenane) yanayoendelea katika viwanja vya John Mwakangale jijini Mbeya siku ya tarehe 04, Agosti 2023.
Mteknolojia Chakula wa Bodi ya Maziwa Tanzania Bw. Kennedy Daniel akitoa elimu juu ya matumizi sahihi ya vipimo vinavyotumika kupimia maziwa kwa mdau aliyetembelea banda la Wizara ya Mifugo na Uvuvi katika maonesho ya Kimataifa ya Wakulima, Wafugaji na Wavuvi (Nanenane) yanayoendelea katika viwanja vya John Mwakangale Jijini Mbeya siku ya tarehe 04, Agosti 2023.
Afisa Masoko wa Bodi ya Maziwa Tanzania Bw. Said Isike akitoa elimu juu ya virutubisho muhimu vinavyopatikana kwenye maziwa kwa Wanafunzi wa shule ya sekondari Nsongwi Juu ya Jijini Mbeya walipotembelea banda la Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwenye maonesho ya Kimataifa ya Wakulima, Wafugaji na Uvuvi yanayoendelea katika Viwanja vya John Mwakangale jijini Mbeya siku ya tarehe 04, Agosti 2023.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi(Mifugo) Dkt. Daniel Mushi (Kulia) akiweka saini kwenye kitabu cha wageni na kuwataka kuendelea kutoa elimu kwa wananchi juu ya upatikanaji wa ng'ombe bora wa maziwa wanaopatikana hapa nchini ilikuweza kuongeza upatikanaji maziwa kwa wingi alipotembelea banda la Bodi ya Maziwa Tanzania kwenye maonesho ya Kimataifa ya Wakulima, Wafugaji na Wavuvi yanayoendelea katika viwanja vya John Mwakangale jijini Mbeya siku ya tarehe 4, Agosti 2023.
Meneja wa Wakala ya Maabara ya Veterinari Tanzania-TVLA kituo cha Sumbawanga Dkt. Rajabu Mlekwa akitoa elimu kwa wadau wa Mifugo waliotembelea banda la TVLA lililopo ndani ya Mabanda ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi kujifunza matumizi sahihi ya chanjo dhidi ya ugonjwa wa Kutupa Mimba (BRUCELLOSIS-S19) kwa Ng’ombe inayozalishwa na TVLA kwenye maonesho ya Kimataifa ya Nanenane uwanja wa John Mwakangale Mkoa wa Mbeya siku ya tarehe 04/08/2023.
Meneja wa Wakala ya Maabara ya Veterinari Tanzania-TVLA kituo cha Iringa Dkt. Geofrey Mbata akitoa elimu kwa wadau wa Mifugo waliotembelea banda la TVLA lililopo ndani ya Mabanda ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi kujifunza matumizi sahihi ya chanjo dhidi ya ugonjwa wa Chambavu (BLACKQUARTER) kwa Ng’ombe, Mbuzi na Kondoo inayozalishwa na TVLA kwenye maonesho ya Kimataifa ya Nanenane uwanja wa John Mwakangale Mkoa wa Mbeya siku ya tarehe 04/08/2023.
Mtaalamu wa Maabara kutoka Wakala ya Maabara ya Veterinari Tanzania-TVLA Bwana Ibrahim Halfani akitoa elimu kwa wadau wa Mifugo waliotembelea banda la TVLA lililopo ndani ya Mabanda ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi kujifunza matumizi sahihi ya chanjo dhidi ya ugonjwa wa Kimeta (ANTHRAX) kwa Ng’ombe, Mbuzi na Kondoo inayozalishwa na TVLA kwenye maonesho ya Kimataifa ya Nanenane uwanja wa John Mwakangale Mkoa wa Mbeya siku ya tarehe 04/08/2023.
Mtaalamu wa Maabara wa Wakala ya Maabara ya Veterinari Tanzania-TVLA kituo cha Iringa Bwana Anderson Yohana kitoa elimu kwa wadau wa Mifugo waliotembelea banda la TVLA lililopo ndani ya Mabanda ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi kujifunza kuhusiana na huduma za kiuchunguzi za kimaabara zinazotolewa na TVLA kwenye maonesho ya Kimataifa ya Nanenane uwanja wa John Mwakangale Mkoa wa Mbeya siku ya tarehe 04/08/2023.
Wataalamu wa Utafiti, Mifugo na Maabara wa Wakala ya Maabara ya Veterinari Tanzania-TVLA (wapo ndani ya Banda) Wakitoa elimu kwa wadau mbalimbali wa Mifugo waliotembelea banda la TVLA lililopo ndani ya Mabanda ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi kujifunza kuhusia na huduma za Kimaabara, utafiti na uzalishaji wa Chanjo za Mifugo zinazotolewa na Wakala kwenye maonesho ya Kimataifa ya Nanenane uwanja wa John Mwakangale Mkoa wa Mbeya siku ya tarehe 04/08/2023.
Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega akipata maelezo kutoka kwa Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Maabara ya Veterinari Tanzania-TVLA Dkt. Stella Bitanyi kuhusiana na huduma zinazotolewa na Wakala, alipotembelea banda la TVLA kujionea shughuli mbalimbali za utoaji wa elimu zinazofanywa na Wakala katika maonesho ya Kimataifa ya Nanenane kwenye uwanja wa John Mwakangale Mkoa wa Mbeya siku ya tarehe 03/08/2023.

Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega (katikati) akitoa maelekezo kwa Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Maabara ya Veterinari Tanzania-TVLA Dkt. Stella Bitanyi kuhusiana na namna bora ya kuboresha huduma zinazotolewa na Wakala hasa katika upatikana wa chanjo za mifugo kwa wafugaji, alipotembelea banda la TVLA kujionea shughuli mbalimbali zinazofanywa na Wakala katika maonesho ya Kimataifa ya Nanenane kwenye uwanja wa John Mwakangale Mkoa wa Mbeya siku ya tarehe 03/08/2023. Kushoto kwake ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi Prof. Riziki Shemdoe na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Mifugo) Dkt. Daniel Mushi.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi Prof. Riziki Shemdoe (katikati) akipata maelezo kutoka kwa Meneja wa Wakala ya Maabara ya Veterinari Tanzania-TVLA kituo cha Iringa Dkt. Geofrey Mbata kuhusiana huduma za kiuchunguzi za kimaabara zinazotolewa na TVLA, alipotembelea banda la TVLA kujionea shughuli mbalimbali zinazofanywa na Wakala katika maonesho ya Kimataifa ya Nanenane kwenye uwanja wa John Mwakangale Mkoa wa Mbeya siku ya tarehe 03/08/2023. Kushoto kwake ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Mifugo) Dkt. Daniel Mushi.
Afisa Mtafiti Mifugo kutoka Wakala ya Maabara ya Veterinari Tanzania-TVLA Bwana Geofrey Siwezi akitoa elimu kwa Mdau wa Mifugo alietembelea banda la TVLA kujifunza kuhusiana na matumizi sahihi ya chanjo ya Mdondo wa Kuku (TEMEVAC) zinazozalishwa na Wakala siku ya tarehe 03/08/2023 kwenye maonesho ya Kimataifa ya Nanenane kwenye uwanja wa John Mwakangale Mkoa wa Mbeya.
Mtaalamu wa Maabara kutoka Wakala ya Maabara ya Veterinari Tanzania-TVLA Bwana Abnery Mrema akitoa elimu kwa Mdau wa Mifugo alietembelea banda la TVLA kujifunza kuhusiana na matumizi sahihi ya chanjo ya Homa ya Mapafu ya Ngombe (BOVIVAC-CBPP) inayozalishwa na Wakala siku ya tarehe 03/08/2023 kwenye maonesho ya Kimataifa ya Nanenane kwenye uwanja wa John Mwakangale Mkoa wa Mbeya.
Mtaalamu wa Maabara Bw. Colman Edward kutoka Wakala ya Maabara ya Veterinari Mwanza akitoa elimu ya chanjo ya kuku aina ya I -2 ambayo ni Kinga ya mdondo/ kideri, kwa mfugaji aliyetembelea banda la wakala hiyo ambalo lipo kwenye mabanda ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi, kwenye maonesho ya sikukuu ya wakulima (Nanenane) yanayoendelea kufanyika katika Viwanja vya Nyamuhongoro vilivyopo Jijini, Mwanza, tarehe 03.08.2023.
Muuzaji wa Madawa ya Mifugo Bw. Konne Kirotet kutoka ASHISHI LIFE SCIENCE, akielezea faida ya virutubisho aina ya Calvitamin Egg ambayo inasaidia kuongeza Uzalishaji kwa kuku wa mayai na kufanya Ganda la yai kuwa gumu, ametoa maelezo hayo kwa wadau ambao wametembelea kwenye Mabanda ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi sikukuu ya wakulima (Nanenane) Kanda ya Magharibi jijini Mwanza, tarehe 03.08.2023.
Mtaalamu wa Uhimilishaji wa Nguruwe Dkt. Baguma Egbert kutoka MR PIG Tanzania, akitoa elimu juu ya uhimilishaji wa Nguruwe na faida zake katika kuboresha Mbali za Nguruwe kwenye mashamba, kwa wadau waliotembelea banda la Wizara ya Mifugo na Uvuvi, kwenye maonesho ya sikukuu ya wakulima (Nanenane) yenye kauli mbiu " Vijana na wanawake ni msingi Imara wa Mifumo endelevu ya Chakula" ambayo yanaendelea katika Viwanja vya Nyamuhongoro vilivyopo Jijini, Mwanza, tarehe 03.08.2023.

Afisa Mifugo kutoka Shamba la Uzalishaji Mifugo (L.M.U Mabuki) Bw. Richard Mrosso, akitoa maelezo kuhusu faida za nyati maji ambaye shamba hilo linazalisha nyati hao kwa ajili ya nyama, maziwa na nguvu kazi katika shughuli mbalimbali, kwa wadau waliotembelea banda la Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwenye maonesho ya sikukuu ya wakulima(Nanenane) yenye kauli mbiu " Vijana na wanawake ni msingi Imara wa Mifumo endelevu ya Chakula" katika Viwanja vya Nyamuhongoro vilivyopo Kanda ya ziwa Magharibi jijini Mwanza, tarehe 03.08.2023.
Mtaalamu wa Uendelezaji nyanda za malisho kutoka Taasisi ya Utafiti wa Mifugo Tanzania (TALIRI) kanda ya Kaskazini, Bw. Jackson Godfrey (katikati) akielezea aina za malisho na umuhimu wake kwa mifugo kwa wadau waliotembelea banda la Wizara ya Mifugo na Uvuvi wakati wa maonesho ya kitaifa ya Wakulima nanenane yanayoendelea kufanyika kwenye viwanja vya Themi jijini Arusha Agosti 3, 2023.
Fundi Sanifu Maabara Mwandamizi kutoka Wakala ya Maabara ya Veterinari Tanzania (TVLA) kanda ya Kaskazini, Bi. Sikujua Magobo (kushoto) akitoa elimu ya matumizi sahihi ya chanjo na aina za chanjo zinazozalizwa kwenye maabara hiyo kwa mdau Bi. Rehema Husein (kulia) alipotembelea banda la Wizara ya Mifugo na Uvuvi wakati wa maonesho ya Kimataifa ya Wakulima Nanenane yanayoendelea kufanyika kwenye viwanja vya Themi jijini Arusha Agosti 3, 2023.
Wanafunzi wa Shule ya Msingi Modern ya Jijini Dodoma wakipata elimu ya namna bora ya kupima maziwa kwa kutumia vifaa vya kitaalamu kutoka kwa Mteknolojia Chakula wa Bodi ya Maziwa Tanzania Bw. Israel Mwingira walipotembelea banda la Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwenye Maonesho ya Wakulima, Wafugaji na Wavuvi(Nanenane) katika viwanja vya Nzuguni Kanda ya Kati Dodoma siku ya tarehe 03, Agosti, 2023.
Mteknolojia Wa Chakula toka Bodi ya Maziwa Tanzania Bw. Kennedy Daniel akimuonesha mwananchi vifaa maalumu vya kuhifadhia na kupima maziwa na kumuelezea umuhimu wakupima maziwa kabla yakusindika alipotembelea banda la Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwenye maonesho ya Kimataifa ya Wakulima, wafugaji na wavuvi (Nanenane) yanayoendelea katika viwanja vya John Mwakangale jijini Mbeya siku ya tarehe 03, Agosti, 2023
Muonekano wa Mabanda ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwenye sikukuu ya wakulima (Nanenane) Kanda ya Ziwa Magharibi, Mwanza. Tarehe 03.08.2023.
Afisa Mafunzo ya Ufugaji Samaki kutoka Bw. Louis Ottaru kutoka Wakala wa Elimu na Mafunzo ya Uvuvi ( FETA- kampasi ya Nyegezi.) akiwaelezea na kuwaonesha bwawa la kufugia samaki linalohamishika (Collapsible pond) wadau waliotembelea banda la Mifugo na Uvuvi kwenye Maonesho ya Sikukuu ya Wakulima (Nanenane) yenye kaulimbiu "Vijana na wanawake ni Msingi Imara wa Mifumo endelevu ya Chakula" Kanda ya ziwa Magharibi jijini Mwanza, tarehe 02.08.2023.
Mhamasishaji wa ufugaji samaki bw. Moabu Msukwa (wapili kulia) kutoka Wakala wa Elimu na Mafunzo ya Uvuvi (FETA- Kampasi ya Nyegezi) akitoa maelezo kuhusu mfumo wa kufuga samaki kwa kutumia maji yanayozunguka (Rerciculating aquaculture System) na namna mfumo huo unavyofanya kazi kwa wadau waliotembelea banda la Wizara ya mifugo na uvuvi kwenye maonesho ya wakulima (Nanenane) Kanda ya ziwa Magharibi, Mwanza, tarehe 02.08.2023.Afisa Uvuvi Bw. Elinsa Masawe (katikati) kutoka Idara ya Ukuzaji Viumbe Maji Kanda ya ziwa, Mwanza akitoa maelezo ya ufugaji samaki kwenye vizimba na mabwawa pamoja na ulishaji wa vyakula vya aina tofauti kwa samaki kulingana na hatua za ukuaji kwa wadau waliotembelea banda la Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwenye maonesho ya sikukuu ya wakulima yenye kauli mbiu "Vijana na wanawake ni msingi Imara wa Mifumo endelevu ya Chakula" ( Nanenane) Kanda ya ziwa Magharibi jijini Mwanza, tarehe 02.08.2023.Mtaalam wa Mifugo kutoka kampuni ya LANDLAKES Bi. Brenda Ngailo (kushoto) akitoa elimu kwa mdau aliyetembelea banda la Wizara ya Mifugo na Uvuvi juu ya namna ya kufuga na kutunza ng'ombe wa maziwa pamoja na chakula cha kuwalisha kwenye maonesho na Kitaifa ya Wakulima nanenane yanayoendelea kufanyika kwenye viwanja vya Themi jijini Arusha Agosti 02, 2023.Mtaalamu wa Mifugo kutoka kampuni ya Interchick Bw. Daniel Kamyori (kulia) akitoa elimu ya namna ya kutotolesha na kufuga vifaranga vya kuku kwa wadau waliotembelea banda la Wizara ya Mifugo na Uvuvi wakati wa maonesho ya Kimataifa ya Wakulima nanenane yanayoendelea kufanyika kwenye viwanja vya Themi jijini Arusha , Agosti 02, 2023Afisa Mifugo kutoka Kituo cha Uhimilishaji cha Taifa (NAIC) Bi. Florida Shayo (kushoto) akitoa elimu ufugaji bora wa ng'ombe kwa Bi. Neema Maeda alipotembelea kwenye banda la Wizara ya Mifugo na Uvuvi wakati wa Maonesho ya Kimataifa ya Wakulima Nanenane yanayoendelea kufanyika kwenye viwanja vya Themi jijini Arusha Agosti 02,2023.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni