Nav bar

Alhamisi, 24 Agosti 2023

DKT. MPANGO AFUNGUA MAONESHO YA KIMATAIFA YA WAKULIMA 2023 KWENY VIWANJA VYA JOHN MWAKANGALE JIJINI MBEYA

 

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akikata utepe kuashiria kufungua rasmi Maonesho ya Kimataifa ya Wakulima 2023 (Nanenane) yanayofanyika katika viwanja vya John Mwakangale jijini Mbeya. Wa kwanza kushoto ni Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. David Silinde. (01.08.2023)

Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. David Silinde akimweleza Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango namna wizara hiyo ilivyojipanga kuwainua kiuchumi vijana ambao wapo kwenye mpango wa “Building a Better Tomorrow (BBT)” kupitia vituo atamizi katika sekta za mifugo na uvuvi kwa kuwapatia mikopo ili kujiendeleza kiuchumi baada ya kupata mafunzo ya vitendo. Makamu wa Rais Mhe. Dkt. Mpango amepatiwa taarifa hiyo baada ya kufika katika banda la BBT lililo chini ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi ili kupata taarifa zaidi juu ya mpango huo. (01.08.2023)

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akipata maelezo ya namna ya kuzalisha chakula bora cha samaki kwa bei nafuu kutoka kwa mmoja wa wanafunzi kwa njia ya vitendo kupitia vituo atamizi baada ya Mhe. Dkt. Mpango kufika katika banda la “Building a Better Tomorrow (BBT)” lililo chini ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi katika Maonesho ya Kimataifa ya Wakulima 2023 (Nanenane) yanayofanyika katika viwanja vya John Mwakangale Jijini Mbeya. (01.08.2023)

Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. David Silinde akipata maelezo kutoka kwa baadhi ya wakurugenzi wa wizara na wakuu wa taasisi na wanafunzi wa vituo atamizi vya sekta za mifugo na uvuvi ili kufahamu namna walivyojiandaa kwenye Maonesho ya Kimataifa ya Wakulima 2023 (Nanenane) yanayofanyika katika viwanja vya John Mwakangale jijini Mbeya. (01.08.2023)

Muonekano wa banda la “Building a Better Tomorrow (BBT)” lililo chini ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwenye Maonesho ya Kimataifa ya Wakulima 2023 (Nanenane) yanayofanyika katika viwanja vya John Mwakangale jijini Mbeya. (01.08.2023)

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni