Nav bar

Alhamisi, 24 Agosti 2023

KIKAO CHA MAANDALIZI YA MKUTANO JUKWAA LA MIFUMO YA CHAKULA BARANI AFRIKA (AGRF) WAFANYIKA.


Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi kutoka Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Prof. Riziki Shemdoe, akizungumza Mjini Unguja kuelekea mkutano wa Jukwaa la Mifumo ya Chakula Barani Afrika (AGRF) utakaofanyika nchini Tanzania kuanzia tarehe 5 hadi 8 Mwezi Septemba 2023, ambapo amewataka wajumbe wa kamati ya maandalizi ya kitaifa kutoka Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kuhakikisha wanafanya maandalizi yote kwa ufasaha ili kufanikisha mkutano huo. Katibu mkuu huyo amebainisha hayo wakati wa kikao cha tatu cha maandalizi kuelekea mkutano wa Jukwaa la Mifumo ya Chakula Barani Afrika (AGRF). (21.07.2023)



Waziri wa Kilimo, Umwagiliaji, Maliasili na Mifugo kutoka Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mhe. Shamata Shaame Hamis akizungumza Mjini Unguja, wakati akifungua kikao cha tatu cha maandalizi ya mkutano wa Jukwaa la Mifumo ya Chakula Barani Afrika (AGRF) utakaofanyika nchini Tanzania kuanzia tarehe 5 hadi 8 Mwezi Septemba 2023, ambapo amewaambia wajumbe wa maandalizi ya kitaifa kutoka Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kufanya maandalizi vyema ili kuhakikisha mkutano huo unafikia malengo yaliyokusudiwa kwa kuwa utashirikisha marais kutoka nchi mbalimbali pamoja na wadau wengine. (21.07.2023)


Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo, Umwagiliaji, Maliasili na Mifugo kutoka Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Bw. Seif Shabaan Mwinyi akifafanua Mjini Unguja namna kamati ya maandalizi ya kitaifa kuelekea mkutano wa Jukwaa la Mifumo ya Chakula Barani Afrika (AGRF) utakaofanyika nchini Tanzania kuanzia tarehe 5 hadi 8 Mwezi Septemba 2023, ilivyojiandaa katika upande wa Zanzibar kuhakikisha wageni wakati wa mkutano huo wanapata pia fursa ya kutembelea vivutio mbalimbali vilivyopo kisiwani humo. Katibu mkuu huyo amebainisha hayo wakati wa kikao cha tatu cha maandalizi kuelekea mkutano wa Jukwaa la Mifumo ya Chakula Barani Afrika (AGRF). (21.07.2023)


Mkurugeni Mtendaji wa Jukwaa la Mifumo ya Chakula Barani Afrika (AGRF) Bw. Amath Pathe Sene akifafanua kwa kina namna AGRF ilivyojiandaa na mkutano wake nchini Tanzania utakaojumuisha wageni kutoka nchi mbalimbali wakiwemo marais, Bw. Sene ametoa ufafanuzi huo Mjini Unguja wakati wa kikao cha tatu cha maandalizi ya mkutano huo kikijumuisha wajumbe wa maandalizi ya kitaifa kutoka Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar. Mkutano wa AGRF utafanyika nchini Tanzania kuanzia tarehe 5 hadi 8 Mwezi Septemba 2023. (21.07.2023)


Wajumbe wa kamati ya maandalizi ya kitaifa kuelekea mkutano wa Jukwaa la Mifumo ya Chakula Barani Afrika (AGRF) kutoka Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar wakiwa Mjini Unguja, kwenye kikao cha tatu cha maandalizi ya mkutano wa AGRF utakaofanyika nchini Tanzania kuanzia tarehe 5 hadi 8 Mwezi Septemba 2023, ambapo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ataongoza mkutano huo. (21.07.2023)

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni